Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Anataka na yeye aitumie katiba iliyopo ya kifalme! Rangi halisi yaanza kuonekana hata mwezi bado!!
 
Sio tu nia njema

Kuanzisha Mchakato wa Katiba mpya hasa kwa nchi kama Tanzania kila mtu anajua kila kitu inahitaji uwe na 'Strong Political Muscles' kama Jk, otherwise unaweza ukachanganyikiwa
JK mwenye aliikimbia. Wanasiasa wengi hawajui kuweka maslahi ya nchi mbele na kama ukiwa Rais mwenye akili timamu muda wa kuanzisha mchakato wa katiba mpya bado hujafika tujifunzeni kwa majirani.
 
Wanajukwaa ni zaidi ya mara mbili mama huwa anakosea, anapohutubia na kusema Bunge la Katiba badala ya kusema Bunge la bajeti, sasa je mzimu wa Katiba Mpya bado unamsumbua hasa baada ya leo kusema kuwa anapata ' push' nyingi kuhusu Katiba Mpya lakini kwa hilo wasahau kidogo.

Nini maoni yako?
Wasahau kidogo maana yake nini, katiba KWA manufaa ya nchi KWA Sasa ni lazima Wala haliwezi kua ombi Kama kweli kiongozi yeyote anadhamila ya dhati ya kulitumikia taifa,
 
Jana Mh Rais Samia alipokuwa akitoa nasaha zake na kutangaza mabadiliko madogo ya Baraza la mawaziri baada ya kiapo cha Dr. Mpango alitamka neno katiba mpya. Na leo baada ya kuwaapisha katibu mkuu kiongozi na mawaziri ametamka bunge la katiba mara mbili ingawaje inaonekana ni kwa bahati mbaya. Bila shaka yo yote ni wazi kuna kitu anawaza kuhusu katiba mpya kwa sababu maneno hayo hawezi kuyatamka bila kuwa na tafakari yo yote kichwani.

Tuzidi kuomba huenda itakuja siku isiyo na jina ataamua kuendeleza mchakato wa katiba mpya. Subira yavuta heri!
Kwa asili yake inawezekana akafumba macho
 
Acha kila mtu ajiprotect panapo bidi
Wengi wanaogopa katiba mpya inaweza kusababisha kupoteza nafas zao na heshima zao walizojijengea kama yuke rais wa ufaransa
 
Cha msingi ni kuweka pressure!

Vyama vya siasa viache kushiriki chaguzi za maigizo.

Civil societies lazima zikanyage mafuta.

Na wananchi tuamke. Tuache kushiriki chaguzi mpaka kitapoeleweka.

Halafu cha ajabu huyu mama alikuwa makamu mwenyekiti kwenye bunge la katiba, maana yake ni kwamba ama kipindi kile alikuwa haamini anachokifanya kuwa ni kwa maslahi ya nchi au sasa keshalewa madaraka kwa hiyo anafikiri kinachoweza kuendelea kumsaidia kumpa stimu zaidi ya ulevi huo ni kuendelea na katiba hii mbovu!

Huyu mama kafeli mapema sana kukataa katiba mpya, kiufupi hakuna hope yyote ya maana chini ya ungozi wake kama ataendelea kukaa kitu ambacho ni obvious!
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.

Naunga mkono hoja!

CCM mbele kwa mbele
 
Kwani ANAJALI?
Akikaza shingo kama alivyofanya mtangulizi wake, asitarajie kuacha historia ya maana. Akiurejesha na kuumalizia kwa matarajio ya Watanzania walio wengi, hakika atakumbukwa milele na vizazi vyote.
 
Back
Top Bottom