Rais Samia ni zawadi kwetu Watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu

😆 😆 😆 😆 Ccm imetuharibia nchi kabisa yaaani inazalisha vijana wa hovyo
 
😆 😆 😆 😆 Ccm imetuharibia nchi kabisa yaaani inazalisha vijana wa hovyo
CCM ni chama pekee barani Afrika kinachoweza kupika na kuandaa vijana wake kuwa viongozi wa baadaye kwa kuwalea vizuri kimaadili na kizalendo
 
Acha uchawa wewe. Hujaona kama samia anatetea tu wafanya biashara? Wamepandisha bidhaa kwa kisingizio cha uongo kwa kupewa kichwa na rais. Amerudisha wapigaji na watumbuliwa kwani kupiga hela ya umma kwake sio tatizo. Ameweza hata kuwaambia watumishi wa umma kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Alipoingia akaanza uharakati kuweka wanawake kwa wingi kwenye uongozi. Ndio wengine bomu kama huyu mulamula. Badala ya kutanguliza weledi uadilifu na uzalendo unaweka uwanaweke kama sifa kumteua mtu.
Tumuombe mungu atufikishe salama 2025 tuweze kuweka magufuli mpya kuongoza nchi.
 
Wewe una matatizo makubwa Sana maana umeandika uongo mtupu, kwani huoni namna mh Rais wetu mpendwa alivyotutetea na kutusaidia wakulima kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya kilimo Hadi kufikia billioni Mia Tisa na pointi, hujaona akitoa Ruzuku ya mabillioni katika kilimo Hali iliyopelekea kushuka kwa mbolea msimu huu,

Hujaona anavyopigania watoto wa maskini ili nao wapate haki ya kupata Elimu kwa uamuzi wake wa kuamua kufuta Ada na kutoa Elimu bure Hadi kidato Cha sita?

Hujaona hata Sasa wanafunzi watakaosoma masomo ya sayansi na kuchukua kozi za sayansi Kama Udaktari watasomeshwa bure? Huoni namna mh Rais wetu alivyoboresha huduma za Afya na kusogeza huduma karibu ya mwananchi? Hujasikia habari za kujengwa kwa vituo vya Afya 234 hapa nchini, hujaona vyumba vya madarasa zaidi ya elfu nane vikijengwa kwote nchini? Wewe upo nchi gani wewe ambako yote haya huyafahamu? Rudi Tanzania uone mama anavyochapa kazi kwa nguvu zake zote
 
😆 😆 😆 😆 Ccm imetuharibia nchi kabisa yaaani inazalisha vijana wa hovyo
Hii ni posti namba no. 112 katika thread hii na wachangiaji walioonesha kumuunga mkono huyu chawa Lucas mwashambwa ni watatu tu huku wengine 108 wakimpinga!

Kwa hesabu za haraka haraka asilimia 98% wanapinga utopolo wake. Bila shaka huu hasa ndio ujumbe anaotaka kumfikishia kiongozi mhusika ajionee mwenyewe asivyokubalika kwa asilimia kubwa ya Watanzania.

Hongera sana Lucas mwashambwa, labda ni kwa kutojua lakini asante kwa kutuwakilisha vyema kabisa, ujumbe wako umegonga pale pale na bila shaka utafanyiwa kazi.
 
Ukweli huwa Haijalishi wangapi mnapinga, ukweli unabaki kuwa ukweli siku zote, kwa kukusaidia tu nenda kasome habari za Galileo ambaye alisimamia ukweli licha ya kupingwaa Sana lakini leo sote tunatambua kuwa kumbe kweli Galileo alikuwa sahihi na alikuwa anasema kweli, hata waliompinga wakati huo walikuja kukiri kuwa alikuwa anasema ukweli, hata nyie wachache ipo siku mtakili maneno yangu kuwa Ni ya kweli, muda Ni mwalimu mzuri na utatufundisha wakati ukifika tu, Rais Samia Ni Dhahabu kwetu watanzania
 
Unazidi kumharibia na kama unalipwa unachofanya ni hujuma, unamhujumu anayekulipa!. Na tafadhali ongea kwa niaba yako wewe na familia yako...na si Watanzania!
 
