Rais Samia: Pwani wanakata sana miti na kusababisha uhaba wa maji

Rais Samia: Pwani wanakata sana miti na kusababisha uhaba wa maji

kwahiyo nikapanda mti nyumbani kwangu ,mvua itanyesha maeneo ya nyumbani kwangu tu, kwa jirani yangu ambaye hana mti haitanyesha? I'm no metereologist but this explanation...sigh!
 
Matumizi ya mkaa yalishaanza kupungua kwa wakazi wa mjini wakati gesi iliposhuka bei.........badala yake wakaja kupandisha tena bei ya gesi kutokana na matozo tozo yao wanayoweka watu wakarudi tena kwenye mkaa, hawa watu sijui kama wana uelewa wa haya mambo au wao wanajali tozo tu.​
Tatizo la serikali wakishaona kitu kina watumiaji wengi tu hapohapo wanaongeza tozo au kodi

Jamaa ubunifu hawana kwenye suala la kukusanya mapato
 
Shida ya Maji Tanzania inasababishwa na Utendaji Mbovu wa Kupindukia....

Mwanza kuna Ziwa Victoria ila watu wanakosa maji..., Impact ya ukataji miti sio kwamba haipo, ila hio inakuja na ikifika tutakuwa tunaongea mengine...
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Gesi ishushwe bei mkaa upigwe marufuku viongozi muwe wakali waziri anayehusika na mazingira ana kazi gani?
 
Sasa huyu mama analalamika au anatupa taarifa?
Poorest president ever
 
26 October 2022

Bwawa la Julius Nyerere / Stiegler's Gorge hatarini kukosa asilimia kubwa ya maji yanayotoka Nyanda za Juu Kusini

BY VERONICA KOMBA ON OCTOBER 26, 2022 HABARI



VIJIJI 5 NA VITONGOJI 41 KUONDOLEWA ENEO LA HIFADHI USANGU​


1-1-1.jpg
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisaidiwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (Kulia) kuteremka kutoka kuangalia ukingo wa kuzuia maji katika kijiji cha Mwanavala eneo la Mnazi Mbarari mkoani Mbeya leo.
3-1.jpg
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiangalia sehemu ya eneo lenye uharibifu wa mazingira na vanzo vya maji katika kijiji cha Mwanaval eneo la Mnazi Mbarali Mbeya.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Serikali imeamuru vijiji vitano na vitongoji 41 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha magwalisi kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilaya ya mbarali kuhamishwa ili kupisha hifadhi.


Pia vitongoji 3 katika kijiji cha Lualaje wilayani Chunya navyo vinatakiwa kuondoka kupisha hifadhi.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 25, 2022 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula katika mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo la Ubaruku Mbarali wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta walipofanya ziara kwenye eneo la mto ruaha na mnazi katika kijiji cha Mwanavala ambapo eneo lote liko katika hifadhi.

Uamuzi huo wa serikali unalenga kutunza na kulinda ardhi oevu pamoja na vyanzo vya kupokea na kutunza maji yanayotiririka kutoka mito mbalimbali.
Alivitaja vijiji vitakavyoondoka kwa asilimia mia moja kuwa ni Luhanga, Madundasi, Msanga, Iyala na kalambo vyenye idadi ya watu 21,252 na kusisitiza watu wa maeneo hayo wanatakiwa wasiwepo na usajili wa vijiji hivyo kufutwa.

‘’Katika zoezi hili wenye kulipwa fidia watalipwa na wale wasiostahili wataondoka kama walivyokuja na lengo la serikali ni kuwa na urithi wa watu wote’’ alisema Dkt Mabula.

Adha, Dkt Mabula alisema serikali imeridhia vijiji 15 vyenye ukubwa wa hekta 74, 324.12 na ranchi ya Usangu ya NARCO kuendelea kubaki huku vijiji vyote vinavyopakana na hifadhi ya Ruaha kufanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi.

Katika mapendekezo yake timu ya wataalamu ilipendekeza eneo la ranchi ya usangu linalopendekezwa kuondolewa ndani ya hifadhi litumiwe na wafugaji watakaohamishwa kutoka kwenye vijiji na vitongoji vinavyopisha hifadhi.

Aidha, Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya za Mbarali na Chunya pamoja na wadau wengine waandae mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji vyote vinavyopatikana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Pia Ofisi Tamisemi iwe inashirikiana wadau wote muhimu katika suala la usajili wa vijiji na vitongoji ili kuepusha migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza miongoni mwa wadau ni wizara ya ardhi, wizara ya maji, maliasili na utalii, ofisi ya makamu wa rais mazingira.

