Rais Samia, Rais wa matajiri(?)

Katiba mpya na serikali ya kanda haviepukiki, kwa hili namtetea li nchi likubwa sana hili, na ukizingatia amezungukwa na watu wa kumdanganya kila siku hawezi toboa
 
Katiba mpya na serikali ya kanda haviepukiki, kwa hili namtetea li nchi likubwa sana hili, na ukizingatia amezungukwa na watu wa kumdanganya kila siku hawezi toboa
Nchi kubwa wakati kuna Ndege ya Rais,hapo Mtwara ni masaa mangapi kwa Ndege ?
 
Kama huwezi changia kampeni 2025 wewe sio rafiki na mama muuza.
 
Imagine unanunua magoli ,kuna shule hata madawati hazina.

Shule ambayo haina madawati hiyo kata ifutwe na wakazi wake wote wahamishiwe kata zingine wakajifunze kujitegemea siyo kuwa tegemezi tu.

Na hiyo shule ifanywe mabanda ya kuku chini ya BBT.

Yaani Mtanzania wa leo hii unakuja kulilia madawati mtandaoni? Wakati shule zingine wananchi wamewafungia mpaka viyoyozi ofisi za walimu. Wamejijengea mpaka maabara za kisasa wanafunzi wasome sayansi kwa vitendo, hawajangoja serikali.

Nyie mnaolilia ma desk mwaka huu mtakuwa wa kwanza kwa ujinga duniani.
 
Q
Mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa
 
Rais Samia hana mitazamo ya kimaskini ile ya kijamaa ya kutaka kumuumiza mtu mmoja ili mwingine apate furaha.

Na hilo ni kosa lake kwa mujibu wa mleta mada. Anapotoa milioni tano kwa kila goli ni kuhamasisha timu zetu zipate matokeo mazuri kimataifa ambayo yataongeza heshima ya Tanzania kimataifa.

Tuna mpango wa kuandaa michuano ya AFCON 2026 ni mikubwa kuliko yote afrika, ni suala la maana sana kuamsha hamasa katika mchezo ambao miaka mitatu ijayo tutakuwa mwenyeji na kukaribisha afrika nzima.

Milioni 100 ya gari alilompa Mzee Mwinyi halina thamani kuliko namna alivyojitoa kwenye siasa za nchi hii tangu miaka ya hamsini. Haina thamani kuliko uungwana wake mpaka akakubali kujiuzulu uwaziri kwa ushenzi wa watu wa chini yake.

Samia ana maono makubwa, anataka Tanzania iwe hub ya kiuchumi ya ukanda huu wa afrika, sina uhakika kama wengi wetu tunaoandika humu jukwaani tunaelewa maana ya nchi kuwa ni hub ya kibiashara.
 
Wewe kama kata yenu bado mnashida ya madeski ni heri mjinyonge tu.

Hata mkitoza.kodi kwenye vilabu vya Pombe ya mia mia tu kiingilio, ndani ya muda mchache mnapata ma desk.

Upo kata ipi, wilaya ipi, mkoa upi ambako hakuna madesk?
Kizimkazi Zenj
 
Umeandika pumba tupu
 
Ukiachana na DP wedi Samia hana Baya mama wa watu.

Kuhusu katiba ni kweli tunahitaji elimu, viongozi washatuona mazwazwa as for years Katiba iliyopo imekuwa ikivunjwa hadharani na wananchi hakuna reaction yoyote tuliyoichukua.....Sasa Kama hii iliyopo hatuisimamii hiyo mpya ndo itajisimamia yenyewe?

Hana Baya Samia, maisha yangu kabla na baada yake yana tofauti kubwa....Huyu ndiye Rais wa wanyonge hasa.
 
Labda wanataka kuuona msafara wake ukiwa unasimamasimama njiani ndio awe katimiza sifa ya kuwatetea wanyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…