Chawa naona unaweka gazeti baada ya gazeti ukiamini utampatia mama na CCM mvuto. Kwa taarifa yako CCM sio chama cha kizazi hiki, ndio maana kimebaki kujishikisha kwenye vyombo vya dola.
 
Wewe si unakula na kushiba na kusaza na familia yako!!! Wanao wanasoma shule utakayo! Si unalala kifahari!! Tunapigwa tozo Sisi tuliokosa vyote hivyo ili kukuongezea ufahari na kufanya utakalo chini ya jua, wenzio hatuna hata malapa ya kuendea shule na shambani wakati wewe, mkeo watoto mnabadilisha mahari Kama mashati!!?. Then unatuletea uzi wa kipuuzi namna hii. Wewe shangilia, piga magoti, lambs viatu Ni wewe. Sisi tuache kitupaka matope na kututafuta maneno.

Kama unampenda sana mkaribishe nyumbani kwako umuonyeshe ufahari wako na mumtukuze.

Wengine Mungu wa mbinguni anatupigania na atatuokoa na huu utawala wa genge dhalimu la kutukuzana na kusifiana.

Ushindwe kwa jina Yesu Mnazareti.
 
Tozo Ni kwa maendeleo ya Taifa letu, usizani mataifa yaliyo endelea yalikaa yakashushiwa maendeleo toka angani, fahamu kuwa walijibana walijinyima walijifunga mikanda na kuchangia kwa kadli ya kila mtu alivyo jaliwa kipato chake kuzijenga nchi zao mpaka kufika hapo walipofika Leo hii, hutaki kulipa tozo na Kodi halafu hapo hapo unataka Elimu Bora na huduma Bora za Afya, je unafikiri vinatoka wapi Kama tusipokubali kuwa wazalendo katika kuijenga nchi yetu? Unazani Nani atabeba wajibu wetu wa kuijenga nchi yetu?
 
Chawa naona unaweka gazeti baada ya gazeti ukiamini utampatia mama na CCM mvuto. Kwa taarifa yako CCM sio chama cha kizazi hiki, ndio maana kimebaki kujishikisha kwenye vyombo vya dola.
Mvuto alio nao mh Rais wetu mpendwa mama Samia pamoja na CCM hata Kama ukiitishwa uchaguzi Leo hii na mama asipige kampeni bado atapitaa kwa kishindooo kikuu hata Kama itasimamia tume ya aina gani

CCM sio chama cha kizazi hiki, hivyo vyombo vya dola pekee ndio pumzi yenu ya mwisho fullstop.
 
Hakika imefikia mahala watu tunaskip kusoma mahekaya kumhusu Kiongozi wa nchi ambaye ameamua kusimama na wanaotesa raia.

Tuseme hapana kwa hizi sifa ambazo hazina merits zozote
 
Hakika imefikia mahala watu tunaskip kusoma mahekaya kumhusu Kiongozi wa nchi ambaye ameamua kusimama na wanaotesa raia.
Kwa akili zake fupi anadhani anamsifia kumbe ndio anazidi kumsagia kunguni kwa wananchi! Fikiria unamtaka mwananchi eti naye asifu chanzo cha mateso anayopitia, hizi ni akili za wapi?
Tuseme hapana kwa hizi sifa ambazo hazina merits zozote
Laiti angejua mbegu za hasira anazozidi kuzipanda vichwani mwa wananchi kupitia haya magazeti yake humu, huyu mpuuzi asingethubutu kuendelea na hizi hekaya zake za kijinga.
 
Watu wanawaza pisi kali na ubuyu ndo wanaoewa kazi ya kupiga pambio.

Kaazi kweli kweli
 
Hakika imefikia mahala watu tunaskip kusoma mahekaya kumhusu Kiongozi wa nchi ambaye ameamua kusimama na wanaotesa raia.

Tuseme hapana kwa hizi sifa ambazo hazina merits zozote
Hapana ndugu yangu Msanii, lazima tuseme ukweli penye kuhitaji kusema ukweli, Rais Samia kwa namna alivyoipokea nchi na katika mazingira yaliyokuwepo ya kiuchumi wa Dunia na hapa alipotufikisha kiuchumi hakika Anastahili pongezi kubwa Sana, Anastahili kupewa faraja, Anastahili kupewa ushirikiano na kuungwa mkono nasi watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…