Uhifadhi wa Bonde la Usangu ulianza mwaka 1953 wakati eneo likijulikana kama pori tengefu la utengule likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 500 kwa lengo la kuhifadhi bioanuwai katika ardhi oevu ya ihefu.

Kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira na vyanzo vya maji uliofanyika miaka ya 1990 serikali iliamua kupandisha hadhi pori tengefu la Utengule na kuwa Pori la Akiba la Usangu likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 4148 kwa tangazo la serikali namba 436A la tarehe 24 julai 1998.

Hata hivyo, uharibifu ulisababisha serikali kuja na mkakati wa kitaifa wa hifadhi ya mazingira ya ardhi oevu na vyanzo vya maji mwaka 2006 na kutaka bonde la usangu kuwa kati ya maeneo ambayo wafugaji waliovamia mabonde na maeneo ya vyanzo vya maji waondolewe.

Bonde la Usangu ni ardhi oevu ya Usangu ni kitovu cha kupokea na kutunza maji yanayotiririka kutoka mito mbalimbali ikiwemo mto Mkoji , Chimala, Kimani, Mbarari , Ndembera na Mzombe inayoanzia katika wilaya ya Wanging’ombe , Makete, Mufindi, Mbeya vijijini na Chunya na kuchangia maji kwenye mto Ruaha. Pia ni makazi ya bioanuwai mbalimbali ikiwemo wanyamapori, ndege wakubwa kwa wadogo aina zaidi ya 300 , samaki na mimea ya aina mbalimbali.
 
Bei ya gesi iwe karibu na bure iondolewe tozo na kodi, makali yahamie kwenye mkaa. Sheria ndogo za halmashauri zitungwe kila mmoja awe na miti 100 tu tutakwenda. Vyanzo vya maji serikali iweke sheria kali kwa wanaovivuruga na pia maeneo ya mifugo malisho yatengwe. Luhaga Mpina maeneo kama yanamfaa sana yanahitaji elimu na ubabe pia.Hili ni janga linahitaji state of emergency
 
Serikali isipochukua hatua kali za dharura katika mazingira miaka ijayo tutaishi wote jangwani.
Ni Nchi nzima Mapori yanakatwa kwa kiwango ambacho hayawezi kurecover.
 
Serikali isipochukua hatua kali za dharura katika mazingira miaka ijayo tutaishi wote jangwani.
Mkuu mimi sughuli zangu hunipeleka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara ninashuhudia maagamizi ya mazingira mpaka naogopa.
 
Afande Sele anahoja za mazingira kushinda washauri wa raisi.

They do know ya kuwa chanzo cha maji ya mto Ruvu ni Uluguru mountains, sio hizo porojo zao za kukata miti maeneo wanapotaka kulaumu watu wengine.

Wananchi huko Morogoro kila siku wanalalamikia Wamasai kutumia njia nzima kunyweshea n’gombe zao huko morogoro; halafu wewe ulaumu watu wa pwani na kutuletea hadithi za mvua.


Besides unaweza pata historical data ya hali hewa Tanzania ya kila mkoa kwa miaka karibu mia. Na annual rain average ni almost the same for the last decade; so shida ni incompetence serikalini nothing else.
 
Rais Samia amesema shida ya maji inayoendelea katika Mkoa wa Dar es salaam imesababisha na athari za kimazingira ikiwemo kukata miti.

Amesema mkoa wa Pwani unaongoza kwa kukata miti iliyoko kando ya mto Ruvu unaoleta maji Mikoa ya Dar es Salaam na hivyo wanasababisha uhaba wa maji.

Rais ameyasema hayo katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la nishati safi ya kupikia
Rais analamika badala ya kutoa solution.
 
10 May 2021
Bungeni, Dodoma
Tanzania

MAAMUZI YA BARAZA LA MAWAZIRI YAWEKWA WAZI, WANANCHI WASIONDOLEWE KTK HIFADHI TENGEFU



Mgogoro wa Ardhi Vijiji 29 Mbarali vyamuibua Lukuvi Bungeni, Magufuli atajwa au ahusishwa, kamati shirikishi ya mawaziri 8 pia wabunge na wananchi walishirikishwa, matokeo ya ziara ya mawaziri 8 yaliwakilishwa baraza la mawaziri uamuzi ulikuwa ...... kamati ya bunge ya maliasili na ardhi ....
 
Back
Top Bottom