Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Rais Samia: Nimepigiwa sana kelele kuhusu Katiba, ila kwa sasa tusahau kwanza

Halafu cha ajabu huyu mama alikuwa makamu mwenyekiti kwenye bunge la katiba, maana yake ni kwamba ama kipindi kile alikuwa haamini anachokifanya kuwa ni kwa maslahi ya nchi au sasa keshalewa madaraka kwa hiyo anafikiri kinachoweza kuendelea kumsaidia kumpa stimu zaidi ya ulevi huo ni kuendelea na katiba hii mbovu!

Huyu mama kafeli mapema sana kukataa katiba mpya, kiufupi hakuna hope yyote ya maana chini ya ungozi wake kama ataendelea kukaa kitu ambacho ni obvious!
Ccm haiwezi kujinywesha sumu
Maana kukubali kufanya mabadiliko ya katiba ni sawa na kusema sasa ccm ndiyo mwisho wa kutawala
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16].
Nilijiuliza urafiki wa Samia na chadema umeanza lini.
BADO SIJAPATA JIBU
Utabakia hivyo hivyo na jiulize kwanini Mungu wenu Bashiru ametolewa pale ikulu hapo ndiyo utapata jibu la maswali yako.
 
Aaah kama kawaida yao.Ni Hadi akiwa nje ya mfumo ndo atajua umuhimu wa katiba.Yeye, polepole, bashiru,kabudi kabla awajakaribishwa mezani sio ndo walioimba wimbo wa katiba mpya.
Nimeamni ni Hadi utoke uwanjani ndo utayaona makosa yako.
 
Cha msingi ni kuweka pressure!

Vyama vya siasa viache kushiriki chaguzi za maigizo.

Civil societies lazima zikanyage mafuta.

Na wananchi tuamke. Tuache kushiriki chaguzi mpaka kitapoeleweka.
Kuacha kushiriki chaguzi ambazo washindi wameadaliwa.
 
Aaah kama kawaida yao.Ni Hadi akiwa nje ya mfumo ndo atajua umuhimu wa katiba.Yeye, polepole, bashiru,kabudi kabla awajakaribishwa mezani sio ndo walioimba wimbo wa katiba mpya.
Nimeamni ni Hadi utoke uwanjani ndo utayaona makosa yako.
Umeonaeeeeeeee?
Kabudi alikuwa anatoa macho kweli kwenye issue ya katiba mpya.

Polepole akawa anakandia nafasi za ma dc kuwa hazifai kuwepo kwenye mfumo wa uongozi wa nchi.
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
CCM ni ukoo wa kambale kila mtu ana masharubu, DJ mpya ila muziki uleule wa chama cha maibilisi wa kijani kibichi .
 
Wana JF

Raisi Samia wakati akiwaapisha mawaziri amesema kuwa amepigiwa sana kelele kuhusu katiba mpya, ila kwa sasa anaomba tusahau kwanza . Swali ni je kuna uwezekano mama akarudisha mchakato wa katiba au ndio hapa kazi tu .?

Haki huinua taifa.
Tunajua wanaopigia kelele Katiba mpya ni akina nani:makarai ya zege ya mafisadi.Wanadhani kupitia hiyo mabwana zao watapata nafasi ya kupenyeza agenda zao za kipuuzi zinazo husu ushoga,feminism,abortion,malezi ya watoto,mifumo kwenye familia nk.nk..However,sioni realistically what we cannot do with the 1977 constitution as far as bringing development to our people and protecting our hard earned peace is concerned.
Kinachotakiwa ni utashi tu wa kisiasa.Hongera Rais wetu Samia kwa msimamo wako.
 
Mama ameanza kuweka ndugu zake.Kaburu botha akukosemea kabisa kuhusu akili ya mtu mweusi juu ya undugu, ukabila na udini.
Asianze tu na yeye kujenga uwanja wa ndege international kijijini kwake.
 
Tulia kamanda! Kunywa maji ya uvugu vugu halafu msikilize tena Madam President!

CCM mbele kwa mbele
Alicho nifurahisha ni kukata ile mifereji iliyo kuwa inatumiwa na mtangulizi wake na hivyo kuwafanya baadhi ya watu wajiandae kuhama mji.
 
Jana Mh Rais Samia alipokuwa akitoa nasaha zake na kutangaza mabadiliko madogo ya Baraza la mawaziri baada ya kiapo cha Dr. Mpango alitamka neno katiba mpya. Na leo baada ya kuwaapisha katibu mkuu kiongozi na mawaziri ametamka bunge la katiba mara mbili ingawaje inaonekana ni kwa bahati mbaya. Bila shaka yo yote ni wazi kuna kitu anawaza kuhusu katiba mpya kwa sababu maneno hayo hawezi kuyatamka bila kuwa na tafakari yo yote kichwani.

Tuzidi kuomba huenda itakuja siku isiyo na jina ataamua kuendeleza mchakato wa katiba mpya. Subira yavuta heri!

Mmeambiwa kwa sasa msahau,au hukusikia?
 
Back
Top Bottom