Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.

Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.

Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.

Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.

Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.

Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.

View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo

Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?

Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?

Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?

Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.

Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?

Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.

Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.

Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!

Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].

Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.

Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.

Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.

Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?

Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?

Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?

Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?

Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.

Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.

Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.

Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.

Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.

Katiba ndiyo imeleta maendeleo china, Malaysia, marekani nk!?
 
CCM ile brain kubwa hua inakaa nyuma kufaidi mema ya nchi. Halafu wale hohehahe ndio wanapewa nafasi za uongozi ili wajione nao ni kitu. Matokeo yake ndio hayo ndugu yangu. Yaani mtu mwenye hadhi ya raia namba moja anabeza umuhimu wa katiba kwenye maendeleo. Ni huzuni kubwa sana. Huyu mtu sasa tukisema uchumi umeshuka au umeoanda anaelewa chochote kweli?
Katiba haileti ugali mezani pako. Kenya hao wanakaribia mpya na bado kila siku wapo mabarabarani kulia lia manjaa na maisha magumu kila uchwao.
 
Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.

Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.

Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.

Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.

Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.

Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.

View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo

Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?

Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?

Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?

Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.

Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?

Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.

Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.

Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!

Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].

Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.

Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.

Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.

Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?

Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?

Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?

Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?

Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.

Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.

Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.

Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.

Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.

Haya maneno ya katiba kwamba ndo itakuletea ugali, mara nyingi huzungumzwa na hao machawa wa ccm wasiojua mbele wala nyuma , sasa naye Rais sijui imekuaje bila kujua nafasi yake katika taifa na kuingia mzima mzima, na mbaya zaidi bora umesema katiba yeye kasema kitabu aiseee hapana
 
Katiba haileti ugali mezani pako. Kenya hao wanakaribia mpya na bado kila siku wapo mabarabarani kulia lia manjaa na maisha magumu kila uchwao.
Wewe na anayesemwa hakuna tofauti. Kenya tatizo sio maisha magumu wala njaa. Wale ukabila ndio unawamaliza. Hayo mengine ni vichochoro tu, labda kama hujui siasa za Kenya.
 
Haya maneno ya katiba kwamba ndo itakuletea ugali, mara nyingi huzungumzwa na hao machawa wa ccm wasiojua mbele wala nyuma , sasa naye Rais sijui imekuaje bila kujua nafasi yake katika taifa na kuingia mzima mzima, na mbaya zaidi bora umesema katiba yeye kasema kitabu aiseee hapana
Kenya wana katiba mpya na bado wanalia kila kama panya kila siku barabarani .
 
Unataka kuniambia kuwa mama yako aliyekubeba Tumboni miezi Tisa ni dhaifu? Mama yako angekuwa dhaifu ungeqwzaje kukaa Tumboni kwake miezi tusa? Kwanini unakuwa na mawazo ya kibaguzi na chuki za kijinga zilizopofusha akili na uwezo wako wa kufikiri?
Kuwa dhaifu sio dhambi ni sifa, ni dhaifu kwenye suala la uongozi hususani wa jamii, mwanamke ni kiumbe anayepaswa kupewa favour sawa na mtoto si mtu wa kumtegemea kwenye maamuzi magumu yenye tija
 
Aliongea pumba tupu!

Uliziona nyuso za Mwamakula na Warioba kamera zilipowaonyesha?

Samia hana hata uwezo wa kujistukia kuwa anachoongea ni pumba.

Mimi sina akili nyingi. Ila nina akili za kutosha walau kujistukia kuwa ninachokiongea ni pumba na hivyo ni bora kunyamaza tu.

Samia hata uwezo huo hana.
Kwa hiyo warioba na mwamakula ndiyo kipimo chako Cha mtu kuongea mantiki!?..we mbona puto tu kichwani!!
 
Back
Top Bottom