Rais Samia naomba usimsahau Elia Wilinasi hata kwenye ukuu wa wilaya

Rais Samia naomba usimsahau Elia Wilinasi hata kwenye ukuu wa wilaya

Kwako mama yetu Samia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natumai umzima wa afya njema na unaendelea na shughuli zako za kiofisi.

Mama, ndugu yetu Elia Wilinasi ni kijana safi mwenye weledi na mzalendo anayetamani kukitumikia chama cha mapinduzi katika ngazi za juu na taifa kwa ujumla.

Alichukua fomu ya kugombea ujumbe wa hamshauri kuu ya CCM taifa kama karata yake ya kwanza kulitumikia taifa lake.

Safari hii anasubiria mkeka wa ukuu wa wilaya kwa hamu, bado anatamani kulitumikia taifa katika ngazi ya ukuu wa wilaya.

Ahsante sana.
Kazi iendelee
Ukuu wa Wilaya sio ajira bali ni utumishi tu wa kisiasa.
Vijana wanakaa uwezo wa kufikiria umefika mwisho wanabaki kusubiri nafasi za uteuzi.
Ndiyo maana wengi wamekuwa watu wa kusifia na machawa tu.
Njaaa zimetoka tumboni zimehamia vichwani, Taifa halina critical thinkers bali kuna makuadi wa wanasiasa na watawala.
Tunazalisha taifa la hovyo sana mbeleni🥲🥲
 
Ukuu wa Wilaya sio ajira bali ni utumishi tu wa kisiasa.
Vijana wanakaa uwezo wa kufikiria umefika mwisho wanabaki kusubiri nafasi za uteuzi.
Ndiyo maana wengi wamekuwa watu wa kusifia na machawa tu.
Njaaa zimetoka tumboni zimehamia vichwani, Taifa halina critical thinkers bali kuna makuadi wa wanasiasa na watawala.
Tunazalisha taifa la hovyo sana mbeleni🥲🥲
Boss lakini sio wote. Wengine wana wito tu wa kuongoza ili kutatua matatizo mbalimbali yanayolikumba taifa letu.
 
Boss lakini sio wote. Wengine wana wito tu wa kuongoza ili kutatua matatizo mbalimbali yanayolikumba taifa letu.
Sasahivi ana nafasi gani ya kiutumishi?
Kama ana wito na anayo nafasi tayari ya kiutumishi na ameitendea haki basi, anastahili kupanda ngazi inayofuata ili aonyeshe zaidi uwezo wake.
ALL in All tuombeane Mema na Kheri.🙏🙏🤣
 
Sasahivi ana nafasi gani ya kiutumishi?
Kama ana wito na anayo nafasi tayari ya kiutumishi na ameitendea haki basi, anastahili kupanda ngazi inayofuata ili aonyeshe zaidi uwezo wake.
ALL in All tuombeane Mema na Kheri.🙏🙏🤣
Amen boss
 
Political Journey:
Elia Wilinasi (born 25 December 1991) is a Tanzanian young man with more interest in politics. He was a petroleum engineering researcher from 2019 to 2022 at the China University of Geosciences, China. He also served as the Natural Gas Process Engineer at Tanzania Petroleum Development Corporation, TPDC, at Madimba natural gas processing plant from 2017–2019. In 2014 and 2015, he served as a petroleum inspector and petroleum quality control and assurance officer at Intertek Testing Services Ltd., Dar es Salaam, Tanzania.

His political interests started when he was in class five in 2005. During that period, Elia joined his mother to campaign for councilors and parliamentary candidates. His mother always wanted her son to be a politician. His mother started serving the CCM party in 2000. She served the party as chairperson, member, and campaign manager of various parliamentary candidates in her territory until December 18, 2015, when she died in a car accident. Elia's mother was buried with CCM flags as an honor she earned for serving the party with great diligence and professionalism throughout her life. In 2017, Elia decided to take an active interest in politics in order to honor her mother in action as a reward for the work she did for the CCM party.

Education:
Between 2000 and 2006, Elia attended Igamba Primary School in the Songwe Region. After primary, Elia attended Igamba Secondary School for his O-level, which took place between 2007 and 2010. Then he moved to the Iringa Region and studied at the Ifunda Technical High School for his advanced level education, taking PCM combination. He graduated from the University of Dar es Salaam in 2017 with a degree in Petroleum (Oil and Gas) Engineering. In 2019, Elia was awarded a scholarship by the Tanzania Ministry of Energy and the Chinese Government to study for a Master's degree. He graduated from the China University of Geosciences in 2022 with a degree in Oil and Natural Gas Engineering.

