Huku vijijini watu wanaogopa Sana serikali,Nani kasema anapita kulazimisha! anapita nyumba kwa nyumba kuelimisha na kufikisha chanjo kwa watu. Huyu anatakiwa kupongezwa kwa kuokoa maisha wa watu vijijini sio kumtungia vitu. Kama mtu anachagua uwezekano wa kufa kwa huu ugojwa huwezi kulazimishwa maana hata ukiumwa malaria ni wewe wa kuamua kunywa dawa lakini haibadilishi ukweli kwamba chanjo ni muhimu. Lakini kingiwa watu wengi hawajui kuna wanaokufa kwa corona hata hawajui hasa vijijini kwasababu wana magojwa mengine
Kitachotokea hapo ni wanakijiji wengi kuchoma kwa kuhofu!
Ukitaka kuamini hilo, ni kwamba operation ya nyumba kwa nyumba itafeli mijini lakini vijijini wengi watachoma, na si kwamba vijijini ni waelewa
Elimu watayokwenda nayo ni "Rais kasema,... "Tumuunge mkono mama yetu... "Tuunge mkono serikali ya CCM...." na vijijini wanashabikia CCM kishamba kabisa... Na utakuta kwenye msafara wanaambatana na katibu wa CCM...
Ila chonde, chonde asichomwe mtu akafa kwa sababu yoyote ile...