Rais Samia ni dhaifu kulingana na mambo yanavyokwenda?

Rais Samia ni dhaifu kulingana na mambo yanavyokwenda?

Huyu mama yuko very ambitous kuipeleka nchi mbele na amejitahidi sana toka mwanzo, haya majanga ya kudorora kwa uchumi wa dunia kutokana na covid, vita ya ukraine, mabadiliko ya tabia nchi ambayo sasa yanaleta hali ya ukame kwenye nchi yanamharibia pakubwa. Kwa jinsi jamii zetu za kiafrika zilivyojijenga kwenye mfumo dume inaweza ikawa pia kikwazo kwa kiongozi mwanamama kuweza ku consolidate power na kutekeleza vision yake kwa uthabiti mkubwa.​
Ni kweli aisee mama ni ambitious huoni katujaza matozo ovyoovyo,nchi ina Mito na maziwa lakini tunalia uhaba wa maji na umeme,mfumuko wa bei wa ovyoovyo,ufisadi wa hatari. kwakweli mama ni ambitious aongeze bidii.
 
MAJIZI aliyoyatupilia mbali JPM, mama kayasogeza mezani. Unatarajia nini hapo.
Siku moja mtanikumbuka kwa mazuri, wala si kwa mabaya. By JPM, RIP, dad.
 
Wakuu habari za mchana?

Ni matumaini yangu kuwa mko poa,katika siku za hivi karibuni kumezuka mijadala kadhaa mitaani, katika mitandao na hata kimataifa kuwa uongozi wa Rais Samia umeghubikwa na sintofahamu nyingi hususan katika masuala muhimu na ya msingi yanayolenga maisha ya wananchi moja kwa moja amekuwa mzito kuchukua maamuzi sahihi na kwa wakati kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake ambapo pale inapoonekana wizara inalegalega katika utendaji waziri husika alikuwa anawajibishwa bila kupepesa jicho lakini kwa upande wake hali imekuwa tofauti kidogo

Mwanzo Wananchi waliona kama ukombozi umekuja kwa wakati sahihi ukizingatia hali ya kisiasa ambayo nchi ilipitia kayika miaka 5 nyuma. Aliitwa mponyaji na mleta maridhiano ya kitaifa na vyama vyote vya siasa nchini na tulishuhudia viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa vikienda Ikulu kuzungumza na mkuu na nchi hadi kuibuka msemo uliopendwa na kuvuma zaidi ya "Mama anaupiga mwingi"

Tulitegemea Wasaidizi wake wangemsaidia kushinda mechi tena mapema tu lakini hali imekua tofauti ghafla kwa Watazamaji na Mashabiki wa timu kwani wanaona kama timu yao inazidi kulemewa na hata zile pasi zilizokuwa zinapigwa mwanzo hazipigwi tena kwa kifupi sasa ule wimbo wa Mama anaupiga mwingi hausikiki tena siyo kwa Wananchi wala wale viongozi wa vyama vya siasa.

NINI KILICHOTOKEA?

Hali ya utendaji wa baadhi ya wizara imekuwa kikwazo mnoo kwa maendeleo ya jamii na uongozi wa Mama kwa ujumla mfano suala la umeme kwasasa limekua tatizo kiasi kwamba wananchi wa hali ya chini wanaotegemea umeme kuendesha shughuli zao za uchumi wameshajikatia tamaa ya kesho yao, tozo za miamala, vifurushi vya simu na mfumuko wa bei ya chakula kila uchwao nayo imekuwa tatizo kubwa

Kuna lingine limefukuta na tayari limeacha jeraha kubwa sana suala la maji ndani ya Jiji la Dsm angalau mafuta yameshuka bei kimtindo

Changamoto hizo hapo juu zinamgusa Mwananchi wa hali ya chini moja kwa moja na mbaya zaidi wananchi wanaona kama Mama kawasaliti na kawaacha peke yao baada ya Baba Kufariki hawana tena tumaini hawajui kesho yao itakuaje, wamejikatia tamaa kabisa hakuna anayejua mawazo ya mwenziye kwasasa ndani ya Nchi kila kitu hakishikiki na mbaya zaidi wananchi wanakerwa na matamashi ya baadhi ya viongozi kuwa yq kuudhi na kukera badala ya kuyafanyia kazi malalamiko yao.

Wakulima walia na bei ya mazao na gharama kubwa ya pembejeo mabadiliko ya hali ya hewa nayo inaendelea kusababisha ukame unaopelekea mifugo kufa wakulima kushindwa kulima kwa wakati na hawajui hatama yao itakuaje.

Nadhani jo kipindi ambacho wasaidizi wa Rais wangemsaidia zaidi Rais kutatua kero za wananchi badala ya kuwa na majibu ya danganya toto wakati utekelezaji ni mdogo.Hii inajenga picha ya kuashiria labda pengine Rais ni dhaifu au anawaogopa wasaidizi wake kwa maana hawezi kuwawajibisha pale wanapokosea ama la tumeona na kusikia mambo mengi yanayotokea kila siku na uzembe mkubwa wa baadhi ya watendaji wa Serikali katika kutimiza wajibu wao kwa dhamana waliyopewa ya kumsaidia Rais.

Kuna shida shida ipo mahala ni wakati sahihi sasa wa kumsaidia Rais kwajili ya mustakabali mzima wa Taifa na watu wake sababu siyo Rais tu anayeharibikiwa ila Watanzania kwa ujumla na vizazi vyetu.Hii ni sauti Mzalendo wa kawaida na haya ni maoni yangu tu kwa ufupi tunaipenda Tanzania yetu kwa moyo wetu wote bila kujali vyama,kabila,dini wala rangi.

Karibuni tuchangie Wakuu.
Ni muhimu tuache matumizi ya neno kumsaidia Rais, tutumie uwajibikaji na ufuatiliaji wa mamlaka, na kutumia neno Serikali zaidi, Madam Rais aachane na matumizi ya maneno na mazoea ya awamu ilopita. Kila kitu Rais Rais afanye kazi ofisi yake ni taasisi, mafaili hana ya wasaidizi? Kama hawatumi au haitaji baadhi ya taarifa unampa Kwa mlango upi, taasisi zipo ni yeye tu akae kitako asome mafaili na maarifa yake na uelewa wake na afikie maamuzi na mengi hupaswa kuwa consultative na opinionated resolutions na deliberations.

Kila mtu atimize wajibu wake.
 
Back
Top Bottom