Rais Samia: Nitaifumua Wizara ya Mambo ya Nje

Rais Samia: Nitaifumua Wizara ya Mambo ya Nje

Anataka kufanya kwa maelekezo ya Makamba? Kama alivyonteua Maharage baada ya kufanyiwa usail na Makamba?


Mambo ni mengi mno, naona Makamba anepata chaka lingine la kupiga fedha za Umma kwa kisingizio cha ‘reform’ [emoji3][emoji3]

Halafu amwambie Makamba yule aliyempa tenda za Nguzo za zege zimeanza kukatika huku [emoji24][emoji24][emoji24]
Waliamua kuipa tenda Kampuni ya DERMA, eti kisa ni kampuni mzawa, of which ni kigogo wa utumishi, wakaacha kuangalia ubora.


Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Anamuogopa sana Marope yani kampa Ile wizara ila kutwa kumuandama, kamuondelea mabwana suti sasa haitoshi anataka tena aifumue fumue yani Marope atataseka sana kama awamu ya nne alimwambia akilamba FA ndo atapata connections 2025 basi hesabu zinaenda kuwa fakesl🤣🤣🤣🤣
 
Balozi zetu dah!

Kama huu uliopo hapa Washington DC. Hata NIDA wana unafuu. Sijui tatizo ni nini [emoji706][emoji706][emoji706]
Huyo kutwa yupo LinkedIn ku-post taarifa za magazeti ya Ulaya kama Afisa habari wa Ubalozi wakati yeye ni Blaozi.
Lakini jana Mama karopoka kuwa majina yanapelekwa kwake mengine wanamwambia ya Katibu Mkuu na yeye anakuwa na yake.Is this how government works globally!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Huyo kutwa yupo LinkedIn ku-post taarifa za magazeti ya Ulaya kama Afisa habari wa Ubalozi wakati yeye ni Blaozi.
Lakini jana Mama karopoka kuwa majina yanapelekwa kwake mengine wanamwambia ya Katibu Mkuu na yeye anakuwa na yake.Is this how government works globally!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Yaani ni aibu kubwa sn
 
Kuna mistake kubwa ilikwisha fanyika. Tujililie wenyewe. Kuchagua viongozi wetu hasa wakuu, isiwe kigezo cha majaribio.
Lazima mtu awe anafaa kukalia kiti. Lazima awe ni mtu mwenye kiasi na anayetambua ukubwa wa dhamana aliyopewa.
Viongozi huandaliwa na siyo mtu anaunda mtandao wake na majambazi wenzake wanatumia pesa chafu kununua uongozi, Baada ya Nyerere alipaswa afuate Jaji Warioba, Dr Salimu, Mkapa kwa mbali n.k
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa ataifumua na kuisuka upya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ili kuirudishia hadhi baada ya kuwa na utendaji usioridhisha kwa muda mrefu.

Hatua hiyo imekuja kutokana na wizara hiyo kupoteza ushawishi kwenye medani za kidemokrasia, huku mashirika ya kimataifa yakilalamika kutoridhishwa na utendaji wa wizara hiyo nyeti.

Rais Samia amesema hayo jana, wakati akipokea ripoti ya kamati ya kutathmini ufanisi na utendaji wa wizara hiyo, kazi iliyofanyika kwa miezi sita chini ya uenyekiti wa Balozi Hassan Simba Yahaya.

Amesema muundo wa wizara hiyo unaenda kuangaliwa upya, ikiwemo namna ya kuwapata watumishi wenye sifa stahiki, kwa kuwa wengi waliopo hawana uwezo.

Amesema kwa muda mrefu wizara imekuwa ikitawaliwa na urasimu katika kuajiri, hali iliyosababisha watu wasio na sifa kuajiriwa kwa maelekezo ya vigogo ndani ya wizara.

“Ripoti imeeleza hapo katikati ajira hazikuwa katika mpangilio mzuri, zilikuwa chache na zilitolewa kwa kujuana. Sasa mengine nayafahamu mie hata kwenye ripoti hayajawekwa, pia kuna makundi, hamisha hamisha na panga pangua ya maofisa waandamizi haya yote yalichangia utendaji wa wizara kupwaya.

