Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.

Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.

Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.

Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.

Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.

Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.

View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo

Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?

Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?

Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?

Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.

Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?

Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.

Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.

Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!

Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].

Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.

Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.

Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.

Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?

Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?

Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?

Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?

Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.

Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.

Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.

Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.

Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.

Hata Hilo la Elimu Si Kweli kuwa hatujui Katiba,

Kabla ya time ya Warioba kukusanya maoni, zilidurufiwa nakala za Katiba hii na tulipata muda kuusoma ktk makundi mbalimbali.

Kwann hataki tuanzie Rasimu ya Warioba kama msingi wa kuendelea mbele?
 
Tatizo sio katiba mpya bali tatizo wanao force hiyo katiba mpya hawana uelewa na katiba iliyopo sasa hivi. Katiba hii tuliyonayo ni the best na ndiyo inafanya Nchi itawalike. Japokuwa hujagusia kuhusu katiba ya kenya ambayo mnaiita ya "kidemokrasia" imewasaidia nini zaidi ya kufanya Nchi isitawalike kila kitu kinachofanywa na serikali kila raia anapinga mahakamani ndiyo nini?

Lengo la watu wanao force katiba mpya ni kupata nafasi za uongozi kwani hata katiba hii hawajui mazuri yake
 
Kauli ya rais kuiita katiba " ni kitabu tu" inadhihirisha viapo wanavyoapa waingiapo madarakani si ya dhati toka moyoni. Rais anatakiwa kuilinda katiba kama asemavyo wakati wa kiapo.
Watanzania upo ulazima wa kuhakikisha kuwa katiba ijayo inatuwezesha kumfungulia mashitaka rais kwa kukiuka katiba ili katiba iheshimiwe na wananchi wote bila kujali vyeo.
 
Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.

Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.

Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.

Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.

Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.

Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.

View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo

Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?

Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?

Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?

Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.

Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?

Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.

Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.

Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!

Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].

Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.

Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.

Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.

Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?

Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?

Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?

Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?

Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.

Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.

Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.

Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.

Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.

View: https://x.com/KipepeComrade/status/1615532090593886208?s=20
 
Onyesha sehemu nilipokubali.
Hii quote haihusiani na hichi ninachoandika...

Umeongea kwa uchungu sana legend...na point tupu...

japo uko ughaibuni... unaonyesha nini maana ya uzalendo halisi.

Kiukweli Tanzania kama kuna janga kubwa lililowahi kutupata...

basi halizidi janga hili la kuwa na raisi wa hovyo! Kabisa tangu Taifa hili kuundwa.
 
Hatari nikuwa watendaji wakuu wote sio big and smart brains... Golden boys/girls huwa excellent toka ngazi za chini mpaka vyuo vikuu!!
Sasa tizama,
R sa100 - alifeli fomfoo akaenda somea ukarani baadae akaunga unga kiujanjajanja vyuo vyajuu
W/M kasim - alifeli fomfoo akaenda ualimu wa praimari baadae akaungaunga kiujanja ujanja vyuo vyajuu
NW/M doto - alifeli fomfoo akaenda ualimu praimari badae akaunga unga kiujanja vyuo vyajuu.
Kazi tunayooo, wataacha kugawa mabandar hawa bila kikomo!!
Kisha wanatumia pesa ya wizi wa mali za umma kununua Phd fake
 
Wa kulaumiwa ni jenerali Mabeho aliyewagomea wale waliokuwa wanamjua vizuri kuwa ni inept, hawezi kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Mafisadi wanampenda kwa sababu wanaendesha wizi wao bila kuguswa. Lake oil
Mkuu how about CCM? How about Magufuli? CCM ndiyo walimpendekeza kama chama. Na Magufuli alishajua uwezo wake hivyo 2020 angeweza kumtema.
 
Kama huwa huelewi kwa nini watu wanakuwa tagged kwenye comment kama hivi..

Usiwe una andika ujinga na upumbavu wako kama hivi.

Labda niku elimishe, kwa nyuzi za walimu usishangae kuona member Mpwayungu village Kawa tagged,nyuzi za mahusiano member Deepond, nyuzi za Mungu Kiranga, nyuzi za mbususu mzabzab.

Wacha kukurupukia vitu usivyo elewa.

Hapa JF hatujuani.
Huyo ni mumeo!
 
Hujamsikiliza vizuri Mheshimiwa Raisi, unachomoa tu kaneno kamoja kisha unakimbia nacho kama kuku aliuekatwa kichwa.

Haters Kila wakati mnatafuta Cha kuzusha. So pathetic.
 
Back
Top Bottom