Rais Samia sijakuelewa hapa unapotaka Kushauri na Kuamrisha kuwa Jina la Wafungwa libadilishwe na sasa wawe wanaitwa Wanafunzi

Kaja na uzanzibari, kule wanaita chuo cha mafunzo
 
Unashangaa hiyo mkuu. Kaamuru itangazwe tenda ya vitaru vya uwindaji na kwamba simba na Tembo wazee wawindwe. WAZEE!! Muwindaji ana kitaru chake ameruhusiwa kuua simba na Tembo halafu aanze kuchunguza simba na Tembo wazee ndiyo awaue!! Dunia inapiga vita kuua Tembo yeye anaruhusu kuua Tembo!!

Achana na hiyo. Amepokea report ya uchafuzi wa mto MARA kwamba kinyesi na mikojo ya ng'ombe ndiyo chanzo cha uchafuzi huo nae kakubaliana na report hiyo. Maji ya mto yanasafiri iweje ng'ombe wakojoe na mkojo huo utuame? Licha ya hivyo miaka ya nyuma ndiyo kulikuwa na ng'ombe wengi mbona madhala hayo hayakujitokeza?

Ukiendelea kushangaa hayo jiulize ni kwa nini alitengua uteuzi wa waziri wa ardhi aliyepunguza kama si kumaliza matatizo ya malalamiko ya ardhi?
 
Wote ni sawa TU mana wasomi wa Bara ndio wahalifu wa kubwa wanaotuibia mabilioni ya fedha za umma na kutengeneza umaskini mkubwa unaoleta uhalifu mdogo unaoleta wanafunzi wa hovyo magerezani.


Vyuo na mashule yetu yameshindwa kuzalisha watu wema.
Wauza madawa ,walevi wa kupindukia,wezi wa madawa na vifaa tiba , Wala rushwa , wadangaji wakubwa, wachepukaji wakuu, wazinzi wakuu, wauzaji wa ardhi mara mbili mpaka tatu, wauaji wa watu wasio na hatia, watekaji, wanaoua Wafanyabiashara wa madini na kupora madini yao, wanasiasa wa hovyo wa aina ya Dr. Mihogo na Mapropesa Samadi,Propesa Jalalani, Propesa Tume ya uchaguzi Kupiga pesa za umma. Wanaochoma majengo ya umma ili wapige pesa za michakato ya ujenzi na uovu mwingi na utakatishaji wa fedha wote ni wale waliohutimu kwenye vyuo na mashule yenye hulkana fikra za kihalifu.

Tofauti ya wanafunzi wa vyuo vyetu na wale wafungwa(wanafunzi ) wa magereza yetu ni kuwa VYUO( Vikuu , vya kati na vya ufundi) wanafunzi wanaanza mafunzo wakiwa watu wema Kisha wanahitimu wakiwa Wahalifu na wanakwenda kutumia Elimu yao kufanya uhalifu unaoathiri vizazi na vizazi Kwa mamilioni ya Watanzania .
Ilihali wafungwa( wanafunzi wa vyuo vya magereza ) wanaanza mafunzo wakiwa Wahalifu Kisha wanahitimu wakiwa watu wema.
Wahalifu Hawa ni wabaya sana mana Mwenzao akijaribu kuwapinga au kuwasaliti anapata majanga makubwa na kukosa pa kukimbilia mana kila anapokimbilia anakutana na Wahalifu ambao wanamuona kuwa ni msaliti anayezuia maslahi yao na vyeo vyao. Matokeo yake ama analogwa au anatafutiwa zengwe au anapotezwa kabisa.

Kwa kweli ukitizama Kwa makini Vyuo vyetu na Magereza Vyote ni vyuo vinavyotegemeana.

Ukitaka Chuo Cha magereza kikose wanafunzi basi ni lazima vyuo vya Elimu na mashule yatoe wahitimu wema ,wenye nia njema na wazalendo wa kweli sio tu makada wa vyama hatimaye tuwe na jamii yenye wasomi wazalendo wenye kuuchukia uhalifu na sio kuusifia na kuulinda Kwa sababu TU umefanywa na watu walioshika kalamu na Computer kwenye ofisi yenye kiyoyozi bila jasho.
 
Tofauti ya wanafunzi wa vyuo vyetu na wale wafungwa(wanafunzi ) wa magereza yetu ni kuwa VYUO( Vikuu , vya kati na vya ufundi) wanafunzi wanaanza mafunzo wakiwa watu wema Kisha wanahitimu wakiwa Wahalifu na wanakwenda kutumia Elimu yao kufanya uhalifu unaoathiri vizazi na vizazi Kwa mamilioni ya Watanzania .Wahalifu Hawa ni wabaya sana mana Mwenzao akijaribu kuwapinga au kuwasaliti anapata majanga makubwa na kukosa pa kukimbilia mana kila anapokimbilia anakutana na Wahalifu ambao wanamuona kuwa ni msaliti anayezuia maslahi yao na vyeo vyao. Matokeo yake ama analogwa au anatafutiwa zengwe au anapotezwa kabisa.

Ilihali wafungwa( wanafunzi wa vyuo vya magereza ) wanaanza mafunzo wakiwa Wahalifu Kisha wanahitimu wakiwa watu wema.


Kwa kweli ukitizama Kwa makini Vyuo vyetu na Magereza Vyote ni vyuo vinavyotegemeana.

Ukitaka Chuo Cha magereza kikose wanafunzi basi ni lazima vyuo vya Elimu na mashule yatoe wahitimu wema ,wenye nia njema na wazalendo wa kweli sio tu makada wa vyama hatimaye tuwe na jamii yenye wasomi wazalendo wenye kuuchukia uhalifu na sio kuusifia na kuulinda Kwa sababu TU umefanywa na watu walioshika kalamu na Computer kwenye ofisi yenye kiyoyozi bila jasho
 
Kuna memba mmoja wa uhamsho aliwahi kusikika watu wa bara hawajui kiswahili akatoa mfano, Halima wamwita Alima.
 
Mkuu yaani nimesikitika na kumshangaa sana. Kuna Kitu niliambiwa nikakibishia ila kwa sasa taratibu naanza Kukiamini. Ama hakika Kazi tunayo na Kazi iendelee pia.
Kitu gani hicho mkuu,tusokeze kwa mbali ,tutoe tongotongo
 
Kwa uchambuzi huu nimetulia. Keep it up Mkuu.
 
MWACHE MAMA YETU AFANYE KAZI YA KUIFUNGUA NCHI MBONA MTANGULIZI NAYE ALISEMAGA WASTAFU WANAWASHWA PIA WAMESABABISHA MATATIZO ANAYOSUMBUKA NAYO.MAMENO YAPO NA DAWA YAKE KUYASEMA NDO NAFSI HUTULIA WEWE YANAWEZA KUKUKERA ILA WENGINE WANAFURAHI NANI ASISEMWE NA BINADAMU YESU MWENYEWE ALISEMWA SEMBUSE HUYO KWA HIYO VUMILIA MKUU NDO MAISHA YALIVYO WHAT GOES AROUND IS WHAT COME AROUND
 
Wnafunzi wa ujambazi, tuombeane dear, tupo pabaya sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…