Pre GE2025 Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya

Pre GE2025 Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Alimuuwa baba'ko au mama'ko?
Mzee Kibao alikuwa Mtoto, Kaka, Baba, Mjomba, Binamu, na Babu za watu. Yesu alisema, nilikuwa sina maji, ulinipa, nilikuwa sina chakula ulinipa, nilikuwa sina pakulala ulinipa, Basi ujue unapo msaidia MTU yeyote , ndivyo hivyo hivyo unapomtendea Mema Yesu.
 
Mwana kadhaa wa kadhaa ana ndugu zake jibuni hoja.

Chadema walivyo wahuni utasikia wanaanza kujiita "sisimizi".
 
Mzee Kibao alikuwa Mtoto, Kaka, Baba, Mjomba, Binamu, na Babu za watu. Yesu alisema, nilikuwa sina maji, ulinipa, nilikuwa sina chakula ulinipa, nilikuwa sina pakulala ulinipa, Basi ujue unapo msaidia MTU yeyote , ndivyo hivyo hivyo unapomtendea Mema Yesu.
Taja jina lake kamili.
 
Rais Samia amesema anasikitishwa baada ya kusikia mwenyekiti (yeye) anavyoshambuliwa na kusema ukweli wanaujua hivyo wasimame imara, akisema mdomo wa mwenyekiti mmoja kujibu hoja zinazotolewa hautoshelezi na ana majukumu mengi badala yake wasimame kujibu hoja hizo.

Wakiambiwa mwenyekiti wao/ Rais ni muuaji wajibu kweli, ameua nguvu hasi ya upinzani, ameua njia zote za kuzidisha umasikini nchini na amekuza uchumi wa nchi hii, ameua giza lililokuwa limegubika Tanzania na kwamba sasa tanzania katika kiwango cha kimataifa inang'ara.

Haya ndio aliyowahi kuua, hajawai kuua mtu, labda sisimizi ndio amewahi kuua.

Vipi hata huko zenji kuna utekaji na mauwaji kama huku ???
 
Hutokuja kuiona hiyo, umesikia hata wakitoa mrejesho! wangapi wamekamatwa kusaidia uchunvuzi? {unakumbuka alipotekwa Mo walivyokuwa wanatoa mrejesho}
sasa kwa kisa hiki ilitakiwa mrejesho na mikwala ya police iwe vile , ukimya huu jiongeze ndio imepita hiyo. Nilitegemea huyu mama kuwa kazi itakamilika soon na lipoti itawekwa wazi, ila kamfananisha alieuawa na sisiminzi. Yaani yeye kaua sisiminzi asisakamwe... mwee
Hii nilikuwa sijaliona kwa hicho la tatu, tunashukuru kwa kuonyesha kwamba kama kaumiza ni sisimizi tu.
 
Haya ndio aliyowahi kuua, hajawai kuua mtu, labda sisimizi ndio amewahi kuua.
EEEeeennHHEEEEE!
Huyu na mipasho sijui tutafika wapi; hata kwenye mambo mazito ni mipasho tu kama kawaida.

Kwani Mwenyekiti/Rais kuua ni mpaka ashike upanga achinje mtu yeye mwenyewe?

Anaposikia watu wakilia "kutekwa na kuuawa" na yeye kuishia kukejeli hali hiyo kuwa ni drama; badala ya kuchukua hatua madhubuti kuzuia uovu huo; huko siyo kuua?

Anapo teua watu kwa lengo maalum katika maeneo yanayo endesha hayo mambo maovu, yeye haoini kuwa ndiye muuaji moja kwa moja?

Anapo simamia utungaji wa sheria inayo ruhusu kundi la watu kushikilia raia, kuwapoteza na hata kuwaua na kuisaini sheria hiyo haoni kuwa yeye ndiye muuaji moja kwa moja?
 
Sawa bibi chaudere haujawahi kuua lakini kwa nini wanao kukosoa wengi wanatekwa na wengine kuuliwa kabisa? Uchumi huu ambao umeshuka kama suruali ya bishoo ndio anasema umepanda ? Shilingi inazidi kuanguka kila siku na maskini wanazidi kua wengi kila leo alafu anajipaka mafuta kwa mgongo wa chupa ? anaowatuma kumsemea hata na wao kuna muda wanaona aibu kuongea uongo japo ndio kazi yao, vitu vingine inabidi ucheke tuu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hata ukimuumiza Faizan Foxy basi umemuumiza Yesu na hata pia Mohammed, kwani wote hawashadadi Maovu
Nyie watoto msio na baba ndiyo zenu hizo, tunawajuwa, akifa mtu ndiyo mnajitokeza kudai urithi. Alipokuwa hai mlikua wapi?

