#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

Nani kasema anapita kulazimisha! anapita nyumba kwa nyumba kuelimisha na kufikisha chanjo kwa watu. Huyu anatakiwa kupongezwa kwa kuokoa maisha wa watu vijijini sio kumtungia vitu. Kama mtu anachagua uwezekano wa kufa kwa huu ugojwa huwezi kulazimishwa maana hata ukiumwa malaria ni wewe wa kuamua kunywa dawa lakini haibadilishi ukweli kwamba chanjo ni muhimu. Lakini kingiwa watu wengi hawajui kuna wanaokufa kwa corona hata hawajui hasa vijijini kwasababu wana magojwa mengine
Huku vijijini watu wanaogopa Sana serikali,
Kitachotokea hapo ni wanakijiji wengi kuchoma kwa kuhofu!
Ukitaka kuamini hilo, ni kwamba operation ya nyumba kwa nyumba itafeli mijini lakini vijijini wengi watachoma, na si kwamba vijijini ni waelewa

Elimu watayokwenda nayo ni "Rais kasema,... "Tumuunge mkono mama yetu... "Tuunge mkono serikali ya CCM...." na vijijini wanashabikia CCM kishamba kabisa... Na utakuta kwenye msafara wanaambatana na katibu wa CCM...

Ila chonde, chonde asichomwe mtu akafa kwa sababu yoyote ile...
 
Wengi chanjo imewaua.

Unakosea sana kumdhihaki Dkt Magufuli. Na ndipo tunapotofautiana. Hata Yesu aliishi na kufanya kazi miaka mitatu na wakamuua. Ila mpaka leo wewe ni shahidi injili ya Yesu Kristo inahubiriwa kila pembe ya dunia...
Wakumbuke JPM ni mkombozi wa CCM iliyokuwa imeoza na kutemewa mate mitaani. Bado watu Kama JPM wanahitajika ktk CCM

Wakikosekana akina JPM chama kitakufa tu.

Kumpamba na kumsifu Rais hakusaidii kukiheshimisha chama.

JK alisifiwa na kutetewa na CCM lakini chama kiliendelea kudhoofika
 
KUNA MAHALI KAMA SIJAMUELEWA. AU NI KWA7BU YA UELEWA WANGU MDOGO. AMESEMA KUCHANJA SIYO LAZIMA, BALI NI HIARI. WANACHI WAPEWE ELIMU KWANZA NDIPO WACHANJWE...
Maana yake mtu akipewa elimu lazima achanjwe!

Kwahio inabidi tuikatae na elimu
 
Updates: Mleta hoja alikuwa mnafiki na alilenga kuchonganisha Mh. Rais na sisi wana CCM. Ujumbe wangu ulidhani Mh. Rais amesisitiza ifanyike lazima, kumbe kaonya isiwe lazima. Namuunga mkono Mama na ninatengua kauli yangu ya maandishi na kuufuta huu ujumbe hapo chini. Mungu ambariki Mama SSH, ni yeye 2025!

Naomba Mod mpigeni BAN mleta maada alileta habari nusu yenye kutuchonganisha sisi wana CCM na rais wetu huku akijua rais katahadhalisha kuhusu chanjo na hakulazimisha.
Tulia wewe.....ati bani?
 
Watu wanalinda ugali wao kwa kutumia gharama ya wengine bhana... Usione ajabu hao wanaopita nyumba kwa nyumba wao hawajachanja
 
Huku vijijini watu wanaogopa Sana serikali,
Kitachotokea hapo ni wanakijiji wengi kuchoma kwa kuhofu!
Ukitaka kuamini hilo, ni kwamba operation ya nyumba kwa nyumba itafeli mijini lakini vijijini wengi....

Chanjo hata sisi tukiwa wadogo wazazi wetu walilazimishwa kutuchoma chanjo na hii ndiyo maana sisi ni wazima leo. Ilimradi tunauhakika chanjo zinaokoa maisha sioni ubaya kuchoma watu wa vijijini.

