Rais Samia ruhusu bidhaa za ujenzi toka nje, unatuua wananchi

Rais Samia ruhusu bidhaa za ujenzi toka nje, unatuua wananchi

Mishenyi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2019
Posts
464
Reaction score
748
Mh. Rais ongea na wafanyabiashara wa ndani washushe bei ya bidhaa za ujenzi hasa bati kama wataleta visingizio "nonesense" Ruhusu bidhaa hizi zitoke nje kwa wingi ili tupate unafuu wa bei wananchi wako.

Kwanini Serikali yako inataka kishindwa kila kitu mama. Hivi hilo baraza linakusaidia nini? Kama limeshindwa kukusaidia achana nalo libaki kama mwanasesele tu. Ikikupendeza tafuta hata wazungu huko nje wakushauri mambo nyeti hasa yahusuyo Fedha na biashara kwa ujumla.

Serikali yako imekwama mama yangu. Kagame anawatumia wazungu kwenye mambo magumu ambayo mwafrika wa kawaida aliyekulia Kanyenye akasoma chuo kikuu Dar es Salaam, Saut nk hawezi kuyatatua zaidi ya kukariri upumbavu kichwani.

Ruhusu uingizwaji wa bidhaa hizo tajwa bila kujali kelele za kuua viwanda vya ndani ambavyo vimeshindwa kumsaidia Mtanzania

Wananchi wakijenga nyumba bora ni sifa kwako mama.
 
Angekuwa na yeye anakutana na ugumu wa maisha kama tulio nao sisi mambo yangekuwa mazuri sn, sasa hivi yeye ni kuagiza tu, ifike sehemu watawala wasihudumiwe na serikali wahudumiwe na mishahara yao kama wafanyakazi wengine nao wasikie machungu kama sisi.
 
Angekuwa na yeye anakutana na ugumu wa maisha kama tulio nao sisi mambo yangekuwa mazuri sn, sasahivi yeye ni kuagiza tu, ifike sehemu watawala wasihudumiwe na serikali wahudumiwe na mishahara yao kama wafanyakazi wengine nao wasikie machungu kama sisi.
Sikubaliani na wazo la viongozi wa serikali kujihudumia. Hii itaondoa resiponsibilitu na accountability kwao, ingawa bado kuna baadhi hata wakihudumiwa wanaendelea kuwa irresponsible and unaccountable!!!
 
ni kwa namna gani waziri wa fedha anaweza kudhibiti mfumuko wa bei.?

Tafadhali Mkuu toa maelezo ya kina wakati ukijibu swali hili.
Waziri wa fedha ndiyo ana control uchumi wetu, anaweza kudhibiti kwa kuondoa kodi ambazo hazina msingi haswa kwenye nishati, kupunguza matumizi yasiyo yalazima, kupeleka mswaada bungeni watawala wote mishahara yao ipunguzwe, magari ya kifahari yaondolewe yabaki kwa Rais, Makamu, PM, Spika na Jaji mkuu wengine wote watumie RAV 4, watawala wote wasihudumiwe na serikali wahudumiwe na mishahara yao n.k
 
Huwa ninashindwa kuelewa hii dhana ya kuzuia bidhaa kutoka nje kwa kulinda viwanda vya ndani wakati viwanda hivyo vinatoa bidhaa kwanza zenye ubora hafifu pili kwa bei juu na kuwaumiza wananchi au ndio kwa kuwa viwanda hivyo ni vya wakubwa na makada wa chama na serikali wananufaika navyo!?
 
True vifaa toka nje viingie,bati Kenya bei chini Sana,hapa reject mbovu ni elf 16 mpya elf 35.
 
Huwa ninashindwa kuelewa hii dhana ya kuzuia bidhaa kutoka nje kwa kulinda viwanda vya ndani wakati viwanda hivyo vinatoa bidhaa kwanza zenye ubora hafifu pili kwa bei juu na kuwaumiza wananchi au ndio kwa kuwa viwanda hivyo ni vya wakubwa na makada wa chama na serikali wananufaika navyo!?
Nadhani ni viwanda vyao haiwezekani wananchi wanaumia eti kisa kulinda viwanda vya Ndani ambavyo ndio vinachochea mfumuko mkubwa na wananchi wanabaki utadhani hawana serikali
 
Back
Top Bottom