Pre GE2025 Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Naomba kueleweshwa, huo umeme tutakao nunua kutoka Ethiopia.Utapitia gridi ya Kenya?
 
Naunga mkono hoja, kuna tatizo mahali, ila pia badala ya kulaumu, tumpongeze Samia kuwa mkweli kuonyesha tuna shida mahali bila kusema hiyo shida ilipo!.

Angekuwa mwingine, tungenunua kimya kimya bila kusema popote!. Tumshukuru Samia for genuinity, hapa sasa ndio IJ ya umeme tuingie kazini kuyafukunyua haya madudu ya Tanesco.

Hii ya mkuu wa nchi kukubali kuna vitu sisi wenyewe hatuwezi, lazima tusaidiwe is a good thing, its about
being genuine!. Niliwahi kushauri Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? hata Tanesco nadhani hatuwezi, tukubali kusaidiwa.

Hata hili la kufanya minimum reforms kwenye katiba ili tufanye uchaguzi huru na wa haki, nadhani wale vilaza wake wa sheria, wameshindwa kumshauri vizuri, hivyo watu tumejitolea kumsaidia, lazima tufanye minimum reforms kwenye katiba ili tuweze kufanya uchaguzi wa haki, ila kwenye ushindi ni Samia Pekee, she is the one and only, hili nimemhakikishia ni yeye tuu Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

P
 
Hivi mfano sisi wa Tanzania tukamuomba Elon Musk awe raisi wa taifa letu kwa mkabata maalumu wa miaka 10 wenye kufungu cha kumtoa kama atakiuka,hivi inashindikana?

Atupeleke mchaka mchaka wa miaka 10 akituachia tuwe hatua tatu nyuma ya china.
Kuna ‘petition’ imeandaliwa ikipendekeza Ibrahim Traore awe Rais wa Africa. Siku za karibuni itafika Tz kwa kutiwa saini. Tutarajie SSH ataunga mkono hii hoja
 
Kuna haja gani ya kufanya uchaguzi (huru na wa haki au vinginevyo) ikiwa una uhakika wa atakayeshinda kama unavyodai? Kwa kuwaita wasaidizi wa Rais ‘vilaza’, huoni unaidhalilisha ofisi ya Rais na Rais unaedai kumsaidia?
 

Sasa mbona huku Minjingu ,monduli kuna Minguzo Mikubwa imekatisha tunaambiwa umeme unaenda kuuzwa nje? Sa inakuwaje tena sisi ndio tunanunua?
 
Kama tuna umeme wa kutosha kwanini tununue? Au ndiyo mambo ya kudanganywa kama watoto wadogo na hii serikali.
 

Wezi wanataka kuiba tu. Eti umeme unatoka Ethiopia . Ni bwawa sasa umeme wetu wa bwawa vipi? Yaani umeme wa Ethiopia unapita nchi ngapi? Wanasingizia umbali. Kusini ni mbali kuliko Ethiopia!
 
Chawa Pro Max umeshtuka eeh!
 
Sababu umbali, cha kujiuliza umeme siyo mawe useme ni bora ununue mpakani mwa Kenya kuliko kuyafata mawe Rufiji kuyapelela Same, Kwanii umeme wasinunue kutoka Moshi kuliko kwenda kununua Ethiopia
 
Na kuna umeme umepita arusha unaenda kenya, au wata u reverse?
Wanaona gharama kujenga transimission line ndefu kwa ajili ya kusafirisha MW chache.. hivyo wanapiga shortcut kwa kununua hizo MW chache Kenya. Maana kenya na kaskazini ni karibu
 
Na kuna umeme umepita arusha unaenda kenya, au wata u reverse?
Wanaona gharama kujenga transimission line ndefu kwa ajili ya kusafirisha MW chache.. hivyo wanapiga shortcut kwa kununua hizo MW chache Kenya. Maana kenya na kaskazini ni karibu
 
Ila kiuhalisia hii nchi viongozi sjui wanatuoonaje juzi waziri kasema umeme upo mpaka wakuuza nje leo tena hv ila muhm watanzania tusiwekeze tumaini kwa kauli yoyote toka kwa wanasiasa.wamechakugua kutuona mafala
 

Kwa stlye hii kila mtu mtamuona Hana akili na sio chadema Tu

Shida yenu huwa mnaongea Kwa mihemuko Sana mpaka mnajisahau

Mara zote mnasema umeme ni mwingi mpaka mnataka kuuza nje

Hamna siku mmewahi kusema umeme ni mwingi yes but not Kwa zone ya kaskazini

Au mnaposema inchi mzima shida ya umeme imeisha, kule kaskazini sio Tanzania?

That's why watu wanahisi mnawaibia
 
Huu umeme unazalishwa Ethiopia, Kenya alinunua huko na ndio na sisi tunataka kuunganishwa kupitia Kenya. Bei yake ni rahisi ikilinganishwa na bei zetu za umeme.

Why tuliingia gharama za bwawa la Nyerere? Why tulikata miti yote Ile?

Hiyo ela si tungenunua Tu umeme kutoka huko Kenya Kwa umeme wa inchi mzima?
 
Kwani bwawa la Nyerere lote limeanza uzalishaji at once? Nusu tuu ya mashine zao ni bwawa Zima la Nyerere.

So wataanza na hizo,bwawa Lina uwezo wa Kuzalisha zaidi ya megawatt 5,000

Why tusimalize bwawa la Nyerere?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…