Rais Samia ni Jemedari Aliyejitoa na kujitolea Utumishi wake Kwa Watanzania Bila Kujibakisha.

Mtu aliejitoa Kwa utumishi wake hawana hiyo tabia unayoizungumza wewe.

1. Rasilimali za nchi na taifa Kwa wageni.

2. Kutaka sifa asifiwe na wapigaji. Hawez kukemea wapigaji. Anachotaka wale bila kuingiliana. Kila mtu Kwa urefu wa kamba yake. Je watanzania ambao hawapo kwenye system wanaotegemea uongozi Bora unaosimamia rasilimali Kwa maendeleo ya wote watakula wapi?

Eti kajitoa Kwa watanzania bila kujibakisha.

Acha uongo. We ni mtu mzima, na mwanaume. Au we ni mwanamke?
 
Dikteta Mama au Mama Dikteta jina lipi hapo tuanze kumuita.
 
Uchawa unekuzidi soon utakua kupe wa mama
 
Rais Samia ni Mama mzalendo sana na mwenye uchungu na Maisha ya watanzania
 
Rais Samia ni Mama mzalendo sana na mwenye uchungu na Maisha ya watanzania
 
Hahaha! Kumbe sasa tuna Mama wa Miujiza, aliyeacha hata chembe ya nguvu zake kwa ajili yetu! Yaani kama siyo yeye, labda mpaka leo tungekua tunatumia tochi kuwasha taa za mtaa!


Huyu mama si kiongozi tena, ni mtume wa kisiasa, amegeuka kuwa “Sadaka ya Taifa”! Kila akipumua, Watanzania tunapata ahueni. Akikohoa, bei ya mafuta inashuka (au kupanda). Mtu mzima kama huyu kugeuzwa kuwa malaika wa kisiasa si mzaha!


Eti “amepandisha mishahara kwa viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa duniani”? Labda kama dunia hiyo ni ya ndoto zako, si hii tunayohangaika na mchele wa buku jero! Huku chini tulipo, watu bado wanaamka saa kumi kwenda kwenye foleni ya ajira isiyo na mwisho, huku wakisoma hotuba za "tumetekeleza".


Na hiyo ya kusema “hakuna anayeachwa nyuma”? Labda kama nyuma ni mbele. Wakulima wanalia, vijana wanahangaika, lakini sisi tunaambiwa mama amejitoa kama sadaka—sasa je, sadaka hii inaliwa na nani? Maana maskini bado wanalamba ukuta.


Kwa kifupi, chapisho lako ni tamu kama asali, lakini changanya na ukweli halisi, linaweza kuleta kisukari cha kisiasa. Kazi iendelee, lakini si kwa kupaka rangi uongo—tufanye kazi kwa macho wazi, si kwa miwani ya propaganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…