Atuongoze Bara kwa Sheria na taratibu zake. Vinginevyo na Sisi Bara tuwe na haki ya kugombea urais Zanzibar ili nasi tulete huko ya Kibara. Nchi hizi mbili ni tofauti kabisa na ninashangaa ni kwa nini turuhusu upande mmoja uwe unaweza pia kuongoza upande wa Nchi nyingine. Tunahitaji katiba mpya na Muungano ufumuliwe ili tuuweke Sawa tuje na Muungano ambao unayo mambo machache ya kushirikiana kama yapo.
Unaona sasa mnataka kudhalilisha uanafunzi Bara. Yaani haiwezekani kabisa Mwanafunzi wa shule awe na jina la Mfungwa wa aliyembaka. Samahani Sana kama ninakuudhi Ila pia huoni Hilo jina mnaita Wafungwa Zanzibar ndiyo maana hata Kielimu matokeo yakitoka hamuwezi kabisa kuuifikia Bara? Kwa kuwa tayari Wanafunzi wenu Zanzibar ni Wafungwa kisaikolojia inaathiri mno. Badilisheni Hilo jina waitwe tu jina lingine lakini siyo Wanafunzi. Chondechonde isije Bara hii kitu ibaki Zanzibar.
Wote ni sawa TU mana wasomi wa Bara ndio wahalifu wa kubwa wanaotuibia mabilioni ya fedha za umma na kutengeneza umaskini mkubwa unaoleta uhalifu mdogo unaoleta wanafunzi wa hovyo magerezani.
Vyuo na mashule yetu yameshindwa kuzalisha watu wema.
Wauza madawa ,walevi wa kupindukia,wezi wa madawa na vifaa tiba , Wala rushwa , wadangaji wakubwa, wachepukaji wakuu, wazinzi wakuu, wauzaji wa ardhi mara mbili mpaka tatu, wauaji wa watu wasio na hatia, watekaji, wanaoua Wafanyabiashara wa madini na kupora madini yao, wanasiasa wa hovyo wa aina ya Dr. Mihogo na Mapropesa Samadi,Propesa Jalalani, Propesa Tume ya uchaguzi Kupiga pesa za umma. Wanaochoma majengo ya umma ili wapige pesa za michakato ya ujenzi na uovu mwingi na utakatishaji wa fedha wote ni wale waliohutimu kwenye vyuo na mashule yenye hulkana fikra za kihalifu.
Tofauti ya wanafunzi wa vyuo vyetu na wale wafungwa(wanafunzi ) wa magereza yetu ni kuwa VYUO( Vikuu , vya kati na vya ufundi) wanafunzi wanaanza mafunzo wakiwa watu wema Kisha wanahitimu wakiwa Wahalifu na wanakwenda kutumia Elimu yao kufanya uhalifu unaoathiri vizazi na vizazi Kwa mamilioni ya Watanzania .
Ilihali wafungwa( wanafunzi wa vyuo vya magereza ) wanaanza mafunzo wakiwa Wahalifu Kisha wanahitimu wakiwa watu wema.
Wahalifu Hawa ni wabaya sana mana Mwenzao akijaribu kuwapinga au kuwasaliti anapata majanga makubwa na kukosa pa kukimbilia mana kila anapokimbilia anakutana na Wahalifu ambao wanamuona kuwa ni msaliti anayezuia maslahi yao na vyeo vyao. Matokeo yake ama analogwa au anatafutiwa zengwe au anapotezwa kabisa.
Kwa kweli ukitizama Kwa makini Vyuo vyetu na Magereza Vyote ni vyuo vinavyotegemeana.
Ukitaka Chuo Cha magereza kikose wanafunzi basi ni lazima vyuo vya Elimu na mashule yatoe wahitimu wema ,wenye nia njema na wazalendo wa kweli sio tu makada wa vyama hatimaye tuwe na jamii yenye wasomi wazalendo wenye kuuchukia uhalifu na sio kuusifia na kuulinda Kwa sababu TU umefanywa na watu walioshika kalamu na Computer kwenye ofisi yenye kiyoyozi bila jasho.