Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Mama huyu anayefanya kazi ya kitume , kazi ya Sadaka ,kazi ya kujitoa na kujitolea Maisha yake kwa ajili ya kubadilisha maisha ya watanzania na kuleta matumaini kwa watu.
Huyu Mama yetu Mpendwa amejitoa na kujitolea Maisha yake kama Sadaka katika kuinua Maisha ya watu, ameutoa muda wake kuwatumikia watanzania usiku na mchana. Maisha yake ya kila siku na kila uchao yamekuwa kwa ajili ya watanzania.
Ni Jemedari Aliyejitoa pasipo kujibakisha wala kuacha akiba ya nguvu zake. Kila kitu ameelekeza kwa watanzania. akili yake ,jasho lake,maumivu yake ,upendo wake ,mipango yake, maono yake na Nguvu zake zote ameelekeza na kupeleka kwa watanzania bila kujibakisha kitu chochote kile wala sehemu yoyote ile.
Ndio maana unaona hakuna anayeachwa nyuma katika meza ya mafanikio. Ndio maana unaona akipandisha mishahara kwa watumishi wa umma katika viwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa Duniani, akiboresha mazingira ya biashara hapa Nchini, akitoa ajira kwa vijana ,akitoa mikopo ya riba nafuu kwa vijana ,akina mama na watu wenye ulemavu,akiinua maisha ya wakulima na kukifanya kilimo kuwa biashara na mengine mengi sana.
Watu na viongozi aina ya Rais Samia huwezi kuwapata wakati wote au wowote unaowahitaji wewe. Hupatikana kwa nadra sana, huzaliwa kwa makusudi maalumu,huletwa na Mungu Mwenyewe,huinuliwa kwa mkono wa Mungu Mwenyewe na kupewa kibali na yeye aliye juu Muumba wa mbingu na Nchi.
Kwa hakika Rais Samia ni zawadi kwa Taifa hili. itatuchukua muda mrefu sana kupata Rais na kiongozi mwingine mwenye akili kubwa na uwezo wa kiuongozi kama alionao Rais Samia. hivyo kwa sasa Inatupasa kumshikilia kwa nguvu sana na kuendelea kumuunga mkono.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.