Rais Samia ni zawadi kwetu Watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu

Rais Samia ni zawadi kwetu Watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu

Sikiliza wewe Mimi Ni mkulima na ninaongea uhalisia wa kile nachokiishi na kukifanya, mwaka huu Bei ya mazao ilikuwa nzuri tangia wakati wa mavuno na hivyo kutufanya kuuza kwa Bei nzuri tokea wakati tunavuna mazao yetu, tofauti na miaka mingine ambapo tuliuza kwa Bei ya hasara wakati wa mavuno
Acha fix wewe! Ni mkulima gani mnyonge wa nchi hii mwenye uwezo wa kusafirisha mazao yake kupeleka nje ya nchi?
 
Hapana haziishii mikononi mwa watu Bali zinafika kutunufaisha wanyonge, mfano katika mbolea ya DAP wakulima tulinunua mfuko mmoja laki na 20 Hadi laki na 40, lakini baada ya Rais wetu mpendwa kutoa mabillioni ya Ruzuku kwa Sasa katika maduka yaliyopewa kibali Cha kuuza na kusambaza mbolea za Ruzuku mfuko wa DAP unapatikana kwa shilingi elfu 70 tu, Sasa hapa Huoni mh Rais wetu mpendwa katusaidia Sana? Huoni hapa kagusa mioyo yetu? Huoni hapa katusaidia kuongeza uzalishaji? Huoni hapa katupunguzia gharama ukilinganisha na msimu uliopita?

Kumbuka pia mh Rais wetu mpendwa yupo katika juhudi za kuhakikisha nchi inapata wawekezaji wengi watakaojenga viwanda vya mbolea hapa Hapa nchini ili mbolea ipatikane kwa urahisi na kwa Bei nzuri ambayo mkulima wa Hali ya chini Kama mimi nitaweza kumudu vizuri bei bila shida yoyote
Bora hata hapa umejitahidi kujenga hoja! Natambua fika kuna ongezeko la bei ya mafuta kutokana na hiyo vita ya Urusi dhidi ya Ukraine!

Lakini usisahau Rais wako kipenzi kwa kumtumia Waziri wake wa fedha, wameongeza tozo kwenye hayo mafuta ili hela itakayo patikana, ikajengee madarasa na vituo vya afya!

Na hata hiyo ruzuku anayoitoa, haina maana yoyote ile! Maana itaishia tu mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa na wasio waaminifu!

Alichotakiwa Bi tozo kufanya, ni kuiondoa kabisa ile tozo yake aliyo ianzisha, mpaka hapo hali ya uchumi itakapo tengemaa.
 
Ndugu zangu Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema, Rais Samia Amejitoa na kujitolea kwa moyo wake wote kututumikia watanzania kwa Dhati ya moyo wake, Ni kiongozi ambaye mawazo yake yapo katika kuona kila siku walau maisha ya mtanzania mmoja au kundi la watanzania linainuka kiuchumi wakati mtanzania mwingine au kundi lingine nalo likiwa limeshikwa mkono na mh Rais Tayari kwa kuinuliwa kiuchumi kutoka katika dhiki

Rais Samia kila anakokwenda unaona akitafuta fursa za kuwanufaisha Watanzania, kila anakokwenda unaona Rais Samia akitafuta mwanya wakuona watanzania wenye uwezo wanafanya biashara katika nchi husika, kila aendako unaona moyo wa Rais Samia umeunganika na watanzania tuliobaki hapa nyumbani

Ni kiongozi anayetamani kuona watanzania tuna neemeka na fursa zote zinazopatikana popote pale katika uso wa Dunia, Anataka kuona watanzania Hatubaki nyuma Wala kuachwa na wenzetu, anataka kuona Tanzania inakuwa kimbilio na chaguo la kwanza la wawekezaji , wafanyabiashara wakubwa, watalii, wanamichezo, wageni na kila aina ya uwekezaji utakao leta fursa katika nchi yetu na kusisimua na kukuza uchumi wetu

Kaiheshimisha Sana Tanzania kwa sasa ndio maana unaona namna watalii wanavyozidi kumiminika hapa nchini, Sasa uwekezaji unaongezeka siku Hadi siku Hali itakayochochea kuongezeka kwa fursa za ajira kwetu vijana, mapato ya Kodi yataongezeka, Huduma mbalimbali za kijamii zitazidi kuboreshwa, kipato Cha mwananchi mmoja mmoja kitaongezeka, mzunguko wa fedha utakuwa wenye Afya, mabenki yataongeza wanufaika wa mikopo na kupunguza riba kutokana na kuwepo kwa Kias Cha kutosha Cha fedha kinachowekwa na watu Kama akiba,