Mimi sipendi sana matabaka wazazi wangu wanaokaa ununio yaani siku ya pili tu wamepata chanjo lakini inatakiwa Watanzania wote wapate huduma sawa.

Kiukweli kabisa chanjo ya covid inatakiwa kuwa lazima hasa kwa watu wazima. Mimi nipo hapa Texas hospital zimejaa wagojwa na 95% ni ambao walikuwa wabishi kuchanja sisi wengine tuliochanja tunadunda tu.

Na ziko poa wamechanja watu milioni 200 ! hakuna issue yeyote. Tuacheni uzushi inasikitisha sana watu kufa kwa sababu kama hizi za uongo ni aibu sana kwa binadamu.
 
habari kubwa mitandaoni sio chanjo nikuaibika kwa fulish mahakamani kufuatia Kari ya ugaidi inayoendelea!

Kenya pamoja na maukabila yao hawatendeani unyama huu kisa siasa! Tuendako ni kubaya saaana... Tunahitaji kiongozi mwenye hofu ya Mungu atayeondoa dhulma mbaya na mateso dhalili kwa wanasiasa hasa wa upinzani bila kutanguliza tamaa zake za uongozi.
 
Inasikitisha sana kuona mtumishi wa Afya aliyejitoa bila hata kulipwa katika kuhakikisha jamii inapata chanjo na kuweza kutoa chanjo kwa watu 160 anabezwa badala ya kupongezwa...This is dissappointing.

Viongozi wa Siasa wawe wanaconsult wataalamu kabla ya kutoa kauli. Nijuavyo hakuna anayechanja bila kuridhia na kuna fomu maalumu ya kufanya hivyo.

Watumishi wa Afya wamefanya kazi kubwa usiki na mchana tangu mlipuko wa korona uanze hawajalipwa stahiki zao mbalimbali ni mbaya sana kuendelea kuwabeza badala ya kutambua mchango wao.

TUJISAHIHISHE
 
Twende na Mama, nani kama Mama.

#MAMA 2025.
 
KUNA MAHALI KAMA SIJAMUELEWA. AU NI KWA7BU YA UELEWA WANGU MDOGO. AMESEMA KUCHANJA SIYO LAZIMA, BALI NI HIARI. WANACHI WAPEWE ELIMU KWANZA NDIPO WACHANJWE. LAKINI KWA MWENYE ELIMU (nadhani ya corona) HANA HIARI KATIKA KUCHANJWA. YAANI LAZIMA ACHANJWE. HAPA NDIPO NINAPOPATA MASHAKA. KWANN HUYU MWENYE UELEWA JUU YA MADHARA YA CORONA, KWAKE ASIWE NA HIARI DHIDI YA CHANJO? KWANI WATU WANAKATAA KUCHANJWA KWA KUKOSA ELIMU? AU WANALO WANALOLIHOFIA DHIDI YA HIZO CHANJO? NAHISI KAMA AKILI YANGU IMEFIKA MWISHO KULIELEWA HILI TUNALOLIENDEA
Usichanje, we elewa tu kwamba kwa sasa kama hutaki kuchanjwa hulazimiki kuchanja.

Sijachanja kwa sababu sijajua hii chanjo nia yake ni nn ila nitakapokuwa na amani nitachanja.
 
Mie ukinifuata nyumbani nachanja, nimebanwa na maisha hata kuitafuta chanjo sifikirii, kama kuna kampeni hiyo iendelee!
 
amezingua hata haeleweki anataka nn sasa kwenda nyumba kwa nyumba kuna kosa gan?
 
Huyu Mtumishi katimiza wajibu wake Kama vile Mwalimu anavyofundisha watoto 200 darasa moja badala ya 45.
Kumbe mnadai marupurupu ndo maana mmeamua kutusaka Kama tumbili.
Hatuchanjwi mtatembea Sana mwaka huu.
Utafikiri mtu akichanjwa hataambukizwa.
 
Back
Top Bottom