“Hili ni moja ya masuala yanayonisukuma kutaka kamati hii uindwe na kuifanyia tathmini wizara, ubobezi ule wa miaka ya 90 na 2000 sasa wizarani hakuna, unguli, umahiri na ushawishi wetu kwenye medani za kidemokrasia umekuwa wa kujikongoja.

Kumekuwa na malalamiko kutoka taasisi za kimataifa zilizopo nchini kuhusu utendaji usioridhisha wa wizara hii,” amesema Rais Samia.

Pia aligusia uwakilishi wa nchi kupitia balozi zake katika mataifa mbalimbali akitaka mpangilio huo kuangaliwa upya kulingana na hali ya sasa.

“Tunapaswa kuangalia upya suala la uwakilishi wetu kupitia balozi tulizonazo nje ya nchi na hadhi zake kutokana na mabadiliko yaliyopo duniani. Wakati ule tulikuwa tunaanzisha balozi kwa kuangalia wanaotusaidia pesa nyingi, lakini mambo yamebadilika, lazima tuangalie wapi tuwe na balozi za kupewa nguvu,” amesema.

Sambamba na uwakilishi wa nchi, alizungumzia pia namna teuzi za mabalozi zinavyofanyika, huku akitaka jukumu hilo sasa wapewe watu wanaostahili na sio kwa kuoneana haya.

“Tunavyofanya sasa wizara inaleta mapendekezo, yanavyoletwa na mie nina yangu mkononi naletewa nani kaharibu wapi anaweza kupelekwa. Sasa hujui mapendekezo yapi ya kisiasa, yapi ya kitaaluma.

“Sasa hivi tufumbe macho anayevurunda kazini akae pembeni, hakuna haja ya kumpoza kumpeleka kwenye ubalozi, lakini pia nafasi za kisiasa hatusemi zisiwepo, lakini tuangalie kwa asilimia gani. Ila changamoto wakati mwingine hao wenye taaluma hawapo pale wizarani kwa sababu ya undugu uliojaa,” amesema.

Kufuatia hilo, kiongozi huyo mkuu wa nchi alielekeza kuwepo vigezo vya kuajiri watumishi katika wizara hiyo na kuondokana na mfumo uliopo sasa ambao unaruhusu watu wasio na sifa kubebwa.

“Hapa mkono wa Rais unakwenda kuingia kwenye hii wizara, tutaanzisha mfumo maalumu wa ufadhili wa kutengeneza vijana ambao watakwenda kufanya kazi pale.

“Haitakuwa rahisi, ni lazima wawe vijana wenye sifa, watafanya mitihani, wakifaulu ndiyo watawekwa kwenye fellowship hii kwa miaka miwili wakipikwa kisha tuwapeleke wakafanye kazi,” amesema Rais Samia.

Awali, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Yahaya alipendekeza kubadilishwa kwa jina la wizara, akieleza jina la mambo ya nje haliakisi vizuri majukumu ya wizara husika.

“Pia tunashauri kuwa na umadhubuti wa uongozi wa mambo ya nje ili viongozi waweze kutumikia kwa muda wa kutosha kwa lengo la kutunza kumbukumbu na misimamo ya nchi na kushughulikia masuala ya kimataifa yanayohitaji ufuatiliaji,” amesema balozi Yahaya.

Pia, kamati ilipendekeza kuundwa kwa idara ya uchambuzi wa kimataifa na kupendekeza jukumu la uchambuzi wa taarifa hizo, habari na matukio mbalimbali liondolewe kutoka idara ya Sera na mipango na iundwe idara mpya.

Credit: mwananchi
Hiyo wizara inazalisha.nini
 
Utumishi wa umma umekuwa rahisi kiasi hicho? Hasa kwenye hizo kazi nyeti?

Yap, kwanini? Maana ufuatiliaji ni mdogo, monitoring ni kama hakuna, na pia hawana pressure ya kudeliver service za viwango.
Kwenye private sector monitoring ni ya hali ya juu maana wanajua wakilega mapato yanapungua.
Serikalini wakilega nn kinapungua kama everymonth mshahara upow with less monitoring?
 
Back
Top Bottom