Kupitia juhudi hizi za Rais Samia katika kuimarisha diplomasia yetu ya uchumi Naona maisha ya mtanzania yakiboreka na kuendana na utajiri wa nchi yetu, keki ya Taifa itafika kwa kila mtanzania na kila mmoja atakula, kila mmoja ataona faida ya utajiri huu tuliopewa na mwenyezi Mungu, Kila mtanzania atajivunia kuwa na kuzaliwa Tanzania katika nchi ya Asali na Maziwa

Hakika Rais samai Ni zawadi kwetu watanzania, kiukweli Anatukosha Sana watanzania kwa namna anavyochapa kazi, kwa namna alivyo mbunifu na anavyo tafuta fursa kwa ajili ya nchi yetu, Rais Samia Ni mama Wa Taifa, Mlezi Bora wa Taifa Na mama Mwenye Maono ya Mbali, Hakika uongozi wake utaacha Alama za kimaendeleo zitakazokumbukwa vizazi na vizazi na kusemwa kuwa haya Ni Matunda ya Mama wa Taifa Samia suluhu Hassani

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Mwashambwa , kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
wewe chawa mbona kama umelogwa. It is if huna wazazi wa kuwasujudia, maana huwezi kumsujudia mtu kiasi hiki.
 
Mkulima asiyeweza kusafirisha Kama Mimi anauza katika soko lililo karibu yake ambalo kwa Sasa yanapatikana maeneo mengi tu kwa Bei nzuri tu yenye faida, kumbuka Kama soko likiwa zuri na la uhakika nje ya nchi kwa wanaopeleka mantiki yake ni kuwa hata huku mitaani Bei inakuwa Ni nzuri Sana, lakini Kama hata nje ya nchi hakuna soko mantiki yake ni kuwa hata mitaani Bei itakuwa Ni mbaya kwa kuwa kutakuwa hakuna kwa kupeleka na kuuza hivyo uhitaji ukiwa mdogo lazima hata Bei iwe ndogo, mama yupo kazini kututumikia na kuleta matumaini palipo na kukata tamaaa
Acha fix wewe! Ni mkulima gani mnyonge wa nchi hii mwenye uwezo wa kusafirisha mazao yake kupeleka nje ya nchi?
 
wewe chawa mbona kama umelogwa. It is if huna wazazi wa kuwasujudia, maana huwezi kumsujudia mtu kiasi hiki.
Namheshimu Sana Rais wangu na kumuunga mkono kwa namna alivyojitoa na kujitolea kututumikia watanzania bila kuchoka Wala kukata tamaaa au kukatishwa tamaa na watu wachache aina yako wasioona zuri katika yote afanyayo kulitumikia Taifa letu, wazazi wangu nao pia nawaheshimu Sana Kama ilivyoandika biblia kuwa waheshimu wazazi wako upate siku nyingi za kuishi hapa Duniani
 
Fafanua basi hapo watu hawajakuelewa.
Upinzani walizoea janja janja ya vimianya vidogo vidogo vilivyoachwa na chama au serikali katika kupata hoja za kuongea, lakini kwa Sasa utumishi uliotukuka wa mh Rais wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge imefanya wapinzani wakose hoja kabisa, maana Rais anafanya vitu vinavyoleta matokeo chanya kwa watanzania, lakini pia mh Rais amekuwa msikivu Sana kwa watanzania kwa kuhakikisha kuwa kila sauti ya mtanzania inasikika na kusikilizwa na kufanyiwa kazi, kila mwenye neno anasikilizwa, kaleta matumaini makubwa Sana katika nchi hii, kila mtu anajiona anayo nafasi katka ujenzi wa Taifa hili, kaleta mwanga mahali ambapo watanzania waliona Giza, kaleta matumaini mahali ambapo watanzania walijaa chuki,amekuwa Ni chombo Cha Amani kwa watanzania
 
Namheshimu Sana Rais wangu na kumuunga mkono kwa namna alivyojitoa na kujitolea kututumikia watanzania bila kuchoka Wala kukata tamaaa au kukatishwa tamaa na watu wachache aina yako wasioona zuri katika yote afanyayo kulitumikia Taifa letu, wazazi wangu nao pia nawaheshimu Sana Kama ilivyoandika biblia kuwa waheshimu wazazi wako upate siku nyingi za kuishi hapa Duniani
Kinyaa! Unatia kinyaa! Rais ni mtu kama wewe na mimi, anakunya, anakojoa , anajampa and all sorts of biological atributes of a living organism. sasa kumpamba hivyo mwanadamu kwanini. Kila siku unapost kumsujudia, why? Amefanya nini la maana ambalo huwezi kulifanya? kichwani mwako kuna nini?
 
