Mama wakati mwingine sijui huwa inakuaje?!!!
Hivi huku kuongea ni lazima kwani kila jambo?!!!
Maswala ya afya ni ya kila siku na kila leo kuna jipya linaibuka......sasa kuna corona, kesho kutakuwa na jingine AMBALO LITAHITAJI WAZALENDO WA KWELI HASWA WA KUJITOLEA KAMA HUYO MTUMISHI. Kauli kama hii itapunguza mno morali na idadi ya watu wazalendo kama hao ambao hata kabla ya hii kauli walikuwa wamepunguzwa kwa kiasi kikubwa na siasa za miaka yetu ya hivi karibuni. Akumbuke pia kuwa huku chini kuna wavivu wa kupitiliza, ambao kauli km hizo kwao ni sherehe kubwa kwani inawapa 'excuse' ya uvivu wao.
Kuna watu huku vijijini wanalazimika kwenda porini na machine zao kufuatilia mapato, kuna watendaji huku hulazimika mpaka kuogelea kupambania mapato ya serikali, kuna walimu huku wanafundisha kuanzia asubuhi mpaka saa mbili usiku na hadi weekend (kwa kujitolea) kuokoa taifa lao huku wakivumilia dhihaka na matusi meengi huko mtaani na humu mitandaoni kutoka kwa wanafunzi wao waliowafundisha na kufanikiwa kimaisha, kwa matarajio kwamba angalau wakubwa wao wataappreciate na kuwapa faraja; ghafla bin vuu anasikia mwenzake anabezwa hivyo. Hili hata mimi limeniuma sana, nikiwa mmoja wa watumishi wa daraja la chini kabisa ninayefanya mengi na makubwa kwa kujitolea tu.
Wakubwa inabidi wawe waangalifu kweli katika kauli zao sababu zinapenya na kuathiri kila pembe. Akimwambia mkuu wa mkoa wa iringa, ''sitaki unyanyase mama ntilie hapa!'' Tafsiri yake ni kuwa amemwambia kila mkuu wa mkoa, kila waziri, kila mkuu wa wilaya, kila mkurugenzi na watendaji wengine wote na hata watu binafsi kutofanya hivyo. Vivo hivyo, kumwambia mtumishi huyo 'shujaa wa taifa' hivyo tafsiri yake ni kuwa amebezwa kila mtumishi anayetoa 'extra to the ordinary'.
Katika kipindi chake hiki cha mpito na ukinzani wa hapa na pale kutoka kwa 'walimu waliofungua mashule ya uongozi' na wale watamanio tu kushindwa kwake, wazalendo km hao ndio watakaofanikisha ajenda zake hivyo wanahitaji kupewa moyo sana tu. Sipati picha, huyo mtumishi leo ana hali gani huko aliko (na tabia zetu hizi za kiswahili za kung'ong'ana huku uswahilini.