FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Siamini kwenye "bahati nzuri na mbaya.January ana bahati mbaya!
Bado ile chemba!
Falsafa ya "failures" hiyo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siamini kwenye "bahati nzuri na mbaya.January ana bahati mbaya!
Bado ile chemba!
Asiye na macho haambiwi tazama, asiye na masikio haambi sikia.Vijana kama wapi wenye spidi kali wamepelekwa huko??
Watu huwa hawakisii.January hana speed yoyote best labda ya upigaji tu. Hakuna wizara yoyote kaacha alama positive labda ile ya kuzuia mifuko ya plastic tu
Hapana kiebraniaSijakuelewa kabisa hapo.
Wewewa kutokea wapi, unaeandika lugha yako ya taifa namna hiyo? Au umeandika kireno?
Mama anza na ripoti ya CAG. Tekeleza maoni yake kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale waporaji walio katika balozi zetu. OVERRais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa ataifumua na kuisuka upya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ili kuirudishia hadhi baada ya kuwa na utendaji usioridhisha kwa muda mrefu.
Hatua hiyo imekuja kutokana na wizara hiyo kupoteza ushawishi kwenye medani za kidemokrasia, huku mashirika ya kimataifa yakilalamika kutoridhishwa na utendaji wa wizara hiyo nyeti.
Rais Samia amesema hayo jana, wakati akipokea ripoti ya kamati ya kutathmini ufanisi na utendaji wa wizara hiyo, kazi iliyofanyika kwa miezi sita chini ya uenyekiti wa Balozi Hassan Simba Yahaya.
Amesema muundo wa wizara hiyo unaenda kuangaliwa upya, ikiwemo namna ya kuwapata watumishi wenye sifa stahiki, kwa kuwa wengi waliopo hawana uwezo.
Amesema kwa muda mrefu wizara imekuwa ikitawaliwa na urasimu katika kuajiri, hali iliyosababisha watu wasio na sifa kuajiriwa kwa maelekezo ya vigogo ndani ya wizara.
“Ripoti imeeleza hapo katikati ajira hazikuwa katika mpangilio mzuri, zilikuwa chache na zilitolewa kwa kujuana. Sasa mengine nayafahamu mie hata kwenye ripoti hayajawekwa, pia kuna makundi, hamisha hamisha na panga pangua ya maofisa waandamizi haya yote yalichangia utendaji wa wizara kupwaya.
“Hili ni moja ya masuala yanayonisukuma kutaka kamati hii uindwe na kuifanyia tathmini wizara, ubobezi ule wa miaka ya 90 na 2000 sasa wizarani hakuna, unguli, umahiri na ushawishi wetu kwenye medani za kidemokrasia umekuwa wa kujikongoja.
Kumekuwa na malalamiko kutoka taasisi za kimataifa zilizopo nchini kuhusu utendaji usioridhisha wa wizara hii,” amesema Rais Samia.
Pia aligusia uwakilishi wa nchi kupitia balozi zake katika mataifa mbalimbali akitaka mpangilio huo kuangaliwa upya kulingana na hali ya sasa.
“Tunapaswa kuangalia upya suala la uwakilishi wetu kupitia balozi tulizonazo nje ya nchi na hadhi zake kutokana na mabadiliko yaliyopo duniani. Wakati ule tulikuwa tunaanzisha balozi kwa kuangalia wanaotusaidia pesa nyingi, lakini mambo yamebadilika, lazima tuangalie wapi tuwe na balozi za kupewa nguvu,” amesema.
Sambamba na uwakilishi wa nchi, alizungumzia pia namna teuzi za mabalozi zinavyofanyika, huku akitaka jukumu hilo sasa wapewe watu wanaostahili na sio kwa kuoneana haya.
“Tunavyofanya sasa wizara inaleta mapendekezo, yanavyoletwa na mie nina yangu mkononi naletewa nani kaharibu wapi anaweza kupelekwa. Sasa hujui mapendekezo yapi ya kisiasa, yapi ya kitaaluma.
“Sasa hivi tufumbe macho anayevurunda kazini akae pembeni, hakuna haja ya kumpoza kumpeleka kwenye ubalozi, lakini pia nafasi za kisiasa hatusemi zisiwepo, lakini tuangalie kwa asilimia gani. Ila changamoto wakati mwingine hao wenye taaluma hawapo pale wizarani kwa sababu ya undugu uliojaa,” amesema.
Kufuatia hilo, kiongozi huyo mkuu wa nchi alielekeza kuwepo vigezo vya kuajiri watumishi katika wizara hiyo na kuondokana na mfumo uliopo sasa ambao unaruhusu watu wasio na sifa kubebwa.
