Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake
Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.
Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.
Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.
Halafu kazi mojawapo ya rais ni kuleta utengamano katika nchi hata kama unapata upinzani kiasi gani kauli za utata kama hizi angeshauriwa aziepuke maana hizo ndiyo zilizomfanya mwendazake kuchukiwa
Kasema ukikaa ki uadui..sio kila anaepinga adui...sio kila upinzani ni uadui ....adui ni Yule anaepinga kila kitu...mtu analalamika mgao ...akiambiwa tumenunua mitambo ya gesi kuondoa mgao hataki pia ..anataka tusubiri bwawa la Nyerere...sasa watu Aina hiyo ni wazalendo au wanafiki

Unaenda uwanja wa vita kwa mapambano wakati bado hujamjua adui ni nani!? Vita itakapoanza ndio utashabgaa adui ni yule ambaye ulikuwa upande wako na msaada wako ndio yule ambaye umeelekeza silaha zako kwake.