Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu Zangu huo ndio uhalisia wa mambo Wenyewe, Ukiona Namna Nchi ilivyo Tulia kwa Sasa na namna mh Rais Samia anavyoungwa mkono na Watanzania wa vyama vyote, Tambua ya kuwa ni sababu ya Tabia ya Rais Samia kuwa msikivu na kumsikiliza kila mtu mwenye dukuduku au kero au mawazo mbadala au ushauri na kufanyia kazi mawazo ya watu wote bila kujari yametolewa na Nani.
Duniani kwote nchi huingia katika migogoro ya kisiasa au hata machafuko baada ya viongozi kuweka pamba katika masikio yao na wananchi kutokupata nafasi ya kusikilizwa kilio chao au malalamiko yao, wananchi hukasirika pale wanapohisi kupuuzwa sauti zao, Wananchi hucharuka pale wanapoona hakuna matumaini wa sauti zao kusikika.
Wananchi Hulia mioyoni pale wanapohisi Kuna kundi limepoka sauti zao, wananchi huamka pale wanapoona viongozi wao hasa kiongozi mkuu wa nchi ameziba masikio yake, wananchi hurusha mawe pale wanapoona Rais wao hawajari,hawasikilizi, hawajibu Wala hawapi nafasi ya kuelezea shida zao na Wala hatoi matumaini yoyote, wananchi huuzika pale wanapoona Rais wao siyo msaada kwao Wala Tumaini lao.
Wananchi huwa wanyenyekevu Sana na wenye Subira kwa kiongozi msikivu na mzalendo, hawanaga ugomvi na kiongozi mwenye kuleta matumaini na mwenye kufanya vitu kwa kuwasqhirikishi na kuwaambia ukweli, wananchi hawapendi kuona ni Kama wametengwa au kudharauliwa au kutokuthaminiwa.
Tangia Rais Samia atwae madaraka wananchi wamekuwa wakimpenda na kumheshimu Sana kutokana na kuwa amekuwa msikivu na amekuwa akifanyia kazi malalamiko ya watanzania, Jambo lililo wafanya watanzania kuona wanathaminiwa na kuheshimiwa, hata penye shida au mapito ya kiuchumi bado watanzania wamejenga Imani na kauli zake juu ya hatua zake kuwasaidia wananchi kutokana na kuwa Mh Rais wetu Amekuwa Ni mtu mkweli na muungwana Sana, siyo kiongozi wa ndimi mbili, Ni kiongozi ambaye huzungumza kile anachomaanisha na humaanisha kile anachozungumza.
Ameziba mianya yote ya mtu yoyote kupandikiza chuki kwa wananchi katika kuichukia serikali yao,kwa kuwa amekuwa muwazi Sana katika matumizi ya kila Senti inayopatikana kupitia michango yetu au Kodi au tozo au hata misaada kutoka kwa wadau ndani na nje ya nchi yetu.
Ni kiongozi mzalendo na mwenye upendo na Taifa lake, Hana majivuno Wala kiburi Cha madaraka, Hana kauli za kejeri kwa wananchi wake Wala maneno ya kuwakatisha Tamaa watu, Ni mfariji wa watanzania penye shida.
Ni kiongozi aliyejitolea kuwatumikia watanzania kwa moyo wake wote,Ni kiongozi ambaye anaumizwa na matatizo ya watanzania wanyonge, Ni kiongozi anayetamani kuona kila mtu akiinuka kiuchumi, Nikiongozi ambaye Hataki kuona mtu akiumizwa na mwenye cheo au madaraka, Ni kiongozi aliyejipambanua Kama mtumishi wa watanzania wanyonge, Ni kiongozi anayemtazama kila mtu kwa jicho la usawa bila kujari Hali yake ya kiuchumi, Ni kiongozi anayetamani kuona wote tunapata Milo mitatu kwa siku.
Rais Samia Ametufanya sisi vijana Tuwe na matumaini na kesho yetu , Ni kiongozi aliyemfanya kila mtu awe na uhakika wakuneemeka na kupata kipande cha keki kitakapoingia ndani, Ni kiongozi ambaye amewafanya watanzania wote kwa ujumla kuwa na Tabasamu katika mioyo yao, Ni kiongozi ambaye ameleta Nuru kwetu watanzania,Ni kiongozi ambaye amewafanya watanzania wajione wanayo nafasi ya kutoa mawazo yakasikika na kufanyiwa kazi.
Rais wetu Ni msikivu Sana, Tuendelee kumuunga mkono na Tuendelee kumuombea ili mwenyezi Mungu Amlinde na kumpigania wakati wote na ampatie Afya njema na nguvu za kututumikia watanzania wote kwa usawa, Mimi naona watanzania ipo siku tutasimama kwa pamoja na kwa kauli moja kusema Asante Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kwa kututumikia kwa moyo wa upendo na uzalendo mkubwa Sana pasipo kutuumiza Wala kutugawa.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake ulio tukuka wa kugusa maisha yetu wanyonge.