Rais Samia, ni Watanzania gani hao waliokubali hizo tozo?

Rais Samia, ni Watanzania gani hao waliokubali hizo tozo?

Nimeshangaa na kufadhaishwa sana naa kauli ya raisi kuwa eti watanzania hawajakataa tozo na wapo tayari kuchangia hizo tozo ila tu zipunguzwe.

Hii kauli imenifanya nijiulize sana kuwa either amechoka kuongoza au hajui afanye nini.

Watanzania gani hao wanaokubali tozo hizi? Mmekaa wenyewe mmekubaliana wenyewe alafu leo unasema watanzania wapo tayari kuchangia.

Huu ni uongo mkubwa sana, na sijui ni kwa faida gani.

Watu wengi walikuwa wakimshutumu mwigulu kuhusu tozo ila picha tunaanza kuiona ni wapi tozo zilianzia.

Huyu mama ukweli usemwe, uwezo ni mdogo sana ni mdogo sana.

Hata tuukimbie vipi huu ukweli utatufata popote tulipo.

#mbowe sio gaidi#
Watanzania waliokubali hizo tozo ni watanzania wale wale waliokubali uhalali wa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Umesahau?
 
Nimeshangaa na kufadhaishwa sana naa kauli ya raisi kuwa eti watanzania hawajakataa tozo na wapo tayari kuchangia hizo tozo ila tu zipunguzwe.

Hii kauli imenifanya nijiulize sana kuwa either amechoka kuongoza au hajui afanye nini.

Watanzania gani hao wanaokubali tozo hizi? Mmekaa wenyewe mmekubaliana wenyewe alafu leo unasema watanzania wapo tayari kuchangia.

Huu ni uongo mkubwa sana, na sijui ni kwa faida gani.

Watu wengi walikuwa wakimshutumu mwigulu kuhusu tozo ila picha tunaanza kuiona ni wapi tozo zilianzia.

Huyu mama ukweli usemwe, uwezo ni mdogo sana ni mdogo sana.

Hata tuukimbie vipi huu ukweli utatufata popote tulipo.

#mbowe sio gaidi#

Aongeze tozo zaidi tafadhali. Maradufu ingependeza zaidi.

Angeweka na kwenye chanjo za UVIKO pia ingependeza zaidi.
 
Mbunge wako akikubali kitu, basi ujue kakubali kwa niaba yako. Yeye ndio mwakilishi wako katika ngazi za maamuzi.
waliichagua ccm wakizani wanakomoa upinzani kumbe wote ni mwendo wa kuisoma namba. Hamna cha upinzani wala cha ccm,

wacha waendelee kujifunza siku wakichoka ndo watafanya maamuzi watakayo ona yanafaa. Yani waendelee kukazwa spana au watumie akili.
 
Mbunge Ni mwakilishi wa wananchi wapiga kura wake hatakiwi tu kuibuka bungeni na kuropoka Je hicho kikao Cha miamala Zungu aliongea na wapiga kura wake Kwanza?

Wananchi wa Ilala walimtuma Hilo? Alifanya nao mkutano kupata mawazo yao kwenye Hilo au aliibuka tu bungeni na bichwa lake tu na kuongea yeye Kama yeye?
Kwani wewe unaishi jimbo la Ilala? Labda alifanya kikao na watu wake?
 
Dereva kapewa chombo katikati ya safari halafu yeye alizoea automatic

Sasa kakutana na manual anatamani aone stand apaki lakini kila akichungulia vibao vimeandikwa bado km 3000 ufike na kila mwaka ni km 1000,

Abiria nao kelele kibao mara tunaenda taratibu wengine leseni yake ndogo gari kubwa wengine wanasema hajui kutumia alama za barabara yaani tafrani tupu
 
Mbunge wako akikubali kitu, basi ujue kakubali kwa niaba yako. Yeye ndio mwakilishi wako katika ngazi za maamuzi.
lakini situlikubaliana kuwa
wale wabunge ni wabunge wa mwendazake
na wanatumika kumwakilisha mwendazake
cc mzee halima,
 
