Rais Samia, ni Watanzania gani hao waliokubali hizo tozo?

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Nimeshangaa na kufadhaishwa sana naa kauli ya raisi kuwa eti watanzania hawajakataa tozo na wapo tayari kuchangia hizo tozo ila tu zipunguzwe.

Hii kauli imenifanya nijiulize sana kuwa either amechoka kuongoza au hajui afanye nini.

Watanzania gani hao wanaokubali tozo hizi? Mmekaa wenyewe mmekubaliana wenyewe alafu leo unasema watanzania wapo tayari kuchangia.

Huu ni uongo mkubwa sana na sijui ni kwa faida gani.

Watu wengi walikuwa wakimshutumu mwigulu kuhusu tozo ila picha tunaanza kuiona ni wapi tozo zilianzia.

Huyu mama ukweli usemwe, uwezo ni mdogo sana ni mdogo sana.

Hata tuukimbie vipi huu ukweli utatufata popote tulipo.

#mbowe sio gaidi#
 
Raisi kajieleza vizuri kabisa. Kwamba tozo ni kubwa na hivyo ziweze kupunguzwa. Lkn pia kasema tozo zilianzishwa ili tuweze kupelekewa huduma za kijamii maeneo ambayo bajeti yetu ya kawaida ilishindwa kufika. Ko badala ya kulalamika ni vyema tukaanza kuiombea serikali yetu itimize adhima ya kutuletea huduma vijijini.
 
Una hakika hizo pesa zitatumika kama wanavyosema? au kununulia ma vieete na posho zao?
 
Raisi kajieleza vizuri kabisa. Kwamba tozo ni kubwa na hivyo ziweze kupunguzwa. Lkn pia kasema tozo zilianzishwa ili tuweze kupelekewa huduma za kijamii maeneo ambayo bajeti yetu ya kawaida ilishindwa kufika. Ko badala ya kulalamika ni vyema tukaanza kuiombea serikali yetu itimize adhima ya kutuletea huduma vijijini.
Kabla ya hizo tozo huduma mlikuwa hampati?
 
Mbunge wako akikubali kitu, basi ujue kakubali kwa niaba yako. Yeye ndio mwakilishi wako katika ngazi za maamuzi.
Mbunge Ni mwakilishi wa wananchi wapiga kura wake hatakiwi tu kuibuka bungeni na kuropoka Je hicho kikao Cha miamala Zungu aliongea na wapiga kura wake Kwanza?

Wananchi wa Ilala walimtuma Hilo? Alifanya nao mkutano kupata mawazo yao kwenye Hilo au aliibuka tu bungeni na bichwa lake tu na kuongea yeye Kama yeye?
 
Nimeshangaa na kufadhaishwa sana naa kauli ya raisi kuwa eti watanzania hawajakataa tozo na wapo tayari kuchangia hizo tozo ila tu zipunguzwe,.
Hii kauli imenifanya nijiulize sana kuwa either amechoka kuongoza au hajui afanye nini.
Watanzania gani hao wanaokubali tozo hizi? Mmekaa wenyewe mmekubaliana wenyewe alafu leo unasema watanzania wapo tayari kuchangia.
Huu ni uongo mkubwa sana, na sijui ni kwa faida gani.
Watu wengi walikuwa wakimshutumu mwigulu kuhusu tozo ila picha tunaanza kuiona ni wapi tozo zilianzia.
Huyu mama ukweli usemwe, uwezo ni mdogo sana ni mdogo sana.
Hata tuukimbie vipi huu ukweli utatufata popote tulipo.

#mbowe sio gaidi#
Tupo wengi mno tunaokubali tozo. Tunachangia vitu vingapi sembuse tozo?
 
Nimeshangaa na kufadhaishwa sana naa kauli ya raisi kuwa eti watanzania hawajakataa tozo na wapo tayari kuchangia hizo tozo ila tu zipunguzwe,.
Hii kauli imenifanya nijiulize sana kuwa either amechoka kuongoza au hajui afanye nini.
Watanzania gani hao wanaokubali tozo hizi? Mmekaa wenyewe mmekubaliana wenyewe alafu leo unasema watanzania wapo tayari kuchangia.
Huu ni uongo mkubwa sana, na sijui ni kwa faida gani.
Watu wengi walikuwa wakimshutumu mwigulu kuhusu tozo ila picha tunaanza kuiona ni wapi tozo zilianzia.
Huyu mama ukweli usemwe, uwezo ni mdogo sana ni mdogo sana.
Hata tuukimbie vipi huu ukweli utatufata popote tulipo.

#mbowe sio gaidi#
Unajiuliza mwenyewe ukiwa na HAMAKI.....

Na unajijibu mwenyewe ukiwa na HAMAKI.....

Watanzania tuko wengi ,post yako hainisemei mimi....MIMI NINATAKA IWEPO HIYO TOZO...muhimu iwe ndogo tu.....

Je una uhakika mtanzania mimi niko peke yangu ?!!

Rais ana vyanzo vya taarifa zaidi yako mdandamoni hapo.....hakurupuki na ndio maana usikivu wake umesababisha aiteue KAMATI ILI IJE NA MAPENDEKEZO.....

NAUNGA MKONO TOZO ILIYO NDOGO KWA MAENDELEO YA NCHI YETU WENYEWE
 
Back
Top Bottom