Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu hivyo ndivyo unavyoweza kusema, Rais Samia amejitoa na kujitolea kwa moyo wake wote kututumikia Watanzania kwa dhati ya moyo wake. Ni kiongozi ambaye mawazo yake yapo katika kuona kila siku walau maisha ya mtanzania mmoja au kundi la watanzania linainuka kiuchumi, wakati Mtanzania mwingine au kundi lingine nalo likiwa limeshikwa mkono na Rais, tayari kwa kuinuliwa kiuchumi kutoka katika dhiki.
Rais Samia kila anakokwenda unaona akitafuta fursa za kuwanufaisha Watanzania, kila anakokwenda unaona Rais Samia akitafuta mwanya wakuona Watanzania wenye uwezo wanafanya biashara katika nchi husika, kila aendako unaona moyo wa Rais Samia umeunganika na Watanzania tuliyobaki hapa nyumbani.
Ni kiongozi anayetamani kuona Watanzania tuna neemeka na fursa zote zinazopatikana popote pale katika uso wa dunia. Anataka kuona Watanzania hatubaki nyuma wala kuachwa na wenzetu, anataka kuona Tanzania inakuwa kimbilio na chaguo la kwanza la wawekezaji, wafanyabiashara wakubwa, watalii, wanamichezo, wageni na kila aina ya uwekezaji utakaoleta fursa katika nchi yetu na kusisimua na kukuza uchumi wetu.
Kaiheshimisha sana Tanzania kwa sasa ndiyo maana unaona namna watalii wanavyozidi kumiminika hapa nchini. Sasa uwekezaji unaongezeka siku hadi siku, hali itakayochochea kuongezeka kwa fursa za ajira kwetu vijana na mapato ya kodi yataongezeka.
Huduma mbalimbali za kijamii zitazidi kuboreshwa, kipato cha mwananchi mmoja mmoja kitaongezeka, mzunguko wa fedha utakuwa wenye Afya, mabenki yataongeza wanufaika wa mikopo na kupunguza riba kutokana na kuwepo kwa kiasi cha kutosha cha fedha kinachowekwa na watu kama akiba.
Kupitia juhudi hizi za Rais Samia katika kuimarisha diplomasia yetu ya uchumi, naona maisha ya Mtanzania yakiboreka na kuendana na utajiri wa nchi yetu, keki ya Taifa itafika kwa kila Mtanzania na kila mmoja atakula. Kila mmoja ataona faida ya utajiri huu tuliopewa na mwenyezi Mungu, kila Mtanzania atajivunia kuwa na kuzaliwa Tanzania katika nchi ya asali na maziwa.
Hakika Rais samai ni zawadi kwetu Watanzania, kiukweli anatukosha sana Watanzania kwa namna anavyochapa kazi, kwa namna alivyo mbunifu na anavyo tafuta fursa kwa ajili ya nchi yetu. Rais Samia ni mama wa taifa, mlezi bora wa Taifa na mama mwenye maono ya mbali. Hakika uongozi wake utaacha alama za kimaendeleo zitakazokumbukwa vizazi na vizazi na kusemwa kuwa, haya ni matunda ya Mama wa Taifa, Samia suluhu Hassani.
Kazi iendelee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge.
Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.