Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna kiongozi aliwahi kusema 2025 tutakuwa na umeme wa kutosha kutumia nchi nzima na tutauza hadi nje.
Afrika ni jini makata,haya majitu meusi ni majinga kuliko,Sina Imani kabisa baada ya Bandari kugawiwa yale majitu ya UAE
 
Wanaona gharama kujenga transimission line ndefu kwa ajili ya kusafirisha MW chache.. hivyo wanapiga shortcut kwa kununua hizo MW chache Kenya. Maana kenya na kaskazini ni karibu
unataka sema mikoa yote ya kaskazini umem hakuna? sa trnsmittion inakuwaje gharama ku-link baadhi ya sehemu zisizo na umeme huko kaskazini?
 
''Something is terribly wrong''
Tumeambiwa umeme wa JNHP unatosheleza nchi na kuuza nje
Tukaambiwa hata mvua isponyesha miaka 3 hatuna shida ya umeme

Kaskazini kuna Nyumba ya Munga na Hale Tanga zinazochangia grid ya Taifa
Tuna Upepo na Jua katika uwanda wa kuanzia Same hadi Singida

Tumejenga ''line' kuunganisha na Kenya ili tuweze kuwauzia umeme wa ziada tulio nao.

Leo tunasikia eti tunataka kuagiza umeme.

Huu mkanganyiko una mambo mawili kwa Wananchi. Ima wakae kimya kwasababu hawaelewi, na wale wanaoelewa wakae kimya kwasababu ya kuchanganyika. Kuna tatizo kubwa sana!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Umeme tunao hadi wa kuuza nje
Tunanunua tu kuwaungisha majirani wasinunee

MAJERANEEEE ITIKIAA AFANDEEEE
Bwawa lishauzwa mnazungumzia umeme gani wa kuuza nje au wa kuuziwa nje? Wawekezaji wamewekeza mpaka kwenye Bwawa unasema Bwawa la kwenu kwenu na nani? Gesi mnasema yenu yenu na nani na ishauzwa watu wanaipakua wanaenda kuuza nje huko nyinyi mpo tu
 
Wanaona gharama kujenga transimission line ndefu kwa ajili ya kusafirisha MW chache.. hivyo wanapiga shortcut kwa kununua hizo MW chache Kenya. Maana kenya na kaskazini ni karibu
Uvivu tu! chako ni chako tu.
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kusaini mikataba ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini ili Mikoa hiyo ipate umeme wa uhakika na iondokane na adha ya umeme kukatikakatika.

View attachment 3264483
Rais Samia amesema hayo baada ya kufungua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwenye hafla iliyofanyika Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo March 09, 2025.

Soma: Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje

View attachment 3264591
Rais Samia amesema "Umeme unakatikatika maeneo ya Kaskazini huku lakini Serikali yenu inachukua hatua ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa hii ya Kaskazini ili umeme upatikane masaa 24 muda wote bila kukatikakatika"

"Tuko kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba ili tuweze kununua umeme ule uungwe Kanda ya Kaskazini na Wananchi wafaidi na umeme, kwahiyo tutakuwa na umeme wa uhakika, maji ya uhakika kila pahali, Vijiji vyote vina umeme tunakwenda Vitongojo na umeme wa kutosha tunaununua unaingia ili kazi za maendeleo ziendelee"

Chanzo:
Millard Ayo
Mkubwa akisema imeisha hiyo
 
Wanasiasa wa tanzania ni wa kuchoma moto kabisa


Vyombo vya usalama wa nchi bado hawaoni sababu tu ya kuwaacha wananchi wachague viongozi kwa njia ya haki kuitia tume huru na katiba mpya.

Huyu aliyepo hajui hata ni kwa nini Aliyepita aliamua kujenga bwawa la Mwalimu Nyerere.

Hajui na hana habari kabisa .
Atatuachia madeni na makesi ya mikataba ya mabilioni kwenye umeme kama ilivyokua miaka yote na ufisadi .

Hapo ndipo hawa wanajeshi na polisi wanapokosea wananchi kwa kuendekeza Watawala wa CCM wanaokaa miaka mitano madarakani kwa ajili ya kujilimbikizia mali wakati polisi kwa mfano wanakaa kazini miaka 40 huku wakiwa hawaewi hata pesa za kuhamisha mizigo yao achilia mbali kikokotoo kinachowapa pesa zisizofikia mil.40.
Mtu anakaa madarakani miaka 10 analiachia taifa likiwa na madeni makubwa na hasara kila kona kutokana na kutaka kuwanufaisha watu wake bila kujali uchumi wa nchi utakua kwenye hali gani.

Tujiulize tu ni Lini mikoa ya Kaskazini wana uhaba wa umeme mpaka kufikia mahali pa kununua umeme kama Mkoa wa Kagera ?

Mikoa ya kaskazini wana chanzo cha Nyumba ya Mungu ,hale na umeme unaotoka Kwenye kiwanda cha sukari ungeweza kuingizwa kwenye gridi na kuongeza ukubwa wa umeme .

