Rais Samia: Nani atazikwa na hela?

Rais Samia: Nani atazikwa na hela?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ni kauli fupi sana lakini nzito kwelikweli. Akionyesha kukerwa na majizi Rais Samia aliitoa kauli hii. Majizi yote hakuna linalolala kwenye vitanda viwili, vyumba viwili wala kula sahani mbili za ugali kwa wakati mmoja, wanaiba na kurundika pesa ambazo wataziacha wakati wakifa.

Pesa hizo mara nyingi ndio zinageuka chanzo cha vifo vyao kwanjia ya kisukari, shinikizo kubwa la damu, uzito mkubwa, ugonjwa wa ini na figo, kansa, ajali za magari, ukimwi na msongo wa mawazo. Na mara nyingi fedha hizo huwa ama zinapotea au kugeuka pia kuwa chanzo cha laana na vifo kwa watoto, ndugu na wajukuu atakaowaacha. Ni heri ya mtu aliacha mti mmoja wa kivuli kwenye uwanja wake wa nyumba kuliko yule aliyeacha mabilioni ya fedha kwenye vihenge na bank.

Nimuombe tu mama yetu atengeneze katiba nzuri yenye meno kabla hajaondoka madarakani. katiba "nzuri" kwangu ni katiba ambayo:
1. Inaondoa kinga ya kushitakiwa kwa wezi wote wa mali ya umma
2. Unatoa njia rahisi ya kumuondoa kiongozi wa ngazi yoyote ambae ni mwizi au mbadhilifu.
3. Inatoa adhabu kubwa sana ya kunyonga au inayokaribia na kunyonga
4. Inatoa dira na mwelekeo wa taifa kwenye uchumi, afya, elimu, chakula na ulinzi.

Mali za Nchi haziwezi kulindwa kwa ukali wa mtu mmoja, bali kwa katiba na taasisi zenye nguvu na meno ya kuzilinda.
 
Yaan hizi kauli haziwez mfanya mwizi aache kuiba .

Mama kama anataka kua Mtume, aanzishe Msikiti awe Mtume huko !!.

Mwanadamu ameumbwa kupewa Adhabu ili abadilike..

Hivi kama Yesu mwenyewe alipigwa misumali na wanazengo licha ya kwamba aliponya viwete, alifufua, na waliona kabisa Kwa macho, ila bado wakamuua,

Sembuse Hela ?? Hela ??? .
 
Sembuse Hela ?? Hela ???[emoji23]
 
Kwani hizi kauli ndo mbadala wa adhabu kwa mujibu wa sheria pale mwizi anapothibitishwa na maakama? Samia hana mtindo wa kuadhibu jukwaani.
 
Ni kauli fupi sana lakini nzito kwelikweli. Akionyesha kukerwa na majizi Rais Samia aliitoa kauli hii. Majizi yote hakuna linalolala kwenye vitanda viwili, vyumba viwili wala kula sahani mbili za ugali kwa wakati mmoja, wanaiba na kurundika pesa ambazo wataziacha wakati wakifa.

Pesa hizo mara nyingi ndio zinageuka chanzo cha vifo vyao kwanjia ya kisukari, shinikizo kubwa la damu, uzito mkubwa, ugonjwa wa ini na figo, kansa, ajali za magari, ukimwi na msongo wa mawazo. Na mara nyingi fedha hizo huwa ama zinapotea au kugeuka pia kuwa chanzo cha laana na vifo kwa watoto, ndugu na wajukuu atakaowaacha. Ni heri ya mtu aliacha mti mmoja wa kivuli kwenye uwanja wake wa nyumba kuliko yule aliyeacha mabilioni ya fedha kwenye vihenge na bank.

Nimuombe tu mama yetu atengeneze katiba nzuri yenye meno kabla hajaondoka madarakani. katiba "nzuri" kwangu ni katiba ambayo:
1. Inaondoa kinga ya kushitakiwa kwa wezi wote wa mali ya umma
2. Unatoa njia rahisi ya kumuondoa kiongozi wa ngazi yoyote ambae ni mwizi au mbadhilifu.
3. Inatoa adhabu kubwa sana ya kunyonga au inayokaribia na kunyonga
4. Inatoa dira na mwelekeo wa taifa kwenye uchumi, afya, elimu, chakula na ulinzi.

Mali za Nchi haziwezi kulindwa kwa ukali wa mtu mmoja, bali kwa katiba na taasisi zenye nguvu na meno ya kuzilinda.
Kauli za mtu aliyekata tamaa
 
Yaan hizi kauli haziwez mfanya mwizi aache kuiba .

Mama kama anataka kua Mtume, aanzishe Msikiti awe Mtume huko !!.

Mwanadamu ameumbwa kupewa Adhabu ili abadilike..

Hivi kama Yesu mwenyewe alipigwa misumali na wanazengo licha ya kwamba aliponya viwete, alifufua, na waliona kabisa Kwa macho, ila bado wakamuua,

Sembuse Hela ?? Hela ??? .
[emoji102][emoji848]
 
Rais amekiri Kuna WAPUMBAVU wamejipenyeza Hadi nafasi nyeti kabisa za kufanya maamuzi,

Wamefikaje hapo? Kwann anavumilia kufanya KAZI na wapumbavu?

Anaenda kukopa akileta zinaibwa.

Bado safari ni ndefu.
[emoji102][emoji102][emoji102][emoji102]
 
Kwa kauli hiyo ni kama Rais amesha surrender kwa wezi, sasa ameamua kuwapa maneno ya upole ili waingiwe na huruma waache kuiba.

Hataki kutumia sheria zilizopo kuagiza vyombo vya usalama viwakamate wahusika wahojiwe, na hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Kwa kauli hiyo, sasa ni rasmi Rais anawalinda au kuwaogopa wezi.
 
Hakika, tunahitaji Katiba imara sana
Katiba Mpya peke yake haitakuwa suluhisho, kama hapatakuwepo na nia ya dhati kufuata sheria kati ya mtawala na watawaliwa..
 
Yaan hizi kauli haziwez mfanya mwizi aache kuiba .

Mama kama anataka kua Mtume, aanzishe Msikiti awe Mtume huko !!.

Mwanadamu ameumbwa kupewa Adhabu ili abadilike..

Hivi kama Yesu mwenyewe alipigwa misumali na wanazengo licha ya kwamba aliponya viwete, alifufua, na waliona kabisa Kwa macho, ila bado wakamuua,

Sembuse Hela ?? Hela ??? .
Ni kweli. Kwanza hiyo ni kauli ya kuonyesha kushindwa. Mwizi hatishiwi bali anakamatwa na kuadhibiwa.
 
Back
Top Bottom