Dereva kapewa chombo katikati ya safari halafu yeye alizoea automatic

Sasa kakutana na manual anatamani aone stand apaki lakini kila akichungulia vibao vimeandikwa bado km 3000 ufike na kila mwaka ni km 1000,

Abiria nao kelele kibao mara tunaenda taratibu wengine leseni yake ndogo gari kubwa wengine wanasema hajui kutumia alama za barabara yaani tafrani tupu
Umenikumbusha wamama wa kiswahili huko uswahilini
 
Tena waongeze tozo zaidi
Hii waliyoweka bado ndogo
Sana

Ova
 
Unamuonea huruma mtu ambae hakuonei huruma...imagine unamfikiria sana mtu ambae hakufikirii hata kidogo
Uwezo wake wa kuchakata mambo ni too low najua hata huko kwenu ndani chama mnalijua hilo, huyu atapata upinzani mkubwa sana hata ndani ya chama
 
Nimeshangaa na kufadhaishwa sana naa kauli ya raisi kuwa eti watanzania hawajakataa tozo na wapo tayari kuchangia hizo tozo ila tu zipunguzwe.

Hii kauli imenifanya nijiulize sana kuwa either amechoka kuongoza au hajui afanye nini.

Watanzania gani hao wanaokubali tozo hizi? Mmekaa wenyewe mmekubaliana wenyewe alafu leo unasema watanzania wapo tayari kuchangia.

Huu ni uongo mkubwa sana, na sijui ni kwa faida gani.

Watu wengi walikuwa wakimshutumu mwigulu kuhusu tozo ila picha tunaanza kuiona ni wapi tozo zilianzia.

Huyu mama ukweli usemwe, uwezo ni mdogo sana ni mdogo sana.

Hata tuukimbie vipi huu ukweli utatufata popote tulipo.

#mbowe sio gaidi#
Wamezoea uongo: "JPM yu mzima wa afya na anachapa kazi".
Hawaheshimu wananchi: "Hata msipotupigia kura tutaunda serikali tu".
Wamelewa madaraka: "Watanzania wote wamekubali tozo kwenye miamala ya simu".
Wamezeeka na kuchoka kufikiri: "Mtushauri ninyi mnaopinga hizi tozo njia zingine za kupata fedha ya kuboresha miundombinu vijijini".
 
Tatizo kubwa jingine ni hizo tozo kutofanyiwa kazi stahiki. Ngoja tuone kama itawezekana hayo anayoyasema.

Na kwa maana nyingine yeye na mwendazake walitudanganya kusema hii nchi ni tajiri sana.
 
Tuna matatizo mengi katika jamii yetu, kwa mujibu wa mama, serikali haina uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kuleta tozo, maeneo kama;
1. Watoto kukaa chini darasani
2. Uhaba wa madawa hospitalini
3. Elimu, uhaba wa walimu
4. Familia masikini, TASAF haikidhi
5. Vitambulisho wa taifa
.
.
.
Asichelewe sana kwenye hayo pia, tozo aliyoongeza ni ndogo sana, angalau angepandisha bei za bidhaa zote muhimu ili kuharikisha maendeleo kila sekta
  • Ukiuza lipa tozo, ukinunua lipa tozo
  • Kuwe na tozo ya kuingia na kutoka kazini
  • Ukichangia sherehe zozote kama za ndoa n.k ulipe tozo
  • Tozo ya kutembea kwenye barabara ya lami
Angalau mlalahoi kabisa atoe sh 100,000 kwa mwezi kama tozo ya maendeleo kizalendo kabisaaa.

Asante.
 
una hakika hizo pesa zitatumika kama wanavyosema? au kununulia ma vieete na posho zao?
Kwanza nataka kujua ni tozo kiasi gani ilikusudiwa kukusanywa na nikiasi gani kinakusanywa, na kiasi gani kimepelekwa kulikokusudiwa, na ni wapi huko ( taja wilaya, kata, kijiji/ mtaa) hayo makusanyo ya tozo yamepelekwa.

Uwazi katika ukusanyaji, utunzaji, utumiaji, usimamiaji wa utumiaji wa pesa zinazokusanywa kutokana na tozo kwenye miamala ya simu ni wa lazima kama serikali ina nia ya kuaminika na raia walio wengi.
 
Back
Top Bottom