Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Akifunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania, Viwanja vya Jeshi la Polisi CCP Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 17 Septemba, 2024.
Rais #SamiaSuluhuHassan akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi (TPS), amesema Serikali ina taarifa ya kikao cha chama cha Siasa anachodai kinalenga kufanya Siasa chonganishi na kuwa Serikali haitakubali hilo kwa kulinda Katiba na kuimarisha ulinzi wa maisha ya Watanzania.
Amesema “Kumepangwa kushusha moto hadi Samia aseme basi naondoka, hiyo Serikali au Serikali ya Samaki? Maana Samaki kadiri anavyokuwa mkubwa na akili inafanyaje? Serikali ya Tanzania haiondoshwi hivyo.”