Research and publication journey:
Elia has authored a number of research articles, including one on the optimization of natural gas production system constraints to extend the plateau rate of a conceptual gasfield. Another is on the design of a MATLAB kerogen classification toolbox (MKCT) for the characterization of hydrocarbon source rocks in the MATLAB software programming language environment. He has also authored an article on using Material Balance to Design an Artificial Neural Network Machine Learning Regression Model for Predicting the Performance of Tangawizi Dry Gas Reservoir in Tanzania’s Block 2 Offshore Field, and an article on using black oil modeling to build a conceptual hydrocarbon reservoir model for comparing the oil production performance of vertical and horizontal wells.

Training and workshops:
Elia has attended several international conferences, exhibitions and national training. In December 2021, he attended the 3rd edition of Indian Infrastructure's Small Scale LNG (ssLNG) and Storage in Oil and Gas in India. He attended the Tanzania-Uganda Oil and Gas Symposium (TUOG), Enhancing the Private Sector, hosted by the Tanzania Ministry of Energy and Mineral Development in November 2021.In November 2021, he attended the Earth Energy Environment Conference at Marietta College, Ohio, USA. In May 2012, he attended Architectural Designs by the International Symposium on Computer Architecture (ISCA). In December 2020, he attended a Training Programme for Engineering Science and Technology Development by the International Knowledge Centre for Engineering Sciences and Technology (IKCEST). In Feb 2021, he attended Refinery and Petrochemical Training by the Petroleum Engineers Association (PEA) in India. In Feb 2021, he attended Dynamic Reservoir Simulation Modelling using Software Training by PEA in India. In October 2016, he attended the 4th Tanzania Oil and Gas Conference and Exhibitions (TOGaCE) organized by MEM, TPDC, EWURA, and other petroleum companies. In February 2016, Elia attended One Subsea Oil and Gas Workshop by One Subsea. In February 2015, Elia attended an oil and gas workshop by Statoil. In October 2014, Elia attended the 3rd Tanzania Oil and Gas Conference and Exhibitions (TOGaCE) organized by MEM, TPDC, EWURA, and other petroleum companies. In Jul-Sep 2013, Elia attended 50 Years of Nation-Building Army (JKT) "Jul-Sept 13" 821KJ in response to the law by JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) 821KJ Bulombora, Kigoma.
Under which qualifications that Elias served that post mentioned above between 2014-2015?
 
Boss lakini sio wote. Wengine wana wito tu wa kuongoza ili kutatua matatizo mbalimbali yanayolikumba taifa letu.
Sasa mtu alisomeshwa masters na serikali bado anarudi kuomba uDC tena, nadhani serikali inahitaji utaalam wake zaidi kwenye fani aliyosoma, kusema tu anapenda siasa haitoshi kumfanya awe DC wote wanaosoma wakisema hivyo nani atabaki kwenye fani walizosomea? Kama ameajiriwa TPDC bado ana nafasi ya kutumikia taifa lake kuliko kutaka siasa..hiyo sasa ni tamaa na ubinafsi unamsumbua, nafasi za uteuzi aachie wengine wateuliwe yeye atumie ujuzi wake aliosomeshwa na serikali..
 
Kwako mama yetu Samia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natumai umzima wa afya njema na unaendelea na shughuli zako za kiofisi.

Mama, ndugu yetu Elia Wilinasi ni kijana safi mwenye weledi na mzalendo anayetamani kukitumikia chama cha mapinduzi katika ngazi za juu na taifa kwa ujumla.

Alichukua fomu ya kugombea ujumbe wa hamshauri kuu ya CCM taifa kama karata yake ya kwanza kulitumikia taifa lake.

Safari hii anasubiria mkeka wa ukuu wa wilaya kwa hamu, bado anatamani kulitumikia taifa katika ngazi ya ukuu wa wilaya.

Ahsante sana.
Kazi iendelee
KUVAA VIZURI NA KUJICHEKESHA HOVYO SIO ISHARA YA UELEWA.

Wanaccm ni lazima tujikumbushe kila mara
Tuna jukumu la kuiongoza nchi hii na kuisimamia Serikali ili iweze kuitekeleza ilani ya CCM 2020 ambayo ni mkataba Kati yetu CCM na Wananchi.
Ili tufanikiwe ni lazima tuwachague Viongozi wenye Uelewa Mpana na wenye Maono Makubwa.