Hata jina umeshindwa kutaja.
 
Kusifiwa anasifiwa yeye peke yake na halalamiki, kulaumiwa anataka washirikiane na CCM wote!
Kwa maana halisi ni kuwa anataka CCM wote wageuke kuwa "CHAWA" wake. Anapenda kusikia kila mwana CCM akiwa kama Lucas Mwashambwa; Tllaa tlaah, VoiceVariable na wengineo.
Anajuwa wazi kwamba yeye mwenyewe hana uwezo wa kujijengea sifa hata kwa kuuza mdomo tu mbali ya matendo ya uongozi wake.
Anataka asikie kila sehemu uzuri wa Samia ukiimbwa na kila mtu.
 
Vipi kuhusu Hawa Askari ambao wanaotuhumiwa kila siku kuua raia ?
Vipi kuhusu hao raia ambao wamekuwa wakifa wakiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi katika Vituo vya Polisi ?? Nao hawamhusu?
Vipi hao mateka ambao baadhi yao wameokotwa wakiwa tayari wameuawa kinyama? Nao hawamhusu??

Akumbuke kwamba yeye binafsi akiwa Kama Mkuu wa nchi hii kwa mikono yake ndiye aliyewateua hao Viongozi wote wa Serikali hii iliyopo, wakiwamo na Wakuu wa Majeshi ambayo wa-Tanzania wanayatuhumu kwamba yamekuwa yakihusika katika kuwateka raia na kisha kuwaua. Matendo yote yanayofanywa na hao Watu Wateule wake ni sawa sawa kabisa kwamba ameyafanya yeye mwenyewe Mteuaji binafsi. Kushindwa kwa hao Watu ambao amewateua ndio kushindwa kwake yeye Mteuaji. Kwa hiyo kwa namna yoyote ile kamwe hawezi akajitenga na matendo mazuri au mabaya yanayofanywa na Wateule wake.

Aidha, hata tuhuma anazotupiwa za kuhusika na tukio la jaribio la mauaji ya Tundu Lissu kule Dodoma yeye pia tuhuma hizo zinamhusu Moja kwa Moja. Rais Magufuli siyo Mtuhumiwa pekee wa shambulizi lililofanywa dhidi ya Tundu Lissu, hata yeye pia anahusika kwa sababu Serikali ya 'MaguSami' (i.e. Magufuli+Samia) ndio iliyokuwa madarakani wakati ule tukio hilo lilipotokea.
Rais wa JMT ana madaraka juu ya serikali yote, mihimili yote, na vyombo vyote vya dola. kiuhalisia yuko juu ya katiba na sheria. Hakuna uhalifu unaoweza kufanywa na vyombo vya dola bila ridhaa yake. Ikitokea hivyo kuna watu watakwenda na maji chapchap. Hatua kali zisipochukuliwa, basi ujue Rais ama KAKUBALIANA au KARUHUSU au hata KAAGIZA. Na akienda mbele na kutetea kinamna kama alivyofanya katika hotuba yake ya majuzi kwenye sherehe ya Jeshi la Polisi, asishangae akinasibishwa na mauaji yanayotuhumiwa kwa vyombo vya dola.

Huko nyuma tumeshuhudia ikitokea waliohusika na mauaji, mashambulizi na unyayasaji wa wapinzani, vyombo vya habari na wanaharakati wakipandishwa vyeo na Rais (sio huyu wa sasa). Hiyo ni indicator ya nafasi na uhusika wa Rais katika mambo haya.

halafu kauli ya kutoua mtu labda sisimizi sio njema sana (kisiasa) kwa mtu kama yeye. Ni kauli ya dharau/jeuri. Kifupi, hata kama anajua kuwa hakuna wa kumfanya kitu, ajitahidi kutulia, kusoma mazingira na kutafuta namna njema ya kuwasiliana na watanzania WOTE kwa busara na hekima. Asiwafikirie viongozi wa CHADEMA na "mabeberu" tu. Ataishia kuchangamkia vijembe na vichambo tu. Kuna Watanzania wengi sana wastaarabu walioanza kuwa na mashaka makubwa kule nchi na uongozi wake unakoelekea. Hawa anazidi kuwapoteza. Na sauti zao hazisikiki kama za machawa anao shinda nao. Bahati mbaya Tanzania hakuna opinion polls za kuaminika na uchaguzi hauna maana kama kipimo sahihi cha kukubalika kwa uongozi wa nchi.
 
