Pre GE2025 Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kumsamehe Mbunge wa Bumbuli January Makamba akisema Mama ukimkera anakupiga kikofi na kukukufichia chakula na hivyo amekiri kuwa alimpiga kikofi January lakini leo February 24,2025 ametangaza kumsamehe na kumrudisha January kwa Mama.

Rais Samia ametangaza msamaha huo kwa January Makamba leo wakati akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga ambapo amemuita pia January na kumkumbatia kwa furaha mbele ya Wananchi.

β€œMwisho kabisa nataka nimuite Mwanangu January hapa aje huku, arudi kwa Mama, sisi Wamama mnatujua, ukimkera Mama anakupiga kikofi anakufichia chakula si ndio?, sasa Mwanangu nilimpiga kikofi nikamfichia chakula lakini leo namrudisha kwa Mama.. haya Mwanangu”

My Take
Hicho chakula ndio yale mavyakula ya kula kwa urefu wa kamba?
 
Kwa hizi kauli Tanzania itaibiwa na kupigwa vikofi kwenye rasilimali Hadi iombe poooo
 
Nimesikia leo huko Tanga kwenye Ziara ya Mama akirudishwa kwa Mama.

Wenye kujua watujuze huyu Mtoto alifanya nini kikamkera Mama hadi kufikia kupigwa kikofi na kufichiwa Chakula?
Fitina za makundi ya wasaka Urais.

Nasubiria gazeti la Kigogo media
 
January na Nape ni machawa wenye entitlement syndrome. Wanastahili kuachwa wale vumbi jumla kama Ibilisi alivyoachwa na Mungu jumla!
 

Vijimaneno jamani pelekeni huko Zenj sisi tunahitaji mambo matatu makubwa
1. Rushwa ipigwe kwa nguvu zaidi
2. Mikataba ya siri ya umma ikome
3.Tume huru ambayo sio ya Raisi
 
Makambako tena?

Makambako huyu huyu asiyeweza chochote zaidi ya kunyemelea 10% kwenye mikataba ya kihuni??
 
🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯β˜ οΈβ˜ οΈβ˜ οΈβ˜ οΈβ˜ οΈβ˜ οΈβ˜ οΈπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘½πŸ‘½πŸ‘½πŸ‘½πŸ‘½πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­
 
Ndio maana marekani waliona bora wampe urais kichaa mwanaume urais kuliko kumpa mwanamke!
Waliona mbali!.
Na kwa msisitizo, wamefanya hivyo mara 2,
2016 dhidi ya Hilary Clinton & 2024 dhidi ya Kamala Harris
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…