Rais Samia naomba usimsahau Elia Wilinasi hata kwenye ukuu wa wilaya

Reread your post please

Temporary job as an inspector? Can I get that chance for my friend anywhere in this country?
Yes, Petroleum inspector, they usually deal with inspection of oil and gas cargoes in Ships and Depot at the Dar es Salaam port.
 
Tanzania hii ya sasa hivi wala hakuna vetting wala career development.

Teuzi zinategemea MTU MAARUFU UCHAWA, kwenye TV, UVCCM, kashimdwa kura huko CCM, alikuwa mpinzani akahamia kwenye chama.

In short, kuna possibility kwa Mtangazaji was TV anaemsifia Rais au Mwijaku na Steve Nyerere kuwa MaDC kuliko MTU makini anaejua kazi.
 
My friend achana na ujinga wa kusema ninavyomuelewa..huwezi kumuelewa mtu wewe kwa maneno tu..lete hapa kielelezo chochote kuonyesha anapenda kusaidia watu, Acha maneno..kwanza kwa haya unayoandika juu yake unamfanya aonekane hadi hapo alipofikia elimu aliyopata haijamsaidia kupata maarifa kusaidia wengine, haiwezekani mtu ni masters holder bado ni omba omba wa nafasi, huhitaji kufanya hivyo..hapo TPDC uwezo alio nao utaonekana, usifanye wote anaofanya kazi nao ni wajinga hawawezi kuona uwezo na vipaji vya uongozi kama anavyo..hiyo kazi aliyo nayo ndiyo kipimo cha uwezo wake katika mambo yote..unachofanya hapa ni kuleta fujo kutetea mtu wakati ana jukwaa kuthibitisha kama anastahili kuwa DC, na sijui kwa nini humuombei awe RC sababu kama ana uwezo ataonekana tu..tuache mambo ya namna hii, uongozi siyo zawadi..hebu funga huu mjadala, mwambie aitendee kazi fani aliyosomea kwanza haya mengine ya uDC yatakuja bila wewe kusumbua hapa na utetezi hauna kichwa wala miguu zaidi ya kuonekana wajinga na tegemezi..pse stop!
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri boss. Ila hajasema anafanya kazi TPDC, Ila ameandika kama sehemu yake ya uzoefu aliopitia. Pengine hapo alipitia kama internship boss ili kupata uzoefu. Hiyo inamaana kama angekua kaajiriwa hapo angekua kesha rudi hapo. Na kama unavyozijua sheria za utumishi haziruhusu mfanyakazi kushiriki siasa. Lakini hicho alichokiandika ni moja ya sehemu ya uzoefu wake, na ukisoma vizuri pale kunalimit yake yaani mwaka aliokomea.
Hivyo kama angelikua ni mtumishi sidhani kama angekuja kushiriki hoja za kisiasa hapa jukwaani. Nadhani hicho ndicho kinampatia confidence zaidi. Kuhusu swala la kuomba nafasi ya kulitumikia taifa lake tena kwa heshima bila makuu sidhani kama inamharibia maarifa aliyonayo rafiki. Tena mwenye elimu pamoja na kwamba anamaarifa ya kutosha lakini kujinyenyekeza mbele za viongozi wako sidhani kama ni jambo baya rafiki.
Nakuomba sana kaka yangu usimwelewe vibaya. Kusomea mambo ya sayansi au uhandisi ni kama education pass tu. Ila mwisho wa siku watu wengi hufanya kile wanachokipenda na kuwa na amani nacho.
 
Fanya kuelewa na wewe, usiitweze JF zaidi..unayemwambia amteue ndugu yako anakushangaa sababu ingefaa km ungemshauri ashiriki kugombea nafasi yoyote ndani ya chama wakati huu wa uchaguzi aonyeshe uwezo wake, usishawishi mteuzi aone km uDC ni nafasi za watu kufanyia majaribio ya uongozi..kwa umri alio nao km kweli ana kipaji cha uongozi angeshapita uvccm, bavicha au wing ya vijana kwa chama chochote tungeona hilo kwenye cv, na hivyo asingehitaji utetezi wako huko ndiko kunaonyesha mtu kuwa ana kiu ya kuwa kiongozi..usitushirikishe kuunga mkono utamaduni mbaya wa kutetea watu kupata uteuzi kupitia mitandaoni, hiki unachofanya hakifai kabisa, tuitumie JF kwa mambo ya kujenga zaidi, hata umri wake tu haumpi sifa kuwa DC usifanye watanzania ni jalala la kuwekewa viongozi hata wasiokuwa na sifa, ameshindwa nini kugombea nafasi hata ya ujumbe wa mkutano mkuu ndani ya ccm? Huyu km amesoma kweli hadi masters basi elimu yake ni sifuri hafai hata kuwa mtendaji wa kijiji..achana nae!
 
Boss ahsante sana kwa ushauri wako mzuri. Natumaini ataufanyia kazi kama ulivyo ufikisha. Pengine anajaribu nayeye kujipenyeza taratibu huwezi jua ya Mungu mengi boss.
 
Kuhusu swala la kuomba nafasi ya kulitumikia taifa lake tena kwa heshima bila makuu sidhani kama inamharibia maarifa yake ya masters aliyonayo rafiki. Tena mwenye elimu pamoja na kwamba anamaarifa ya kutosha lakini kujinyenyekeza mbele za viongozi wako sidhani kama ni jambo baya rafiki.
Nakuomba sana kaka yangu usimwelewe vibaya. Kusomea mambo ya masters ya sayansi au uhandisi ni kama education pass tu. Ila mwisho wa siku watu wengi hufanya kile wanachokipenda na kuwa na amani nacho.
 
Boss ahsante sana kwa ushauri wako mzuri. Natumaini ataufanyia kazi kama ulivyo ufikisha. Pengine anajaribu nayeye kujipenyeza taratibu huwezi jua ya Mungu mengi boss.
Kuna kanuni moja ya hesabu inasema..bora ndege mmoja uliye naye mkononi kuliko kukimbiza ndege wawili mwituni..ni rahisi kwake kutafuta kazi ya fani yake akapata kuliko kufukuzia uteuzi kupitia kwako.
 
Unachofanya hapa wala si kujinyenyekeza ni ujinga, wanaopitia uvccm kama wanachama au viongozi huko ndiko kujinyenyekeza..halafu haiwezekani unasoma hadi masters hujui kile moyo unapenda kufanya..kuelimika ni pamoja na kujua mapema vipaji ulivyopewa na Mwenyezi Mungu uvitumie, una masters halafu hujui areas of interest, lakin uwezo pia..si lazima kila unachokipenda una uwezo wa kukifanya..ndio maana ndugu yako hawezi hata kukumbuka kuwa kama anapenda siasa si angeanzia uvccm..sio kusubiri wewe umtetee apate uteuzi, kifupi siasa hawezi labda tumbo ndio linamdanganya apende siasa.
 
Kuna kanuni moja ya hesabu inasema..bora ndege mmoja uliye naye mkononi kuliko kukimbiza ndege wawili mwituni..ni rahisi kwake kutafuta kazi ya fani yake akapata kuliko kufukuzia uteuzi kupitia kwako.
Ahsante sana kwa ushauri mzuri boss
 
Ahsante kwa ushauri mzuri boss, natumaini hizi jumbe zimemfikia na atazifanyia kazi wakati akiendelea kujipanga.
 
Zamani enzi zetu ilikua ni ajabu sana kuona mtu anaomba apewe cheo. Lakini enzi hizi za walamba asali watu wamekosa haya wanajitokeza waziwazi kuomba wapewe teuzi. Serikali na chama mnakwama wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…