Tangu lini wewe Lucas mwashambwa umekuwa msemaji wa watanzania?
Hii tabia ya kushinda mitandaoni kusifia viongozi ni ya hovyo sana siku nyingine jisemee mwenyewe
Kama hushindi mtandaoni ungewezaje kuona hoja hii,
 
Hapana haziishii mikononi mwa watu Bali zinafika kutunufaisha wanyonge, mfano katika mbolea ya DAP wakulima tulinunua mfuko mmoja laki na 20 Hadi laki na 40, lakini baada ya Rais wetu mpendwa kutoa mabillioni ya Ruzuku kwa Sasa katika maduka yaliyopewa kibali Cha kuuza na kusambaza mbolea za Ruzuku mfuko wa DAP unapatikana kwa shilingi elfu 70 tu, Sasa hapa Huoni mh Rais wetu mpendwa katusaidia Sana? Huoni hapa kagusa mioyo yetu? Huoni hapa katusaidia kuongeza uzalishaji? Huoni hapa katupunguzia gharama ukilinganisha na msimu uliopita?

Kumbuka pia mh Rais wetu mpendwa yupo katika juhudi za kuhakikisha nchi inapata wawekezaji wengi watakaojenga viwanda vya mbolea hapa Hapa nchini ili mbolea ipatikane kwa urahisi na kwa Bei nzuri ambayo mkulima wa Hali ya chini Kama mimi nitaweza kumudu vizuri bei bila shida yoyote
Ona sasa mimi naongelea ruzuku hewa ya kwenye mafuta, wewe unaleta story za ruzuku ya kwenye mbolea!

Tena ruzuku inayotolewa kwa ajili ya kilimo kinachotegemea mvua, huku tukiwa tumezungukwa na vyanzo lukuki vya maji! Kuanzia maziwa, mabwawa, bahari, mito,, nk.
 
Kinyaa! Unatia kinyaa! Rais ni mtu kama wewe na mimi, anakunya, anakojoa , anajampa and all sorts of biological atributes of a living organism. sasa kumpamba hivyo mwanadamu kwanini. Kila siku unapost kumsujudia, why? Amefanya nini la maana ambalo huwezi kulifanya? kichwani mwako kuna nini?
Yaani wewe sijuwi kwanini huwezagi kujenga hoja bila kutumia maneno ya ukakasi na kuvunjia mtu heshima, Mimi huwa naamini mtu unaweza ukaandika kwa heshima na meneno ya kistaarabu na ujumbe wako ukaeleweka vizuri kabisa na watu wote wakachangia bila shida yoyote Ile , tunaweza tukatofautiana mitizamo na tunakosoana kistaarabu bila kumvunjia mtu heshima au kutumia maneno ya ukakasi
 
Ona sasa mimi naongelea ruzuku hewa ya kwenye mafuta, wewe unaleta story za ruzuku ya kwenye mbolea!

Tena ruzuku inayotolewa kwa ajili ya kilimo kinachotegemea mvua, huku tukiwa tumezungukwa na vyanzo lukuki vya maji! Kuanzia maziwa, mabwawa, bahari, mito,, nk.
Ruzuku ya kwenye mafuta ilikuwaje hewa wakati unaona Kuna kiwango Cha Bei kilikuwa kinapungua katika kila Lita ya mafuta kutokana na Ruzuku iliyokuwa inawekwa na serikali inayoongozwa na Rais Samia?
 
Kumamamamama************ tuishie hapo
Wewe tukana uwezavyo Ila Mimi sitakutukana na nitaendelea kuheshimu michango yako humu na hata nisipokubaliana na wewe nitaichukulia Kama maoni yako binafsi Maana najuwa hatuwezi tukakubaliana na kufanana mawazo na mitizamo katika kila eneo, Mungu akupe moyo wa hekima busara na upendo
 
Yaani wewe sijuwi kwanini huwezagi kujenga hoja bila kutumia maneno ya ukakasi na kuvunjia mtu heshima, Mimi huwa naamini mtu unaweza ukaandika kwa heshima na meneno ya kistaarabu na ujumbe wako ukaeleweka vizuri kabisa na watu wote wakachangia bila shida yoyote Ile , tunaweza tukatofautiana mitizamo na tunakosoana kistaarabu bila kumvunjia mtu heshima au kutumia maneno ya ukakasi
Ukakasi upi, unataka kupingana na reality, tena reality of science?
 
Back
Top Bottom