Viongozi Aina hiyo tunao wengi nchini ila maisha wanayoyaishi wamezungukwa na watu walio wengi wajinga kabisa ambao nyakati za Uchaguzi huleta mizaha na ushabiki wa kipumbavu ambao Matokeo ya hayo hupelekea kupenya watu wasio na sifa za Uongozi na Matokeo yake Viongozi hao Maboya huonekana vituko mbele ya Viongozi wa Serikali ambao Viongozi hao wa Serikali Daima Wana viapo vya uhakika na hulazimika kuishi wakisimamiwa na baadhi ya Viongozi wenye Uelewa Mdogo ambao viapo vyao huwa ni Danganya toto .
Pia history ya baadhi ya Viongozi wa Chama husomeka walivyopatikana kwa Rushwa ila wao huwa Makauzu hujitoa *Ufahamu na kujifanya na wao wanakemea* Rushwa ilihali wao wametokana na Rushwa.
Ifikie Mahali Wanaccm tujielewe tuache kutumika na kushangilia Mambo ya hovyo hovyo.

Wasomi wa Serikalini baadhi wanatushangaa na wanasikitika hata Post tunazo Post kwenye Magroup hasa kwa kuzingatia Sisi ndiyo watawala.

Ni lazima Sasa tuanze kuwakabili watu wajinga wajinga pale wanapopotosha Raia
NI kwa kufanya hivi tutakuwa pia tunayatekeleza Mapenzi ya Mwenyezi Mungu anayetutaka kutumia Uelewa wetu kuwasaidia wasio jielewa.

Nakumbuka Tarehe 22/08/2021
Askofu Dkt Josephat Gwajima alisema,

" Mimi kumkabili mtu Mjinga Mjinga , nimeambiwa hivyo na Mungu.
Akitokea mtu Mjinga Mjinga mkabili hasa anayechezea Mungu na nguvu zake..

Wanaccm tukibahatika tukakuza Uelewa tukakataa kutumikishwa na kufikiri kwa mizani ya njaa zetu naamini kabisa hata Sisi hatutakuwa Omba Omba na kuishi kwa kutegemea huruma za Viongozi Baadhi walio kwenye Vyombo vya Dola ambao wakinuna TU Sisi huku na familia zetu tunachanganyikiwa na kutafuta umbea wa kuwapelekea ili wacheke walau kidogo ili nasi familia zichangamke.

🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔

Tubadilike turudi kwenye malengo mapana ambayo Wananchi wenzetu Makapuku wenzetu walituamini na tukakubaliana nao kupitia ilani.

Nakumbuka Tarehe 07 / July/2021
Comrade Kanali Mstaafu
Mheshimiwa Ngemela Lubinga .
Katibu NEC Siasa na Mahisiano ya Kimataifa
Alisema,

" Kazi kubwa tunayokuja kufanya ni kusimamia ilani kwamba tulipoingia Madarakani tuliwaomba Wananchi kura .
Tukisema tutatekeleza hili tutatekeleza hili, tutatekeleza hili, Sasa tunataka kuona je, hayo yanatekelezwa?"

Mwisho wa kunukuu

Tusome Kitabu cha Ilani ya CCM 2020 uk 01 ibara 04 na uk 161-168.

Ili Mambo yaende ni lazima Muhali tuuweke pembeni , tuchukuwe kila hatua inayostahiki ikiwa ni Pamoja na kuto wachagua Viongozi wenye Uelewa Mdogo
Ambao baadhi yao wanapenya kwa Rushwa Kisha kulindwa kwa nguvu zote na baadhi ya Viongozi Wasio Waadilifu kwa visingizio vya kikao ambavyo hufanya Maamuzi vikiwa na Chuki Binafsi na Mitazamo hasi uliogandana na Uelewa finyu .
Katiba Kanuni Miongozo na Taratibu zetu zinaelekeza wazi na ziko wazi ila zinasiginwa kwa sababu ya baadhi ya Viongozi wetu walio na Uelewa finyu ambao baadhi yao walipata Uongozi huo kwa Rushwa na walio kosa lishe kwenye ubongo wao.
Watu wameelekezwa Sana watende haki kwa kufuata katiba Kanuni Miongozo na Taratibu ila kwa ukosefu wa lishe baadhi wamekuwa wakifikiri kwa kuwaza matumbo yao. NA faida wajipatazo kwa Rushwa ya kuwapitisha Wagombea Maboya kwa Maelekezo ya Viongozi wenye Fedha na kuwakata wote wenye Uelewa Mpana na ambao wangukuwa chachu ya kukiimarisha Chama.
Nakumbuka Tarehe 30/09/2022
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan
Katika Mkutano wa Mwaka wa Tathmin ya Sita ya mkataba wa lishe September 30, 2022
Alisema,

