Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Kwani yeye mwinyi hana hiyo hela ya kununua Benz? Au hajui km anatakiwa kununua Benz imrahisishie ufasiri? Mambo mengine yanakera sana.
 
Mkuu gharama ya Hilo Benz Ni kituo cha afya kimoja chenye kila kitu ndani anapewa mtu mmoja kweli ?
Kama ametoa mfukoni mwake mbona. Haina shida ila Kama amtoa KWA walipa kodi Kuna shida,sababu babu ni mstahafu na kodi za watanzania zinaendelea kumhudumia na Kama haitoshi katika dunia ni marais wachache waliowai stahafu wakaishi maisha ya kifukara but Afrika sidhani Kama yupo tofauti na mwalim nyerere, so KWA KUA mwalim hayupo ila mama nyenyere yupo Basi Kama ni KWA hisan ya wananchi Basi Mama nyerere nae apewe benz labda Kama mh katoa mfukoni mwake vinginevyo moto kuwaka lazima ,tunasema hakuna Alie zaidi ya mwenzake katika taifa hili japo ni madaraka tu kwamba Kuna Rais na mwananchi ambae ndo mwajiri basi
 
Nadhani watu hawafuatilii.....yaani mama si mnunuzi wa gari bali mama ni mkabidhi wa zawadi.....
 
Kituo kimoja Cha Afya kinagharim Ml 400. Hii inajumuisha ujenzi was majengo 5 ambayo ni Jengo la Mama na mtoto(martenity ward), OPD, Maabara, Labor ward na Makazi ya Mgangu Mkuu.

Hivyo, Mwinyi amepewa Kituo Cha Afya Kimoja akaongezwa na Zahanati moja. Hii ingewezwa kujengwa kwa Wananchi wa Kijijini
 
Kwamba Hussein hawezi kumnunulia babake personally mzigo wa 450mil? Kweli aliyenacho huongezewa
 
Huyu Mzee Ali Hassan Mwinyi hata angepewa magari 5 kama hayo Mimi naona sawa tu. Kwa wenye umri wa miaka zaidi ya 45 watakumbuka kuwa huyu Mzee Mwinyi kwa kipindi cha 1985-1995 ndiye aliyefanya maamuzi makubwa sana kutuvusha kutoka kwenye lindi la umaskini uliokithiri.

Akiba ya fedha za kigeni baada ya Vita vya Uganda iliteremka, nchi ilikuwa haikopesheki na maahirika ya fedha kimataifa, Watanzania walikuwa wanakula mchele wa msaada wa kitumbo, unga wa yanga. Halafu vyote hivyo unavipata kwa foleni. Huko Mtwara wananchi walikuwa wanavaa mifuko ya visulphate kama mashati.

Mwinyi ndiye aliyeruhusu biashara huria, kuanzishwa kwa daladala, kuingizwa kwa mitumba kutoka Ulaya. Akaruhusu watu wafanye biashara mbali mbali.

Hata privatization ya maahirika Kama TBL na TCC ilianzia kipindi chake na uanzishwai wa TRA.

Muache babu afaidi nchi aliyosaidia kuijenga
 
Mwanae pia n Rais angeweza kumnunulia.
 
Kama miaka 60 ya uhuru wetu bado hatujawahi kupata kiongozi bora kwa taifa hili, basi taifà halina watú bora. It's as simple as that, tusiendelee kulalamika, whether ni akili za kurithi, utapiamlo ama lishe duni, hatuwezi kulalamika tena. Taifa halina watu wenye uwezo...basi tena!
 
You are begrudging a 96 year old man getting a car that he can conveniently use?
 
Aisee mmenishangaza sana nyie watu kagari kanataka kuwatoa roho.
 
Yaani dah!
 
Ashakula ngapi mzee? Bado tu ale?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…