#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

Ukweli usemwe na maamlaka za juu bwana yule alipotosha watu ili iwe rahisi waandamizi kutoa elimu covid na Chanjo.
Wewe ukichoma si inatosha, utabaki wewe na wengine waliochanja...

Mamlaka ipi ya juu wakati mamlaka hii ndio ile ile iliyokuwepo tofauti tu ni kwamba kiongozi wa juu alifariki???

Elimu ya kuhusu chanjo mamlaka imejitaidi sana kutoa sidhani kama yaweza laumika tena kuhusu jambo hili
 
mbn mama kasema wazi watu wasilazimishwe sasa swala la yeye kushauriwa vibaya linatoka wapi? mbn ni kama unajichanganya mkuu? sasa hp mtu unalaumu nn au tu ndio mmeamua kukosoa na kulaumu tu chochote kile jmn duh!
 
Ukweli unaujuwa, ila mimi namuunga mkono Mama mia kwa mia, tulikuwa kwenye mikono ya washamba na makatili.

Wanamchukia mama ni kupungukiwa tu busara, tupime miaka 6 ya ukatili na miezi 6 ya huyu mama bora ipi?

Huyu mama anahitaji kupewa sapoti, kwanza ngoja tulisambaratishe kundi la mumiani wa Sukuma gang ndio turudi kwenye harakati.

Siko tayari kumuhujumu mama kuwapa nguvu mashetani wa Sukuma gang, ni heri haya majizi ya msoga huwa yanakula huku yanatuachia makombo kuliko hawa Sukuma gang ni makatili na wauwaji wakubwa.
Wewe ni ken.e,
 
Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu wa mkoa wa mbeya.

Swali hizo cost zinazotumika kulazimisha watu wachanjwe zinatoka wapi? Kwanini pesa zisielekezwe kwenye mambo mengine ya msingi.

Mama wanaomshauri wanamponza Sana.

---
Rais Samia Suluhu, amemzungumzia mhudumu wa afya anayepita nyumba kwa nyumba kuchanja chanjo ya Uviko-19, akionya kampeni hiyo isitumiwe vibaya katika kuwalazimisha watu kuchanja.

Jana katika mitandao ya jamii, kulisambaa habari na picha ikimuonyesha Ofisa wa Afya wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma akipita nyumba kwa nyumba kuwachanja chanjo ya Uviko 19 watu zaidi ya 160 kwa siku moja.

Akizungumzia leo Septemba 27, 2021 katika mkutano mkuu maalum wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma hilo, Rais Samia amesema asingependa kuona suala hilo likifanyika kwa mabavu kwa kuwalazimisha watu kuchanja.

Amesema kati ya mambo ambayo angependa ALAT kulishughulikiwa kwa kasi kubwa ni suala la mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 ikiwemo utoaji elimu.

“Juzi na jana nilivyoingia nchini nimekuta hii agenda ya watu kupita nyumba kwa nyumba na mikoba ya sindano kuchoma watu.

“Tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome, asiyetaka usichome, lakini kubwa nalotaka kusema mtu hana mamlaka ya kukubali au kukataa kama anayo elimu.

“Kwani kama ana elimu yakutosha hawezi kukataa, lakini hana elimu unapita tu na mkoba wako unamwambia nikuchome nisikuchome, atakuambia usinichome,” amesema Rais.

Amewataka wahudumu wa afya kutoa elimu ya afya kwa wingi ili wananchi waone umuhimu wa kuchanja.

“Asipoona hilo hawezi kuona uchungu wa hili suala, nendeni kafanyeni kampeni kubwa watu wakubali kuchanja msiende kufanya kwa mabavu. Tupunguze vifo vinavyotokana na ugonjwa,” amesema.

Aidha amesema ndani ya nchi yetu kuna matatizo makubwa matatu na hili la uviko limejitokeza ni la nne.

Ametaja magonjwa mengine kuwa ni TB, HIV na malaria na kueleza kuwa yameshughulikiwa kwa kiasi kikubwa na kuagiza janga la Uviko-19 lishughulikiwe na watu wapate kinga.

Chanzo: Mwananchi
Ndipo nampo mpendea Mama Samia. Mungu ambariki sanaaaa!
 
KUNA MAHALI KAMA SIJAMUELEWA. AU NI KWA7BU YA UELEWA WANGU MDOGO. AMESEMA KUCHANJA SIYO LAZIMA, BALI NI HIARI. WANACHI WAPEWE ELIMU KWANZA NDIPO WACHANJWE. LAKINI KWA MWENYE ELIMU (nadhani ya corona) HANA HIARI KATIKA KUCHANJWA. YAANI LAZIMA ACHANJWE. HAPA NDIPO NINAPOPATA MASHAKA. KWANN HUYU MWENYE UELEWA JUU YA MADHARA YA CORONA, KWAKE ASIWE NA HIARI DHIDI YA CHANJO? KWANI WATU WANAKATAA KUCHANJWA KWA KUKOSA ELIMU? AU WANALO WANALOLIHOFIA DHIDI YA HIZO CHANJO? NAHISI KAMA AKILI YANGU IMEFIKA MWISHO KULIELEWA HILI TUNALOLIENDEA
 
Lugha hizi za kupindisha pindisha kauli zinaleta mkanganyiko sana. Sijui ni kutojua kiswahili au tu kuepuka kusema maneno yaliyonyooka?

Maneno kama haya yana maana gani?

“Tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome, asiyetaka usichome, lakini kubwa nalotaka kusema mtu hana mamlaka ya kukubali au kukataa kama anayo elimu. Kwani kama ana elimu yakutosha hawezi kukataa, lakini hana elimu unapita tu na mkoba wako unamwambia nikuchome nisikuchome, atakuambia usinichome,” amesema Rais.
 
Pita nyumba kwa nyumba kama mlivyokua mnapita nyumba kwa nyumba kuomba kura.

Mtakayemkuta atachagua kuchanja au kutokuchanja.
 
Huyo naye kihelehele chake Cha kutafuta sifa. Umeshaambiwa ni zoezi la hiari.
 
Wanazi wa kutaka watu walazimishwe kuchanjwa,wakisikia rais anapinga mabavu,tumbo la kuhara linawashika lol.
 
Ukweli unaujuwa, ila mimi namuunga mkono Mama mia kwa mia, tulikuwa kwenye mikono ya washamba na makatili.

Wanamchukia mama ni kupungukiwa tu busara, tupime miaka 6 ya ukatili na miezi 6 ya huyu mama bora ipi?

Huyu mama anahitaji kupewa sapoti, kwanza ngoja tulisambaratishe kundi la mumiani wa Sukuma gang ndio turudi kwenye harakati.

Siko tayari kumuhujumu mama kuwapa nguvu mashetani wa Sukuma gang, ni heri haya majizi ya msoga huwa yanakula huku yanatuachia makombo kuliko hawa Sukuma gang ni makatili na wauwaji wakubwa.
Wewe inaonekana chanjo imeisha kuvuruga ubongo,sikwa povu hili, inabidi upigwe boats ili akili ikae sawa,moja haitoshi
 
Hizo chanjo zinakaribia ku expire huu mzuka wote ni frustrations za kutaka mzigo uishe, huko ni mwendo wa kushurutisha watu kwa maneno ya hapa na pale ili wawe na hofu ya kugomea zoezi, kifupi wanachofanya ni intimidation kwani watu wanakuwa hawako huru kufanya maamuzi kwa kuhofia kuwa sanctioned tunawasubiri huku kwa watumishi wa umma waje kupambana na visiki.
 
Back
Top Bottom