" Ndiyo Yale aliyoyasema , nadhani Waziri Ummy, tunagombana huko TAMISEMI huko Chini, hata huko juu Serikalini.
Unamuelekeza mtu kitu mara nne , mara tano,hata hakimuingii.
Unamuuliza Dharau !?,
Jeuri !?, Hutaki !?
Kumbe Maskini hujuwi historia yake.
History yake imefichwa na suti na tai aliyoivaa.
Inawezekana kabisa maanake unasema ahaa, mbona mi naona hapa Kuna tatizo!?"
"Naona (Matatizo) moja , mbili, tatu, hivi inakuwaje huyu niliyemuamini hapa (Yeye haoni )!?"
"Haoni"
"Haiwezekani"
" Kumbe Kuna hayo ( ya Uelewa Mdogo na ukosefu wa lishe)"
"Tuna watu lakini sio Raslimali watu."

Mwisho wa kunukuu

Naye Pastor Mmbaga
Wa Mahubiri TV
Tarehe 26/12/2020
Aliwahi kusema,

"Sasa mnisamehe Sana Kama hii sentence itawakwaza"
" Kuna watu mtaishia kuwa Wapishi wa (watu) wengine (kwa) maana hamjiongezi
"(Kwa sababu ya ) Ufahamu (Mdogo)"
" Pata Maarifa , na kinachozuia tusipate Ufahamu ni ka Roho kale ka Nini!?
"Wivu , korosho "
" Yaani korosho ilivyo tamu lakini watu wakasema eti ( mtu) ana Roho ya korosho wakati korosho NI tamu!?"
Tubadilishe TU , tuite (Roho) ya ndoano ".

Mwisho wa kunukuu

Tuzaliwe Upya Kifikra Uongozi sio kuvaa nguo zilizo kolea kijani na nyeusi huku tukiwa hatujielewi tunatumikishwa na kujionyesha kuwaponda wanaotupatia Uelewa ili tukalipwe vihera kwa wenye hela za Rushwa.

Tusome Kitabu cha Katiba ya CCM 1977 Toleo 2020 ibara 15(3)(4)(6)(7) , Ibara 12(1)(a) ili tukasome uk 151 vifungu 1,3,6 na 8.

Nakumbuka Tarehe 28/10/2021
Comrade Humphrey Polepole
Akiwa Mbunge
Aliwahi kusema,

" Leadership is the ability to develop a Vision that motivate others to move with a passion towards a common goal."
Mwisho wa kunukuu.

Tuache kucheka check kwenye Mambo yanayoweza kuathiri jitihada za kulisongesha Taifa letu mbele.





Kidumu Chama Cha Mapinduzi






Mathias Mugerwa Kahinga
 
Sasa mtu alisomeshwa masters na serikali bado anarudi kuomba uDC tena, nadhani serikali inahitaji utaalam wake zaidi kwenye fani aliyosoma, kusema tu anapenda siasa haitoshi kumfanya awe DC wote wanaosoma wakisema hivyo nani atabaki kwenye fani walizosomea? Kama ameajiriwa TPDC bado ana nafasi ya kutumikia taifa lake kuliko kutaka siasa..hiyo sasa ni tamaa na ubinafsi unamsumbua, nafasi za uteuzi aachie wengine wateuliwe yeye atumie ujuzi wake aliosomeshwa na serikali..
Rafiki unazungumza maneno yenye mantiki sana. Ila kiukweli kwa navyomjua mtu wa kupenda siasa basi huyu bwana anapenda sana. Hizo kazi ulizo zielezea hapo kwa navyomwelewa japo nimekaa naye kwa muda mfupi hazimtoshi. Huyu ni mtu wa kupenda kusaidia kutatua matatizo ya jamii yake. Moyo wake ndio umekaa hivyo. Hivyo anatakiwa kukaa mahali ambapo atatatua shida za watu wa jamii yake moja kwa moja. Akiwa kwenye hizo kazi za professional anafanya kazi na machines tu.
 
Back
Top Bottom