Rais Samia, shughuli za uapisho nchini ni gharama kubwa zisizo za lazma, Viongozi badilikeni

Rais Samia, shughuli za uapisho nchini ni gharama kubwa zisizo za lazma, Viongozi badilikeni

Toka maktaba:

Wateuzi wa Gavana wa Tanganyika waja juu baada ya lawama kibao :

Katika kurasa zinazofuata ninasimulia hadithi ya miaka minne kati ya Septemba 1956 nilipohitimu kozi elekezi Oxford na Agosti 1960 nilipomaliza ziara yangu ya kwanza kama Afisa wa Wilaya katika Utumishi wa Kikoloni katika Tanganyika (iliyoitwa Tanzania mwaka 1964).


Nikiwa Afisa wa Wilaya DO / District Officer, nilikuwa msimamizi mdogo na mtu wa kufanya shughuli zote wakati nikiwa wakala wa mamlaka ya kikoloni wakati Tanganyika ilipokuwa sehemu ya Milki ya Uingereza.

Ilikuwa kazi ambayo nilikuwa na furaha sana na iliyotimizwa kabisa na ninatumai wasomaji wa familia watapata faida kujifunza nilichokuwa nikifanya wakati huo. Wakati huo huo najua kuwa aina ya kazi niliyofanya baadaye imekuwa chini ya ukosoaji mkubwa.

Mwanzoni mwa miaka ya 1960, wanahistoria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliishtaki serikali ya kikoloni kwa kutokuwa na uwezo na wakati fulani kwa nia mbaya, na wanahistoria waliofuata na waandishi wa habari wamepuuza mafanikio yake au walitaka kuyadharau.

Kwa mfano, Rais wa Jamhuri ya Tanzania alisema muda si mrefu uliopita, Serikali ya kikoloni haikuwa na nia ya kuendeleza nchi bali ilitaka kunyonya rasilimali zake.” Maoni yake yanaonekana kushirikiwa na baadhi ya watoa maoni katika nchi hii, na hata na sauti zenye mamlaka katika maeneo kama vile BBC na gazeti la Times.

Soma zaidi lawama :
Source : https://www.britishempire.co.uk/article/districtofficerintanganyika.htm
 
Hivi nyie watawala wa hii nchi ni mpaka watanzani nao siku moja wafanye maamuzi magumu kama vijana wa Kenya?

Like kundi lote kwenye uapisho lina ulazima gani na ni kwa gharama ya nani?

Watu wanapanda ndege kutoka Dodoma mpaka Zanzibar na kurudi bila sababu yoyote ya msingi eti kwenda kushiriki uapisho tu wa viongozi wawili au watatu.

Kwanini mnapenda ufahari katikati ya umaskini?

Wakati mwingine matendo yenu ni ndio chanzo cha watu kuwaandika vibaya mitandaoni.

Hii nchi inatafunwa sana na kundii dogo la watu.

Anyway, labda ni mpango wa Mungu kuwafanya watawala kuwa na mioyo migumu kama Farao ili siku moja makusudio ya. Mungu yatimie juu ya watu wake.

Inaumiza sana.
Kwani wana akili hizo hawa waliolelewa kidini? Hata akina mama wakijifungulia chini ni sawa tu ili mradi wenyewe wanaweza kufanya anasa zao. Kinachowauma ni kukosolewa tu mitandaoni
 
TAFAKURI YA NYAKATI ZETU

"A time is coming when men will go mad, and when they see someone who is not mad, they will attack him, saying, "You are mad; you are not like us."- St. Anthony the Great of Egypt

"Wakati unakuja ambapo watu watakuwa na wazimu, na wakimwona mtu asiye na wazimu, watamshambulia, wakisema, "Wewe ni wazimu; wewe si kama sisi."
- Mtakatifu Anthony Mkuu wa Misri
 
Kwani wana akili hizo hawa waliolelewa kidini? Hata akina mama wakijifungulia chini ni sawa tu ili mradi wenyewe wanaweza kufanya anasa zao. Kinachowauma ni kukosolewa tu mitandaoni
Tatizo wanasahau walikotoka. Wengi wao wametoka katika familia masikini ila wakipata madaraka wanasahau kabisa walikotoka. Hopeless kabisa.
 
Kuna vipengele sio maisha ni magumu mno mtaani halafu watu wananeemeka kipuuzi tu sawa amani imeyumba Kenya lakini je maamuzi aliyoyachukua Ruto huoni kuwa yanaenda kupunguza kutafunwa hovyo kwa Pesa ya walipa kodi wa Kenya?tetea vitu kwa hoja zinazoeleweka acha kuwatisha watu unategemea kundi hili dogo litajineemesha mpaka lini?tumechoka
Lazima tuamke kulinda raslimali zetu
 
Katiba inataka Rais awaapishe..haisemi awaapishie wapi..labda hata kwa zoom
Ndio maana tunataka katiba. Iliyopo iliandikwa kwa dhana ya ''Uaminifu na Uadilifu'' ndio maana watu kama Nyerere walitumia uadilifu kutambua kwamba Butiama ni makazi, hawakuapisha watu huko.

Katiba haikuzingatia tunaweza kupata viongozi ''morally bankruptcy''
Viongozi watakao 'abuse' ile freedom iliyotolewa na katiba kwamba wanaweza kuapisha popote

Kama viongozi wangekuwa ''waadilifu' wangefanya kupitia Zoom lakini hawajali, ni anasa tu

Hoja si Katiba ieleze kila kitu , hapana! tunahitaji katiba itakayowafanya watawala wajiulize maswali kabla ya kuchukua hatua au kutenda jambo. Ufujaji ni kwa kujua wakistaafu! wala hawashtakiwi

Leo kuna akina mama wanapokezana vitanda wakiwa na ''Vichanga' mikononi halafu kuna watu wapo Hotel za nyota tano wanakwenda kuapishwa! Wanaolipa kodi za nyota tano ni akina mama na vichanga

Tuna vituo vya afya havina '' solar' lakini tuna pesa za kusafirisha watu na hoteli nyota tano kwenda kuapishwa

Mh Rais alitakiwa aone uchungu na kuzuia matumizi mabaya ya rasilimali, haikuwa dharura ! .
 
Waige uingereza kiongozi mkuu (waziri mkuu) amechaguliwa jana, siku hiyo hiyo ameanza kazi hamna uapisho wala masherehe ya kukusanya watu, kesho yake ametangaza baraza la mawaziri na kazi zimeanza.

Hamna gharama za uapisho, mikusanyiko uwanjani, wageni wa nje n.k. pia baraza limeteuliwa ndani ya siku moja hamna kupoteza muda.

Nchi tajiri zinamatumizi mazuri kuliko nchi masikini.
 
Waige uingereza kiongozi mkuu (waziri mkuu) amechaguliwa jana, siku hiyo hiyo ameanza kazi hamna uapisho wala masherehe ya kukusanya watu, kesho yake ametangaza baraza la mawaziri na kazi zimeanza.

Hamna gharama za uapisho, mikusanyiko uwanjani, wageni wa nje n.k. pia baraza limeteuliwa ndani ya siku moja hamna kupoteza muda.

Nchi tajiri zinamatumizi mazuri kuliko nchi masikini.
Njoo bongo sasa. Wateule wote watakusanyika kwenda Mwanza kwa gharama za serikali ndege na maprado.

Unajua kwa kuwa hawatumii pesa zao mfukoni they do whatever they wish
 
Back
Top Bottom