Earthmover
JF-Expert Member
- Sep 28, 2012
- 24,977
- 23,799
Kesho yetu ni ngumu kuliko jana...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Atatoboa mapema kabisaaa saa tatu na nusu asubuhiKwenye uchaguzi ulio wa huru na haki, Samia hatoboi.
Hata mie sijaelewa nani anatakiwa kufunzwa Katiba kati yetu na wao wanaoiyekeleza Katiba. Kuna mambo hayatakiwi kutamkwa hadharani na mojawapo ni hilo nililisikia jana. Nikisema hivyo wale wajiita chawa wa Mama wataniita CHADEMA. Hii ndiyo namna yao ya kusitisha kufikiri. Tumwombe Mungu.Kauli ya rais kuiita katiba " ni kitabu tu" inadhihirisha viapo wanavyoapa waingiapo madarakani si ya dhati toka moyoni. Rais anatakiwa kuilinda katiba kama asemavyo wakati wa kiapo.
Watanzania upo ulazima wa kuhakikisha kuwa katiba ijayo inatuwezesha kumfungulia mashitaka rais kwa kukiuka katiba ili katiba iheshimiwe na wananchi wote bila kujali vyeo.
Wa kulaumiwa ni JPM Mungu amlipe anayostahiki. Mabeyo alihakikisha katiba inafuatwa. UsijisWa kulaumiwa ni jenerali Mabeho aliyewagomea wale waliokuwa wanamjua vizuri kuwa ni inept, hawezi kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Mafisadi wanampenda kwa sababu wanaendesha wizi wao bila kuguswa. Lake oil
Sisi wengine tuliona hili miaka mingi iliyopita.Duh...!.
P
Nchi gani hizo zenye maendeleo makubwa na hazina katiba?Sijasoma yote coz nimeona bandiko lako ni msukumo wa chuki uliyoifuga ndani ya nafsi yako,
Hivi unajua kua kuna nchi zina maendeleo makubwa na hazina hiyo katiba? Jipe muda tumia simu yako kujua ni nchi gani hazina hata hiyo katiba ila zina maendeleo makubwa sana.
Kwani haya maoni yako uliyoyaweka hapa kuna mtu amekutafuta na kukuuliza?Ulinitafuta kuniuliza maoni yangu na nikakuambia kinyume na nisemavyo hapa?
Hajui kuwasiliana na hadhira anapoongea, huyo ni level za mkuu wake wa mkoa wa Dar ChalamilaAliongea pumba tupu!
Uliziona nyuso za Mwamakula na Warioba kamera zilipowaonyesha?
Samia hana hata uwezo wa kujistukia kuwa anachoongea ni pumba.
Mimi sina akili nyingi. Ila nina akili za kutosha walau kujistukia kuwa ninachokiongea ni pumba na hivyo ni bora kunyamaza tu.
Samia hata uwezo huo hana.
Sasa ulichouliza kina mantiki gani?, Nikikutakana na huyo Taos wako ntaonekana mgomvi?.Katiba
Wewe kweli ni Nyani,Nchi gani hizo zenye maendeleo makubwa na hazina katiba?
Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.
Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.
Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.
Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.
Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.
Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.
Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.
View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo
Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?
Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?
Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?
Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.
Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?
Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.
Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.
Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!
Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].
Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.
Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.
Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.
Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?
Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?
Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?
Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?
Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.
Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.
Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.
Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.
Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.
Umeelewa ninachozungumza hapa mkuu?Hata wewe hujui maana ya katiba Mpya kwa nchi yetu! Laiti ungejua, usingemuona mama hajui.
Naona kama amefuzu sawa na JK pale alipoifutilia mbali hoja ya katiba Mpya.
Kwa kukusaidia, lengo kuu la katiba Mpya ni kuondoa madaraka makubwa ya Rais. Fikiria Nani anaweza kukubali wakati ashasema 2025 anagombea!!!!! Hivi nani hajui kuwa CCM inashinda kwa kuiba kura? Akubali uchaguzi huru ili awe mpinzani?
Kweli hamjui maana ya katiba Mpya tukubaliane
Na bendera ya taifa ni kitambaa tu! Uje utembee wakati inashushwa ndipo utaijua.Hivi katiba siyo kitabu?
Jjiwe AlikuNi remote tuu hiyo, hamna rais hapo.
Kabisa,huyo au hao tatizo ni dini ya rais wasasa tuhWewe kweli Nyani..na ule msemo wa Nyani haoni kundule una kufaa kabisa.
Nyuma tu hapa Shujaa wetu alitamka kabisaa kuwa haoni umuhimu wa Katiba mpya na akafifisha mijadala yote na hata pale mlipotingisha kibiriti cha UKUTA nyote mliufyata. Sikupata maoni yako kuwa Jiwe ndio Raisi mwenye uwezo mbovu kabisa!
Au pale alipokataa kutoa rambi rambi na kuchangia chakula kwa wahanga wa Ukame akatoa kauli kuwa kwani yeye ndo ameleta tetemeko.
Nyani Ta'ddab! Hata kama humpendi huyo ndo Raisi wako acha dharau na maneno ya shombo! Hovyo kabisa wewe mtu!
kwani wewe hili swali lako hapa kuna mtu aliyekutafuta na kukuomba uje kuniuliza?Kwani haya maoni yako uliyoyaweka hapa kuna mtu amekutafuta na kukuuliza?