..watendaji wametoka Dodoma mpaka Zanzibar kwa ajili ya shughuli ya malisho tu?
..kuna awamu ambazo wateule wote waliapishwa Ikulu Dsalaam, na kulikuwa hakuna hotuba za mipasho.
Exactly!
Hizi gharama ni ufujaji wa pesa. Rais SSH angeweza kuwa apisha kabla hajaondoka
Lakini pia umuhimu wa kuapishwa kila mara mtu akibadilishiwa majukumu uko wapi?
USA wanaoteuliwa na kuthibitishwa na Senate wakibadilishwa nafasi hawarudi tena kuhojiwa na Senate
Nchi masikini tunapata wapi pesa za kuchezea za kubeba watu kutoka Dodoma kwenda Zanzibar n.k.
Rais SSH analalamika kuhusu mapato, katika hali hii matumizi ya serikali ni makubwa sana na ya anasa.
Muda wa kufanya sherehe katika nchi masikini kama yetu upo wapi?
Nyerere , Mwinyi, Mkapa waliapishwa watu kimya kimya tena ni Ikulu Dar siyo Butiama au Lupaso
Haya yalianza na JPM na sasa yamekuwa utamaduni unaotugharimu fedha nyingi.
Tuna matatizo mengi, okoeni muda acheni matumizi ya pesa za umma bila sababu
Rekebisheni sheria ya kuapishwa ( na hata sijui ina maana gani) hatuhitaji kila siku na wala hatuhitaji kusikia mnapeana hadithi za majukumu! tunataka matokeo ya kuondoa umasikini
Nchi yetu ina viongozi wanaopenda anasa sana, serikali ni kubwa na matumizi ni makubwa ya anasa