#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

Chanjo ni muhimu sana tuache ujuaji...Binadamu tunatofautiana wengine miili yao ni konki ,ina kinga ,carrier so tusiwaige wao na kutupoteza maboya, kama wewe mwili wako "MPESEMPESE" likipa vumbi la mafua imoo ,vumbi la kifua imooo,vumbi la kuhara imoo, vumbi la malaria imoo basi nenda kachanje.
 
Wangefanya hivyo na kwenye kukusanya maoni ya wananchi kwenye issues mbalimbali kama katiba, utawala bora, n.k

Yaani uwe ni utamaduni wa kukusanya maoni ya watu kwa maamuzi ya kitaifa...
 
Chanjo ni muhimu sana tuache ujuaji...Binadamu tunatofautiana wengine miili yao ni konki ,ina kinga ,carrier so tusiwaige wao na kutupoteza maboya ,kama wewe mwili wako "MPESEMPESE" likipa vumbi la mafua imoo ,vumbi la kifua imooo,vumbi la kuhara imoo,vumbi la malaria imoo basi nenda kachanje.
Na hata yule mburula Stephen Harmon kutoka CA aliyekuwa analeta mzaha kwenye chanjo, watu "washakula wali" kitambo!
 
Inasikitisha sana kuona mtumishi wa Afya aliyejitoa bila hata kulipwa katika kuhakikisha jamii inapata chanjo na kuweza kutoa chanjo kwa watu 160 anabezwa badala ya kupongezwa...This is dissappointing...
Huyo mtumishi kufuata watu majumbani kunaondoaje mazingira ya watu kukubali kutokana na intimidation, kama watu wameridhia kwa dhati hizo hanjo zingeisha siku ya kwanza bila hata uhamasishaji wowote.

Msidanganye kwamba ni hiyari wakati mkiweka mazingira ya kuwatisha watu ili wachanjwe kwa kuhofia kuwa sanctioned......na hili tumelishuhudia jana kwa katibu mkuu afya kutoa amri kwa watumishi wa umma kuchanja.
 
Inasikitisha sana kuona mtumishi wa Afya aliyejitoa bila hata kulipwa katika kuhakikisha jamii inapata chanjo na kuweza kutoa chanjo kwa watu 160 anabezwa badala ya kupongezwa...
Amesema vizuri tu kama umepewa elimu ya chanjo hakuna hiari ,kiufupi chanjo ni lazima
 
Hujielewi. Unahitaji elimu is alivyosema Raisi.
Wala sihitaji elimu yoyote, aliyemuelimisha atakayekuelimisha kaelimishwa na muuzaji wa chanjo, na sio kaelimishwa kakaririshwa
 
Na muachage ubishi maana gwajifix aliwaambia chanjo ni noma mkaanza kuhangaika naye sasa waliochanjwa ndio wanapukutika kama majani , ni suala la muda tu tusubiri tutayaona
 
Mama wakati mwingine sijui huwa inakuaje?!!!

Hivi huku kuongea ni lazima kwani kila jambo?!!!

Maswala ya afya ni ya kila siku na kila leo kuna jipya linaibuka......sasa kuna corona, kesho kutakuwa na jingine AMBALO LITAHITAJI WAZALENDO WA KWELI HASWA WA KUJITOLEA KAMA HUYO MTUMISHI. Kauli kama hii itapunguza mno morali na idadi ya watu wazalendo kama hao ambao hata kabla ya hii kauli walikuwa wamepunguzwa kwa kiasi kikubwa na siasa za miaka yetu ya hivi karibuni. Akumbuke pia kuwa huku chini kuna wavivu wa kupitiliza, ambao kauli km hizo kwao ni sherehe kubwa kwani inawapa 'excuse' ya uvivu wao.

Kuna watu huku vijijini wanalazimika kwenda porini na machine zao kufuatilia mapato, kuna watendaji huku hulazimika mpaka kuogelea kupambania mapato ya serikali, kuna walimu huku wanafundisha kuanzia asubuhi mpaka saa mbili usiku na hadi weekend (kwa kujitolea) kuokoa taifa lao huku wakivumilia dhihaka na matusi meengi huko mtaani na humu mitandaoni kutoka kwa wanafunzi wao waliowafundisha na kufanikiwa kimaisha, kwa matarajio kwamba angalau wakubwa wao wataappreciate na kuwapa faraja; ghafla bin vuu anasikia mwenzake anabezwa hivyo. Hili hata mimi limeniuma sana, nikiwa mmoja wa watumishi wa daraja la chini kabisa ninayefanya mengi na makubwa kwa kujitolea tu.