Sidhani kama kuna mtu alikuwa anamtukana Magufuli kumshinda Mange kipindi chake.

Na uhalisia ni kwamba katika bloggers ambao wapo active kwenye ku-interact na followers wao MangÄ™ anaongoza.

Yeye mwenyewe imebidi akubali watanzania walikuwa wanapenda Magufuli na bado wanampenda; kwa jinsi wanavyo mshambulia akimsema vibaya. Imebidi anyooshe mikono kwa huyo mtu japo yeye amkubali kabisa mpaka kiama.

Sasa followers wa MangÄ™ ni watanzania wa kawaida, huyo mama anatakiwa kuelewa katika hotuba zake kwa watanzania kusema sijui tumetoka kwenye giza na yeye kaleta mwanga ajijengei kabisa kwa wananchi.

Kuna mambo ya kufirika na kuna uhalisia ambayo wananchi wanataka kusikia (ata kama yeye raisi anajua zaidi anachosema maana alikuwa jikoni) watanzania awataki kusikia shujaa wao akibezwa.
Sijui na wala sioni mantiki ya hoja hii.
Magufuli alikuwa na watu wake walio mpenda hata kama angefanya maovu ya namna gani; hali kadhalika, huyu Samia naye kama unavyoona mwenyewe, analo kundi lake la 'chawa', huwezi kamwe kuwaambia chochote juu ya Samia wakakusikia.

Lakini 'common denominator' kwa hawa wawili ni hiyo CCM ambayo ndiyo inayo husika na kuleta viongozi wabovu wa aina hii kuwaumiza waTanzania.

Kwa hiyo, kama ni hoja unataka kujenga kuhusu maumivu yanayo wakabili waTanzania wote bila kujali kiongozi aliyepo madarakani, ijengee hoja hiyo hiyo CCM. Kwa nini imekuwa ndio chimbuko la viongozi wa hovyo namna hii.

Sijazungumzia chochote kuhusu uzuri au ubaya wa vyama vingine vya siasa, kwa hiyo usikimbilie huko kujaribu kutetea ubovu tunao uona ndani ya hiki chama cha CCM.
 
Mungu wa Mbinguni azidi kukubariki mh Rais Samia 🌹


Tatizo ni hawa akina Mwagito Chalamila maelezo yao hawayanyooshi Sawa Sawa

Ila kiukweli hili swala la kushambuliwa Mwenyekiti ambaye ni Rais wa JMT halikubaliki kabisa!
Na ndiyo maana nikasema huenda wanaoua wanalengo la kumwangusha
 
Ujumbe wa 4R, Uchaguzi 2024 pia 2025, Matumaini, Utu kwa Wote na Amani kwa Dunia Yote Uliotolewa na Tanzania UNGA79
Kassim Majaliwa Majaliwa,Prime Minister Of The United Republic Of Tanzania, Addresses The General Debate Of The 79th Session Of The General Assembly Of The United Nations (New York 24-30 September 2024)
Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa wakati akihutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa la 79 jijini New York nchini Tanzania :


View: https://m.youtube.com/watch?v=tGE2Y4GwALY

Malengo endelevu na ushirikishwaji wa wote, utu wa mtu na watu wote, utatuzi wa migogoro, amani, ukosefu wa chakula .... haki kwa wote, uwajibikaji, Haki ya Kuishi ili Kufikia Matarajio yao yote msishani ni tamko Tanzania inasisitiza asema waziri mkuu wa Tanzania akihutubia Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa akimuwakilisha rais Samia Hassan katika kutano hilo muhimu la kila mwaka ....

Kuhusu uchaguzi wa November 2024 wa serikali za mitaa na ule uchaguzi mkuu wa 2025, waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa ameihakikishia Dunia na Jumuiya ya kimataifa kupitia mkutano wa UNGA 79 kuwa chaguzi zitakuwa wazi, huru na wa haki kwa vyama vyote vitavyoshiriki ...
 
Nyie watoto msio na baba ndiyo zenu hizo, tunawajuwa, akifa mtu ndiyo mnajitokeza kudai urithi. Alipokuwa hai mlikua wapi?

Hata jina umeshindwa kutaja.
Nashukuru sina Baba lakini nina utu, kumjali Faith Foxy ingawa simjui, lakini utu wake unathamani kubwa , kuliko urithi anaokimbilia Faiza Foxy
 
Back
Top Bottom