CCM imetydharau sana wapiga kura kwa sababu ya mfumo wa tume unaoua maamuzi ya kura za wananchi.

Yaani kweli kabisa Akina majaliwa, Kabudi ,Ndugai ,polepole,Makonda , Jafo, Januari ,Tulia ,Tibaijuka ,Mpina wote wamewakanyagia chini wanatuletea huyu aliyewahi hata kuchukua fomu na kuomba ridhaa kwa haki na kutuambia nini maono yake juu ya vizazi vya watanganyika mil 60 !!!
Yaani Tanzania tutoe fedha za tozo tupeleke nchi za nje kununua umeme wakati tuna gesi na makaa ya mawe ,upepo na joto kubwa la ardhini kwenye mikoa ya Singida ?
Kweli kabisa wanaCCM wanaona ni bora matakwa ya JK na familia yake na Samia wafurahie kwa maumivu makubwa ya Taifa kwa miaka mingi ijayo ?

Hii sio sawa .

Samia atalipeleka kubaya sana Taifa hili hasa Tanganyika atakua na kukiua kabisa chama cha mapinduzi .
Chama cha mapinduzi Mwisho wake ni huu wa utawala wa Samia . Kutakuwa kimechokwa na kuchukiwa sana na wananchi mpaka hivyo vyombo vya dola vitachoka sana kwa sababu wengi na watoto wa maskini ambao wanaona jinsi wanavyotaabika kwa manufaa ya watu wasio na uchungu na nchi hata kidogo. Magufuli aliwashuguulikia wapinzani lakini aliwashuguulikia mafisdi na kukataaichongo yao lakini huyu anawashughulikia wapinzani huku akiwachekea mafisadi na kufurahia michongo yao ya kifisadi
 
Wanaona gharama kujenga transimission line ndefu kwa ajili ya kusafirisha MW chache.. hivyo wanapiga shortcut kwa kununua hizo MW chache Kenya. Maana kenya na kaskazini ni karibu


Msiwe wavivu wa kufikiri.
Uvivu wa kufikiri ndio mitaji ya wezi wa rasilimali za umma .

Unajua Kiwanda cha Sukari Kinazalisha umeme unaoweza kugawa umeme mji wote wa moshi.?

Lini umewahi kusikia Mikoa ya kaskazini kuna uhaba wa umeme kama sio mchongo ?

Tangu mkoloni kaskazini mikoa ya Tanga Kilimanjaro na Arusha palikua na umeme wa kutosha .
Kuna chanzo cha Umeme Hale na Nyumba ya Mungu.

Kama umeme unaweza kufika Chalinze kwenye viwanda vingi utashindwa vipi kufika Tanga ?
Yaani Tanga mpaka Chalinze ni mbali kuliko Nairibo mpaka Tanga na Moshi .

Kama umeme utafika Dodoma Makao Makuu . Ni vipi ushindwe kufika manyara na Arusha .

Je,gharama za kutoka nchi nyingine mpaka Manyara ni ndogo kuliko kuutoa umeme Dodoma mpaka Arusha na manyara .


Haya ndiyo mama yanayotakiwa kwa wapinzani na wazalendo kujitokeza na kuandamana kwa nguvu zote kupinga huu ufisadi mkubwa unaotengenezwa .
Kenya waliomba kuuziwa umeme na gesi na makaa ya mawe . Leo Kenya wanatuzia umeme .
Au ndio ile kasi ya magari yao kupeleka makaa ya mawe Kenya sasa Kenya wamezalisha uleme kutuuzia tena badala ya sisi kuwauzia ?
Inamaa kila awamu inaojinufaisha na michongo ya uhaba wa umeme wakati JPM alikaa miaka sita bila umeme kukatika wakati huo hakuna bwawa la Nyerere.
 
Tukisema chadema huwa hawana akili ndiyo mtambue, gharama ya kutengeneza njia kuu ya umeme ya kv 33, toka ilipo kwa sasa mpaka uifikishe mombo ni gharama kubwa mno, kwa kutatua matatizo ya dharura ni heri kuuchukuwa kutoka Kenya, kupeana umeme kibiashara ni jambo la kawaida.(Amerika inaumeme mwingi sana, lakini kanada imeipa umeme amerika wa kibiashara wa makazi 15,000, almost mpaka NY inatumia umeme wa kanada.
Unafikaje kenya same na mwanga inarukwa? Hii ilikuwa 2021 hatua za kukamilika bwawa la nyerere

View: https://x.com/JamiiForums/status/1468302027193307138?t=-cjouoo7PrWf8M79EfasrA&s=19
 
Huyo ma rope alisema bwawa likijaa hata mvua isiponyesha miaka mitatu hakuna shida.

Kama hii nchi imeuzwa au kukodishwa tupewe chetu tuamue moja
 
Back
Top Bottom