baadala ya kujengea uwezo watanzania wawekeze wenyewe unakwenda kuwaleta slave masters waje kuchukua slave wao na kuwaswaga...
Tuna eneo kubwa sana ambalo tukiwatumia hawa hawa watanzania nchi itakwenda mbele sana kwa kasi....
Jenga irrigation schemes kila kona ya nchi, shusha riba za mikopo kwenye mabenki mpaka chini ya 5%, yalete makampuni yajenge viwanda vya kuunganisha matractor na toa kodi kabisa na ushuru wa matraktor na zana zingine za kilimo... toa kabisa ushuru wa mazao huko mapolini...WAACHE WATANZANIA WALIME HALAFU UONE WATU WATAKAVYOLETA MAMELI KUNUNUA MAZAO YA KILIMO....
Serikali kupitia STAMICO ianze mara moja kuexplore maeneo ya uchimbaji na kutoa elimu kwa wachimbaji sambamba na usimamizi, muanze kukopesha vifaa vya uchimbaji na kodi iwe ndogo, mhamasishe watu wachimbe kwa kutoa usaidizi wa kitaalam na controlling kwenye maeneo yote ya uchimbaji.... serikali inunue madini kwa hata 50% na kuweka stock..
Serikali ipeleke vijana kwa kuwapa scholarship nchi mbalimbali wakajifunze skills mbalimbali sio kwenda kusoma PHD na degrees hapana short courses za kuacqure skills na pia hapa ndani vyuo vya veta viwekewe mafungu ya kutosha na kuwezeshwa kitalaam ili viweze kufundisha vijana wengi na serikali kutoa usaidizi wa mikopo kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo...
Unahitaji akili ndogo sana kuitoa Tanzania hapa na kuipeleka mbele, Vingine vyote Mwenyezi Mungu alishatenda kwa kutupa ardhi yenye kila kiti...