Wakubwa inabidi wawe waangalifu kweli katika kauli zao sababu zinapenya na kuathiri kila pembe. Akimwambia mkuu wa mkoa wa iringa, ''sitaki unyanyase mama ntilie hapa!'' Tafsiri yake ni kuwa amemwambia kila mkuu wa mkoa, kila waziri, kila mkuu wa wilaya, kila mkurugenzi na watendaji wengine wote na hata watu binafsi kutofanya hivyo. Vivo hivyo, kumwambia mtumishi huyo 'shujaa wa taifa' hivyo tafsiri yake ni kuwa amebezwa kila mtumishi anayetoa 'extra to the ordinary'.

Katika kipindi chake hiki cha mpito na ukinzani wa hapa na pale kutoka kwa 'walimu waliofungua mashule ya uongozi' na wale watamanio tu kushindwa kwake, wazalendo km hao ndio watakaofanikisha ajenda zake hivyo wanahitaji kupewa moyo sana tu. Sipati picha, huyo mtumishi leo ana hali gani huko aliko (na tabia zetu hizi za kiswahili za kung'ong'ana huku uswahilini.
 
Haya maneno hajayasema, alichosema hakuna kumlazimisha mtu chanjo na hiyo ya nyumba kwa nyumba amehofia ufanisi wake. Alichosema ni watu wapewe elimu na sio kuwalazimisha.
Hii ni afadhali mama kakataa. Ninajua watumishi wa afya walivyo. Wakifika huko lazima wanalazimisha ili wafikie target [emoji457].

Lakini najiuliza hivi unafika nyumba ina adult wote afu wote wanachanja afu baada ya hapo wanaanza kupata changamoto ingawa hatuombei nani atatunza mwenzake. Na tukumbuke kuwa ukichanja chanjo hii madhara yakitokea ni yako wewe na familia yako.


Hebu tijitafakali. Chanjo siyo dawa ni kinga tu. Tuache watu waendelee kufuata wao wenyewe wanapo hitaji. Ila mama anajiwekea kitanzi kampeni zake zitakuwa ngumu sana 2025 as far ameshatangaza atagombea.
 
CCM mbona wanamchezea sana mama?

Alisema magezeti yafunguliwe - wakamgomea wanazidi kuyafungia
Akasema machinga wasiguswe - wamegoma
Akasema chanjo hiari - Wanamgomea
Akasema tozo zisiumize wananchi - wamepunguza kidogo tu hence wamemgomea kiaina
Amesema watu waruhusiwe kufanya shughuli za kisiasa - wamemgomea

Hawa CCM wakoje? hawaogopi dola.
 
Kaitafute!! jukwaa hili ni la GTs only.
Kama ulichofanya ndo u-GT wenyewe, then I better not become the so-called GT cuz' being one, sounds like having inability to present complete information!
 
Kama ulichofanya ndo u-GT wenyewe, then I better not become the so-called GT cuz' being one, seems like being unaware of what you actually need to present!
Mimi siwezi kukuekezea kama mwanakijiji wa Kitonga.
I expect uwe na ABC za kila mada
 
Haya maneno hajayasema, alichosema hakuna kumlazimisha mtu chanjo na hiyo ya nyumba kwa nyumba amehofia ufanisi wake. Alichosema ni watu wapewe elimu na sio kuwalazimisha.
Sasa kama ndo alichosema, sasa tatizo lipo wapi?!

Kauli ya serikali hadi sasa ni ile kwamba "chanjo ni hiari"!

Kama inaonekana ni muhimu kufanya iwe lazima, watalaamu waantakiwa kuishauri serikali OFFICIALLY kwanini iwe lazima!!

Hilo likitokea, na kukubalika, serikali tena itatangaza kwamba chanjo ni lazima lakini sio eneo moja TU anatokea mtu anatangaza kwamba chanjo ni lazima!!

Au kama wahusika wa eneo husika waliona umuhimu wa kufanya chanjo iwe lazima kwa eneo lao, basi walitakiwa kutoa ombi kwa mamlaka husika la kwanini wangependa chanjo kwenye eneo lao iwe ni jambo la lazima!!

Halafu mambo mengine ni uzwazwa, na ndo maana hata hao serikali wenyewe kwa sasa hawawezi kufanya iwe lazima!!

Unaanzaje kuamuru chanjo iwe lazima wakati vichanjo vyenyewe vipo ONLY 1M kwa sasa huku Watanzania tukiwa mamilioni!!

Sasa ukifanya ni lazima wakati chanjo ni chache si ndo mwanzo unaishia kuchanja wasio na uhitaji mkubwa, huku wenye uhitaji mkubwa wakiwa wamebaki kwa mamilioni bila kuchanja na kuanza kusubiria chanjo zingine za HISANI YA WATU WA MAREKANI!!
 
Mimi siwezi kukuekezea kama mwanakijiji wa Kitonga.
I expect uwe na ABC za kila mada
Ngoja nikupuuze GT fake, manake kama hilo nalo linatafsiri how GT you're, busara ni kukupuuza! No wonder hata ka-thread kenyewe kameunganishwa kwenye thread zinazo-make sense!!!
 
Back
Top Bottom