PostGE2025 Rais Samia: Nitaunda Tume ya Maridhiano na Upatanishi ‘baada ya kujua kiini cha vurugu’

PostGE2025 Rais Samia: Nitaunda Tume ya Maridhiano na Upatanishi ‘baada ya kujua kiini cha vurugu’

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais Samia amesema ataunda tume ya maridhiano na upatanishi na kuanza mchakato wa mabadiliko ya Katiba baada ya kujua kiini cha vurugu kwenye uchaguzi mkuu.

 
Rais Samia akizungumza katika hotuba ya kufungua Bunge la 13, amesema kusikitishwa na kilichotokea wakati wa uchaguzi, hivyo serikali imechukua hatua ya kuunda tume ya kuchunguza yaliyotokea ili kujua kiini cha tatizo ili kupata taarifa itakayowaongoza kujielekeza kwenye mazungumzo ya kuleta amani na maelewano.

 
Too late.

Kuingia kwenye Maridhiano bila wakati watekaji wanaendelea kutamba mtaani, wauaji wanatamba, miili mnaishikilia ni kudhihaki damu za watu zilizopotea.

Busara ni Kuwajibika.
 
I might be mistaken lakini ukiniuliza kwa haraka haraka chanzo kwa neno moja nadhani nitasema Wewe..., yaani It's you Madam President - ndio maana wenzako wote waliopita hatujawahi kufika hapa angalau waliweza kusoma alama za nyakati.
 
20251114_070405.jpg
Hakuna maridhiaano na muuaji.
20251108_042937.jpg
 
Kiini cha vurugu kinajulikana,
Kukithiri kwa utekaji, kupotezwa, kutekwa na mauaji ya wapinzania na wakosoaji wa CCM, uchaguzi wa kiini macho na utawala mbovu kwa ujumla ukichangiwa na katiba mbovu, kunyamazishwa kwa vyombo vya habari, ufisadi na kutowajibika.
 
Eeeh, kumbe kiini cha vurugu hakikajulikana?

Asa itakuwaje?

Kiini ni Wakenya 😀😀😁
 
Back
Top Bottom