Rais Samia: Sasa Dodoma umeme ni ware ware hakuna tena kukatika, Uhakika 24/7

Rais Samia: Sasa Dodoma umeme ni ware ware hakuna tena kukatika, Uhakika 24/7

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewahakikishia Watanzania kuimarika kwa huduma ya nishati ya umeme nchini kufuatia kukamilika kwa miradi mikubwa ya miundombinu na usambazaji wa umeme.

Akizungumza tarehe 22 Agosti 2026 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Uzalishaji wa Umeme cha Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa megawati 2,115 kilichopo Rufiji mkoani Pwani, amesema kuwa Serikali inaendelea na uwekezaji wa kuimarisha gridi ya taifa ili kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wote kwa tija.

Rais Samia amebainisha kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 345, pamoja na upanuzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Zuzu mkoani Dodoma, umekamilika na kuwashwa rasmi mnamo Agosti 20, 2026, hivyo kwa Dodoma hakutakuwa na shida ya kukatika kwa umeme



​
 
Bado maeneo mengi umeme ni shida, unakata mida fulani kila siku mfano jioni, kwingine umeme mdogo hadi kuwasha Friji ni shida, pia ile ahadi ya bei ya umeme kwa unit kupungua iliishia wapi?
 
Bado maeneo mengi umeme ni shida, unakata mida fulani kila siku mfano jioni, kwingine umeme mdogo hadi kuwasha Friji ni shida, pia ile ahadi ya bei ya umeme kwa unit kupungua iliishia wapi?

Naomba nikujibu kiungwana kama ifuatavyo:

1. Asilimia tisini (90%) ya kukatika katika umeme ni kazi ya mikono yetu. Na tunafanya hivyo ili tuweze kulisha familia zetu. Wewe unaweza kukataa Tsh 200k kwa saa?

Lakini pia tunatekeleza kwa vitendo kauli ya mama ya kula kwa urefu wa kamba zetu.

2. Kuhusu bei ya umeme kushuka kwa sababu bwawa limekamilika, hiyo nakushauri kwa uzuri tu uiondoe kwenye mawazo yako.

Tuna sababu nzuri za kufanya hivyo:

1. Bei ya sasa ya Tsh 292 kwa unit moja ni ndogo sana. Na kama unaona ni kubwa; basi tumia kibatari.

2. Mitambo ya kufua umeme hufanyiwa preventive maintenance kila baada ya miezi 6 kwa gharama kubwa.

3. Serikali haina uwezo wa kuipa Tanesco ruzuku ili washushe bei ya umeme. Si unajua baada ya 29/10 wafadhili wametukatia mirija yao?

4. Ukiona mambo hayaendi, hamia Burundi
 
Back
Top Bottom