“Hapa mkono wa Rais unakwenda kuingia kwenye hii wizara, tutaanzisha mfumo maalumu wa ufadhili wa kutengeneza vijana ambao watakwenda kufanya kazi pale.
“Haitakuwa rahisi, ni lazima wawe vijana wenye sifa, watafanya mitihani, wakifaulu ndiyo watawekwa kwenye fellowship hii kwa miaka miwili wakipikwa kisha tuwapeleke wakafanye kazi,” amesema Rais Samia.
Awali, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Yahaya alipendekeza kubadilishwa kwa jina la wizara, akieleza jina la mambo ya nje haliakisi vizuri majukumu ya wizara husika.
“Pia tunashauri kuwa na umadhubuti wa uongozi wa mambo ya nje ili viongozi waweze kutumikia kwa muda wa kutosha kwa lengo la kutunza kumbukumbu na misimamo ya nchi na kushughulikia masuala ya kimataifa yanayohitaji ufuatiliaji,” amesema balozi Yahaya.
Pia, kamati ilipendekeza kuundwa kwa idara ya uchambuzi wa kimataifa na kupendekeza jukumu la uchambuzi wa taarifa hizo, habari na matukio mbalimbali liondolewe kutoka idara ya Sera na mipango na iundwe idara mpya.
Credit: Mwananchi
Duh....!. Sasa leo ndio nimeelewa!. Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza, imekuwaje mtu mwenye level ya DGIS, anateuliwa ubalozi na kupostiwa nchi ya hovyo tuu?!. Sasa nimeanza kupata majibu!.“Sasa hivi tufumbe macho anayevurunda kazini akae pembeni, hakuna haja ya kumpoza kumpeleka kwenye ubalozi.
wewe nanjilinji huwezi kuiandika,itajua vijana wenye spidi?[emoji23][emoji1787][emoji1485][emoji22] Vijana wenye spidi kali unawaelewa vizuri binti yangu?.
Wewe unaelewa nini maana ya ujana maji ya moto?.
Kijana aliyechelewa na mwenye njaa, katoka huko nanjirinchi mwambeo unampa kwa speed kali unategemea nini?.
Hivi pasipo kuwa na maamuzi ya kumfundisha huyo kijana wako mwenye speed 120kph unadhani atafika salama?.
Umemuona mdogo wako alipokuwa pale wizarani alichofanya?, Tena ndiyo mmoja wa hao vijana wenye speed kali.
Naendelea kujifunza tabia ya binadamu!.
una ushahidi wa walivyoiba tanesco?wenye speed kali ya kuiba kama walivyoiba kule TANESCO
Kampe wwSamia apewe awamu saba za uongozi, big up madam presidenti
Hiyo ya kuzui mifuko ilibebwa na aina ya serikali iliyopo huyo januro haina influence yoyoteJanuary hana speed yoyote best labda ya upigaji tu. Hakuna wizara yoyote kaacha alama positive labda ile ya kuzuia mifuko ya plastic tu
Agreed with youmifuko ya plastik siyo yeye aliyezuia na wala hakuwa na uwezo huo ilikuwa ni mpango wa serikali 2015/20 hivyo yoyote ambaye angekuwa hiyo wizara angezuia pia hata kama angekuwa nape …
Hivi report ya CAG ya mwaka huu ipo wapi jamani ,au wameamua kumpiga spana CAG kupitia mwigulu na NepiMama anza na ripoti ya CAG. Tekeleza maoni yake kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale waporaji walio katika balozi zetu. OVER
It's too late ,kama imemchukua miaka 3 ndo anagundua hilo vipi mambo mengineDuh....!. Sasa leo ndio nimeelewa!. Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza, imekuwaje mtu mwenye level ya DGIS, anateuliwa ubalozi na kupostiwa nchi ya hovyo tuu?!. Sasa nimeanza kupata majibu!.
Tuliwahi kushauri Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
Kisha tukashauri tena, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?
Sasa ushauri huu umepata sikio la kuusikia, sasa unakwenda kufanyiwa kazi, kiongozi anayevurunda mahali, hata awe nani, hakuna tena kupoozwa kwa kupewa ubalozi!, atupishe kazi iendelee!.
Ila Mama nae...!, ameanza kuwa mkweli wa type ya JPM, hakopeshi!. Kumbe kuna watu huwa wanavurunda, ila kwa vile post zao ni nyeti sana!, wanaondolewa hapo walipovurunda na kupoozwa kwa kutupwa ubalozini!.
Naunga mkono hoja, wanaovurunda, wasipoozwe na ubalozi, watupishe!.
P
Better late than never, chelewa ufike.It's too late ,kama imemchukua miaka 3 ndo anagundua hilo vipi mambo mengine
Hama nchi pumbavu wwKampe ww
Arusha - Kaloleni.wewe nanjilinji huwezi kuiandika,itajua vijana wenye spidi?