Rais Samia ni Nuru ya Taifa iangazayo na kuleta Matumaini kwa mamilioni ya watanzania

Rais Samia ni Nuru ya Taifa iangazayo na kuleta Matumaini kwa mamilioni ya watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa Nchi zetu zinazoendelea hususani barani Afrika kiongozi mkuu wa Nchi yaani Rais Wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu Anaweza leta nuru ama giza katika Taifa na mioyoni mwa Watu,anaweza leta Matumaini au kuwavunja watu moyo ,anaweza wafanya watu kuona leo ni afadhali ya jana au kuona kesho yenye Matumaini.

Rais Wa Nchi anaweza wafanya watu kwa mamillioni yao kuishi kwa amani,upendo, mshikamano,furaha,utulivu ,umoja na ushirikiano.lakini mtu mmoja huyo huyo anaweza kufanya Taifa likaingia gizani,watu kuishi kwa hofu ,uoga,chuki,visasi,uhasama, vinyongo,kukosa Matumaini,malipizi pamoja na kutoona faida ya kuzaliwa Nchini na kuomba mabaya tu yatokee Nchini.

Kichocheo cha hayo yote hutokana na kauli pamoja na matendo ya Rais.maneno yatokayo katika kinywa cha Rais yanaweza jenga umoja wa kitaifa au kulisambaratisha na kuligawa Taifa vipande vipande.kauli na matendo ya Rais yanaweza wafanya watu walale kwa hofu na kuamka kwa hofu wakiwa hawana Matumaini mioyoni mwao.

Ndio maana ni muhimu sana kwa Rais kuchunga sana ulimi na maneno yake yatokayo katika kinywa chake.kwa sababu ulimi wake unaweza vutia wawekezaji, watalii, wafanyabiashara au kuwafukuza wote hao na kuwafanya kufunga shughuli zao na kuweka mapesa yao mfukoni na kukimbia kwa hofu.

Ukiangalia Tangia kuingia madarakani kwa Rais wetu Mpendwa kipenzi cha watanzania na Jemedari wetu imara na hodari Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.unaona namna Taifa lilivyo tamalaki kwa amani ,utulivu na usalama wa hali ya juu sana.ameleta na kujenga umoja wa kitaifa kwa 4R zake,amewaleta watu pamoja na kujiona ni watanzania wenye haki sawa.

Amekuwa ni mtenda haki na mpenda haki kwa watu wote.amekuwa ni kiongozi aliyemfanya kila mtanzania kuona fursa na nafasi ya kutimiza ndoto zake,ametufanya watanzania tuishi kwa matumaini,umoja ,upendo na mshikamano wa hali ya juu sana.Kwa kauli zake na matendo yake amewavutia wafanyabiashara, watalii, wawekezaji kumiminika Nchini kwa wingi na hata wazawa kufungua miradi pasipo hofu wala wasiwasi.

Amejenga imani na kuaminiana kukubwa sana miongoni mwetu watanzania.kila mmoja anamuona ni kiongozi wa wote ambaye unaweza kumkimbilia ,kumlilia shida nakuomba msaada na ukaupata kwa haraka na uharaka bila kujali hali yako au itikadi za kisiasa.hii ndio sababu watu hupenda kumwita Mama mfariji wa Taifa na Mama mlezi wa wote pasipo ubaguzi.

Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu Mpendwa na shujaa wetu Kipenzi na jasiri aliyeongoza njia yenye Matumaini katika maisha ya kila mtu.fahamuni kuwa wapo wanaoumia sana wanapoona Mama anaongoza nchi vizuri katika muelekeo mzuri, wakati wao walitamani na kuombea ashindwe na kuchukiwa na watanzania.ndio maana watu hawa waliofilisika kihoja utaona wakijaribu kupandikiza mbegu ya ubaguzi kwa misingi ya ukabila,Udini ,ukanda,jinsia na wengine wakianza mawazo ya kijinga jinga Utafikiri wao ni Mungu kwa kuanza kuzungumza habari za umri.hawa wote wanatumiwa na wale watu wenye uchu wa madaraka na wanaotoa ulimi nje kutamani kiti cha Urais kwa njia yoyote ile
Screenshot_20240901-150630_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Chawa wana laana kubwa sana!!

Hakuna kipindi chochote katika uhai wa Taifa ambapo kumkosoa Rais au Serikali lilikuwa ni tendo la kuhatarisha uhai wako kwa kiwango kikubwa kama awamu hii. Taarifa ya TLS inasema wanaharakati wakosoaji wa Serikali na viongozi na wanachama wa upinzani waliotekwa na hawajulikani waliko mpaka sasa ni zaidi ya 60. Rais anasema eti hao waliotekwa ni drama!!

Watu wanatekwa na kuawa, Rais anasema eti kifo ni kifo tu, yaani kutekwa na kuuawa kwa sababu wewe ni mpinzani ni sawa na kufa kwa malaria!!
 
Comredi Mwashambwa ulipotelea wapi siku mbili hizi?
Nilimiss kutokwa machozi ya furaha sababu ya nyuzi zako za kumsifia mama.

Hakika chozi la furaha linanidondoka sasa hivi kutokana na mng'ao wa nuru ya mama kwa taifa🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom