Rais Samia, shughuli za uapisho nchini ni gharama kubwa zisizo za lazma, Viongozi badilikeni

Kuna vipengele sio maisha ni magumu mno mtaani halafu watu wananeemeka kipuuzi tu sawa amani imeyumba Kenya lakini je maamuzi aliyoyachukua Ruto huoni kuwa yanaenda kupunguza kutafunwa hovyo kwa Pesa ya walipa kodi wa Kenya?tetea vitu kwa hoja zinazoeleweka acha kuwatisha watu unategemea kundi hili dogo litajineemesha mpaka lini?tumechoka
 
..watendaji wametoka Dodoma mpaka Zanzibar kwa ajili ya shughuli ya malisho tu?

..kuna awamu ambazo wateule wote waliapishwa Ikulu Dsalaam, na kulikuwa hakuna hotuba za mipasho.
Exactly!

Hizi gharama ni ufujaji wa pesa. Rais SSH angeweza kuwa apisha kabla hajaondoka
Lakini pia umuhimu wa kuapishwa kila mara mtu akibadilishiwa majukumu uko wapi?

USA wanaoteuliwa na kuthibitishwa na Senate wakibadilishwa nafasi hawarudi tena kuhojiwa na Senate

Nchi masikini tunapata wapi pesa za kuchezea za kubeba watu kutoka Dodoma kwenda Zanzibar n.k.
Rais SSH analalamika kuhusu mapato, katika hali hii matumizi ya serikali ni makubwa sana na ya anasa.
Muda wa kufanya sherehe katika nchi masikini kama yetu upo wapi?

Nyerere , Mwinyi, Mkapa waliapishwa watu kimya kimya tena ni Ikulu Dar siyo Butiama au Lupaso
Haya yalianza na JPM na sasa yamekuwa utamaduni unaotugharimu fedha nyingi.

Tuna matatizo mengi, okoeni muda acheni matumizi ya pesa za umma bila sababu
Rekebisheni sheria ya kuapishwa ( na hata sijui ina maana gani) hatuhitaji kila siku na wala hatuhitaji kusikia mnapeana hadithi za majukumu! tunataka matokeo ya kuondoa umasikini

Nchi yetu ina viongozi wanaopenda anasa sana, serikali ni kubwa na matumizi ni makubwa ya anasa
 
Ameshatuzowea! Hatusikilizi tena! Wala haogopi kutumia matumizi makubwa yasiyo na tija!
Chawa wake wakiongozwa na 'Stive Nyerere' wapo Koreaaaaaaa, kwa kodi zetu, na bila ruhusa yetu!
 
Amka uandamane basi kama ni rahisi kiasi hicho.
 
Katiba inataka Rais awaapishe..haisemi awaapishie wapi..labda hata kwa zoom
 
Hapo unaweza kuta imetumika bilioni 10 kukamilisha tukio hilo tu. Pesa nyingi zinatumika kwenye matumizi yasiyo muhimu wala ya lazima.
 
Hapo unaweza kuta imetumika bilioni 10 kukamilisha tukio hilo tu. Pesa nyingi zinatumika kwenye matumizi yasiyo muhimu wala ya lazima.
Kuna wazazi wanalala katika vitanda kwa zamu katika Hospitali zetu. Ukiuliza bei ya kitanda kimoja halafu ukalinganisha na ghara za 'kuapisha' watu tena si kwa dharura utasikitika sana.

Wazazi wanalala na kujifungulia sakafuni halafu wanalipa kodi za watu kusafiri kutoka Dodoma kwenda Zanzibar kuapishwa na gharama zinazoambatana nazo. Kwanini wasimsubiri Rais arudi au kwanini hawakwenda kabla hajaondoka. Hizi sherehe za kuapishwa ni anasa tu! watu wetu ni masikini hawahitaji hizi anasa

Sheria ibadilishwe, kiongozi akipaishwa na kuhamishwa hakuna kuapishwa tena.

Hatuhitaji kusikia Rais anawapa majukumu gani, tunahitaji kuona changamoto zinatatuliwa.
Waongee huko ofisini sisi tunataka matokeo.
 
Kinachokwamisha maendeleo ya Tanzania ni matumizi mabaya ya pesa za umma tu. Wanapohimiza watu walipe kodi na wao wanaongeza matumizi ya anasa. Wasichokijua wananchi wengi ni kwamba hao walioko kwenye serikali hawajali kabisa maisha yao.
 
Mshahara wake haukatwi kodi ndiyo maana hana uchungu na mali za nchi hajui maumivu ya walipa kodi, huwezi kuwa na Rais anahimiza watu walipe kodi huku yeye hataki mshahara wake ukatwe kodi, shame on us.
 

Umenena ukweli mtupu. Watu wengi wanaona maovu ya nchi hii yanayofanywa na watawala.

Watawala siyo tu bubu bali ni viziwi pia, wakiamini hakuna wa kuwafanya kitu, lakini wajue kuna siku wasioijua, watajuta.
 
Pesa ndio zinavyo ingia kwenye mzunguko hivyo jamani
Wataalamu wa uchumi wanasema zinaleta Multiplier Effect
 
Pesa ndio zinavyo ingia kwenye mzunguko hivyo jamani
Wataalamu wa uchumi wanasema zinaleta Multiplier Effect
acha uhuni🤣
Kinachochochea uchumi ni uzalishaji na balance of trade. government expenditure hazisaidii uchumi.
 
acha uhuni🤣
Kinachochochea uchumi ni uzalishaji na balance of trade. government expenditure hazisaidii uchumi.
Zinasaidia
Kama hapo ZNZ ina maana walilala hotelini kunywa chai kwenye migahawa etc wenyeji hawaja neemeka hapo na kutoa machozi ya furaha
 
Ni muhimu sana ili Watanzania waelewe sababu za watu kunyofolewa na kuapishwa wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…