Rais Samia ruhusu bidhaa za ujenzi toka nje, unatuua wananchi

Rais Samia ruhusu bidhaa za ujenzi toka nje, unatuua wananchi

Mh. Rais ongea na wafanyabiashara wa ndani washushe bei ya bidhaa za ujenzi hasa bati kama wataleta visingizio "nonesense" Ruhusu bidhaa hizi zitoke nje kwa wingi ili tupate unafuu wa bei wananchi wako.

Kwanini Serikali yako inataka kishindwa kila kitu mama. Hivi hilo baraza linakusaidia nini? Kama limeshindwa kukusaidia achana nalo libaki kama mwanasesele tu. Ikikupendeza tafuta hata wazungu huko nje wakushauri mambo nyeti hasa yahusuyo Fedha na biashara kwa ujumla.

Serikali yako imekwama mama yangu. Kagame anawatumia wazungu kwenye mambo magumu ambayo mwafrika wa kawaida aliyekulia Kanyenye akasoma chuo kikuu Dar es Salaam, Saut nk hawezi kuyatatua zaidi ya kukariri upumbavu kichwani.

Ruhusu uingizwaji wa bidhaa hizo tajwa bila kujali kelele za kuua viwanda vya ndani ambavyo vimeshindwa kumsaidia Mtanzania

Wananchi wakijenga nyumba bora ni sifa kwako mama.
Kujenga nyumba Tanzania ni anasa
 
Bati inayouzwa tz Sh 30,000/ kenya inauzwa sh 17,000 kwa Tsh. Sasa kenya wao wako ulimwengu gani ambao haujakumbwa na Covid???
Gharama za uzalishaji zinachangia, uncertainty kwenye production..leo mnaambiwa hivi kesho vile, nishati ya umeme iaiyoeleweka, kubambikiwa returns na kaisari...mkuu sababu ni nyingi.
 
Nyinyi ndo wale wasomi naowasemea mnaomshauri rais ujinga,,,ruhusuni bidhaa zimiminike kwa wingi toka nje alafu wafanyabiashara washindane mwenye bei nzuri ndio auze
Miaka mitano kurudi hivi tumeona faida ya Protectionism ya Viwanda vya ndani.

Bei ya Maziwa kwa mfugaji wa kawaida iliongezeka kutoka Tsh 600 mpk 1200 na hata zaidi.

Nyama ya Ngombe inaongezeka bei kila uchwao.

Unless mtu hutizami na kufanya tathmini...

Muhimu hapa ni kufanya DIPLOMATIC PROTECTIONISM...

TACTICAL....

STRATEGICAL...

FORE CASTED...

BY the way,Hakuna mtu amekatazwa kuingiza Cement...

Nenda Kalete.

Bei ya 12000 iliyozungumzwa ni kwa wananchi wa Kenya.

Ikivuka impaka itauzwa kwa 20+

Unless upite kimagendo..

Hakuna Bidhaa inayokatazwa kuingia nchini...

Kwa hivo huo siyo mjadala.

Mjadala ni Mazingira gani Rafiki ktk uwejezaji ktk VIWANDA.

HUO UNA TIJA...
 
Hata tiles za mkuranga hapo zina bei kishenzi
 
Mh. Rais ongea na wafanyabiashara wa ndani washushe bei ya bidhaa za ujenzi hasa bati kama wataleta visingizio "nonesense" Ruhusu bidhaa hizi zitoke nje kwa wingi ili tupate unafuu wa bei wananchi wako.

Kwanini Serikali yako inataka kishindwa kila kitu mama. Hivi hilo baraza linakusaidia nini? Kama limeshindwa kukusaidia achana nalo libaki kama mwanasesele tu. Ikikupendeza tafuta hata wazungu huko nje wakushauri mambo nyeti hasa yahusuyo Fedha na biashara kwa ujumla.

Serikali yako imekwama mama yangu. Kagame anawatumia wazungu kwenye mambo magumu ambayo mwafrika wa kawaida aliyekulia Kanyenye akasoma chuo kikuu Dar es Salaam, Saut nk hawezi kuyatatua zaidi ya kukariri upumbavu kichwani.

Ruhusu uingizwaji wa bidhaa hizo tajwa bila kujali kelele za kuua viwanda vya ndani ambavyo vimeshindwa kumsaidia Mtanzania

Wananchi wakijenga nyumba bora ni sifa kwako mama.
Nakuunga mkono kwa nguvu zote, hatuwezi kulinda wafanyabiashara wa ndani kwa gharama ya maisha ya Wananchi.
 
Tanzania ingekuwa na sera ya kulinda viwanda endapo vile viwanda na mashirika ya umma yaliyokuwa chini ya uendeshaji wa umma vingekuwepo na vingekuwa vinafanya vizuri. Baada ya zoezi la ubinafasishaji na serikali kujiondoa kwenye maswala ya uzalishaji wa bidhaa na biashara wawekezaji binafsi wanatakiwa kuwekeza kiushindani na wawekezaji wengine duniani pasipo kutegemea mbeleko ya serikali. Ni upuuzi serikali kuumiza wananchi ili kumlinda mwekezaji ambaye anatakiwa kuwa na strategy za kiuwekezaji aweze kushindana kwenye soko huria hasa kwenye swala la kupanga bei shindani (price war).​
Asante mkuu,umenena vzr lkn serikali hii inawaacha wawekezaji wanadeka tu huku wakimwacha mwananchi hana la kufanya
 
Gharama za uzalishaji zinachangia, uncertainty kwenye production..leo mnaambiwa hivi kesho vile, nishati ya umeme iaiyoeleweka, kubambikiwa returns na kaisari...mkuu sababu ni nyingi.
Ili kusaidia wananchi serikali iache bidhaa za nje zije kwa wingi ili bei iji regulate yenyewe
 
Zambia na Zimbabwe kuna vita? Kwani Tzn hujui kwamba mwaka huu kuna Hali ya ukame?
Nadhani hukumbuki Zimbabwe wamepigwa na ukame juzi hapa tukawapa na msaada wa mahindi,,,Zambia wanasumbuliwa na Mgogoro wa madeni yasiyolipika
 
Nadhani hukumbuki Zimbabwe wamepigwa na ukame juzi hapa tukawapa na msaada wa mahindi,,,Zambia wanasumbuliwa na Mgogoro wa madeni yasiyolipika
Kwani Tzn hakuna hayo madeni? Mvua umeona zipo kama miaka ya kawaida?

Haya hapa kama sio madeni ni kitu gani?👇

Screenshot_20211113-134557.png
 
SAMIA msikivu atalifanyia kazi
Nategemea hivyo, lakini mpaka sasa kaweka pamba masikioni kuhusu suala la ulipukaji wa bei ya bidhaa. Yaani Mama hajalitaja hilo hata kwenye hutuba yake hata moja. Ni kama tatizo halipo vile. Na mbaya zaidi hatujui sababu ni nini, bora angetueleza hilo tu.
 
Ila Maza anazingua sana, inakuwaje yupo kama hayupo?!
hadi tunamkumbuka dikteta bhn!
 
Back
Top Bottom