Rais Samia ruhusu bidhaa za ujenzi toka nje, unatuua wananchi

Mwigulu hana msaada kwa huyu maza!!
 
Sasa hivi hata serikali ikiruhusu bidhaa, hasa za Ujenzi kutoka nje bado bei itakuwa juu kwa sababu ulizozisema hapo juu, raw materials nyingi zinatoka China, Malaysia na huko Singapore. COVID effect imekuwa kubwa sana kwa wenzetu, kazi hazifanyiki kwa 100% hivyo uzalishaji umepungua, usafirishaji wa bidhaa unachelewa sana. Raw materials za iron zinachelewa hivyo viwanda vinakosa materials, end of the day bidhaa zitapanda bei tu.

Nimetoa mfano wa nondo za nje na ndani, tani ya nje 12mm ni 2.55mil, na za ndani ni 2.35mil. Kumbuka hizi nondo zilikuwa zinauzwa 1.65mil hadi 1.75 last year.
 
Ujuaji mwingi wakat ata kiwanda cha kibeliti hatuna
Ebu tuache ujuaji na kujifanya tunajua sana kushauri na kuongea wakat ni Zero
Watanzania weng ni watu wa hovyo sana tunajifanya tunajua sana kuoji af ikifika wakat wa kufanya maamuzi tunakua mapimbi
 
Kwa ugumu ninaokutana nao kufanya finishing ya nyumba, nawasikitikia watumishi ambao ndo wana plan kuanza ujenzi.....kama baadhi ya wachangiaji walivyosema hawa viongozi kwa sababu wanahudumiwa kwa kila kitu hawawezi kuhisi hali yoyote ngumu ya kimaisha, huyo waziri ambaye anatakiwa kudhibiti uchumu nasikia ni mfanyabiashara wa mabasi.......kazi aliyobaki nayo ni kuhimiza tu kukusanywa tozo zaidi na blah blah za pesa kumwagwa mtaani, hovyo kabisa............
 
Jamaa wametengeneza gap kubwa sn kati yao na wananchi wa kawaida
 
Nyinyi ndo wale wasomi naowasemea mnaomshauri rais ujinga,,,ruhusuni bidhaa zimiminike kwa wingi toka nje alafu wafanyabiashara washindane mwenye bei nzuri ndio auze
 
Bati inayouzwa tz Sh 30,000/ kenya inauzwa sh 17,000 kwa Tsh. Sasa kenya wao wako ulimwengu gani ambao haujakumbwa na Covid???
 
Asante sana kwa ufafanuzi. Kama waziri wafedha anania njema na watanzania atautilia maanani ushauri wako. Nina uhakika post yako hii itamfikia kwa sababu wanapita wengi humu wanaokusanya maoni kwa ajili ya viongozi kuyafanyia kazi.
 
Nyinyi ndo wale wasomi naowasemea mnaomshauri rais ujinga,,,ruhusuni bidhaa zimiminike kwa wingi toka nje alafu wafanyabiashara washindane mwenye bei nzuri ndio auze​
Tanzania ingekuwa na sera ya kulinda viwanda endapo vile viwanda na mashirika ya umma yaliyokuwa chini ya uendeshaji wa umma vingekuwepo na vingekuwa vinafanya vizuri. Baada ya zoezi la ubinafasishaji na serikali kujiondoa kwenye maswala ya uzalishaji wa bidhaa na biashara wawekezaji binafsi wanatakiwa kuwekeza kiushindani na wawekezaji wengine duniani pasipo kutegemea mbeleko ya serikali. Ni upuuzi serikali kuumiza wananchi ili kumlinda mwekezaji ambaye anatakiwa kuwa na strategy za kiuwekezaji aweze kushindana kwenye soko huria hasa kwenye swala la kupanga bei shindani (price war).​
 
Shida iliyopo hao wafanyabiashara wenye viwanda ni wafadhili wakubwa wa CCM hivyo lazima walindwe kwa gharama zozote hata kama mtakula nyasi lakini wao wanawaza 2025
 
Bati inayouzwa tz Sh 30,000/ kenya inauzwa sh 17,000 kwa Tsh. Sasa kenya wao wako ulimwengu gani ambao haujakumbwa na Covid???
Si ndo hapo mkuu, mbona bidhaa nyingine madukani wameacha ushindani wa bei ufanye kazi. Nitakupa mfano, kuna air fryer ambayo nilinunua kama 190,000, lakini kuna air fryer ya aina na ukubwa uleule kutoka kampuni nyingine inauzwa 750,000........sasa haya mambo ndo tunayoshauri, waache ushindani wa bei ufanye kazi ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu kununua bidhaa muhimu.​
 
Yaani li nchi utadhani lipo vitani aisee hakuna kinachoshikika!!
 
Kila nikiona hilo jina apo kwenye headline najisikia vibaya na huruma kwa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…