Sasa hivi hata serikali ikiruhusu bidhaa, hasa za Ujenzi kutoka nje bado bei itakuwa juu kwa sababu ulizozisema hapo juu, raw materials nyingi zinatoka China, Malaysia na huko Singapore. COVID effect imekuwa kubwa sana kwa wenzetu, kazi hazifanyiki kwa 100% hivyo uzalishaji umepungua, usafirishaji wa bidhaa unachelewa sana. Raw materials za iron zinachelewa hivyo viwanda vinakosa materials, end of the day bidhaa zitapanda bei tu.
Nimetoa mfano wa nondo za nje na ndani, tani ya nje 12mm ni 2.55mil, na za ndani ni 2.35mil. Kumbuka hizi nondo zilikuwa zinauzwa 1.65mil hadi 1.75 last year.