"Ninalazimika Kusafiri nje ya nchi na Nitasafiri mno tu ili Kuwavutia zaidi Wawekezaji na kamwe sitokaa tu Ikulu ya Chamwino na Magogoni Kisha Watu wengine wanawadanganya Wawekezaji kuhusu Tanzania na tunawakosa kisha nchi yetu inazidi Kuanguka Kiuchumi" Rais Samia jana Kigamboni.
Chanzo: Radio One Nipashe Leo
Mlioko Rwanda, Ethiopia, Misri, Afrika Kusini, Kenya, Morocco na Botswana je, na Wao huko kwa idadi Kubwa ya Wawekezaji ( mpaka Watalii ) walioko na wanaoendelea Kufurika huko ni kutokana na Marais wao 'Kutalii' Ulaya, Marekani, Asia na Mashariki ya Kati Kuwatafuta?
Na je, kama Kazi ya Rais wa Tanzania ni Kusafiri sana Nje ya nchi ili kuwavutia Wawekezaji waje Tanzania nini Kazi ( Jukumu Mama ) la Mabalozi wetu walioko huko na Waziri wa Mambo ya Nje?
Mwisho kabisa GENTAMYCINE nauliza hivi Wawekezaji wanakuja nchini kutokana na Mazingira Rafiki ya Uwekezaji na Biashara ambayo huwa yanajitangaza tu yenyewe kutokana na Historia ya nchi husika Kisiasa na Kidemokrasia au yanamtaka Rais aanze 'Kuzunguka' kuwafuata?
Hata hivyo sishangai sana kama Mshauri Mkuu alikuwa Kinara wa Kukesha Angani huku akilala na kuamkia huko 'Majuu' kwanini na anayemshauri nae 'asiambukizwe' Utamaduni huo ambao kwa Wataalam wa Uchumi wanasema unaitia Hasara nchi / Serikali kwa Kugharamia 'Delegation' yake nzima.
Sijui na Mimi kwa Kusema na Kuhoji hili nitajumuishwa katika kile alichokiita Kikosi Maalum na cha Kimkakati cha Kumkwamisha na Kumuharibia alichokitaja huku akiwa amekasirika sana Juzi kule Mbagala.
Ewe Mwenyezi Mungu usiniache Baba!!