Pre GE2025 Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya

Pre GE2025 Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
mama,
Wewe ndio afande NAMBA MOJA HAPA.
maafande wako wa chini wakiua na Wewe umeua.
sababu wewe ndo mwenye amri ya kukataza haya mambo ya utekaji na mauaji.labda useme unawaogopa wakuu wako wa ulinzi.
Huyu mama namuhurumia mno kwakukutana na watanganyika ambao ni mafisi ambao wana lengo la kumvuruga mama wa watu ili aonekane mbaya
 
Hapana,ubaya ana utaka mwenyewe.
Ameharibu na bado anaendelea kuharibu.
Hitler tunasema kaua wayahudi milioni 6.haimaanishi waliuliwa kwa mikono yake .au hata amrita ya kuua inawezekana hajatoa.ila kwa kuwa mauaji yalitokea kipindi chake.
yeye ndiye anayetajwa.
hata kwa mama samia.
anatakiwa awe mkali kwa vyombo vyake.ajue baya lolote likifanyika yeye ana sehemu yake.maana yeye ndo kiongozi wa nchi.

Huyu mama namuhurumia mno kwakukutana na watanganyika ambao ni mafisi ambao wana lengo la kumvuruga mama wa watu ili aonekane mbaya
 
Kule Busega lamadi yale mauaji yamefanywa na nani?
Kule Geita sijui wapi mauaji yamefanywa na kina nani?
Hatua gani zimechukuliwa?
Ktk namna yoyote ile binadamu hapaswi kuumizwa wala kuuliwa kwa kujibu wa sheria.
Kama ni ktk kujihami askari anapaswa kutumia minimum force kama vile Maji ya washawasha au kama ni jambazi kupigwa risasi miguuni ili asiponyoke kwenye uangalizi wa askari au katika kujihami na sio kuua.
Watu wamepotea majibu hakuna,
Mzee kibao 😭😭🙆‍♂️🤦‍♀️
N.k.
Juzi kwenye hotuba ilitarajiwa kushinikiza wenye dhamana kuwajibika kwa kujiuzuru wenyewe au kuwatumbua,
Badała yake Eti wajuvi wanasema ni kana kwamba amekuja kuwasuta wananchi kuwakumbatia wanaopaswa kuwajibika kupisha uchunguzi huru na wa haki ??!!
 
Naunga mkono hoja, mtu mwenye wajihi kama huu, Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” hawezi hata kuua panya!, kama ni kuua labda mbu, mende na sisimizi.

Ila kwa vile yuko serikalini na yeye ndie mkuu wa serikali, na anajua kuna mazingira fulani, serikali zote duniani huwa zina waua watu hatarishi kwa usalama wa nchi, dissidents, na kabla hawa dissidents hawajauliwa lazima CinC asaini ile death warrant, then death warrant yoyote ikisainiwa, aliyeua ni aliyesaini death warrant na sio wale watekelezaji.

Ikitokea makosa ya watu wake kumuua kwa makosa mtu safi kwa kudhaniwa ni dissident, then the blood of that person is upon aliyetoa hiyo order kwa niaba yake.

Na kunapotokea vifo ambavyo vingezuilika kwa kufanya kitu lakini hakikufanyika, then damu iliyomwagika is upon yule ambaye angezuia lakini hakuzuia.

Hivyo tumeshauri Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!
P
Sasa sheria/mahakama kazi yake nini?
Maana hukumu zote zipo; miaka, maisha hata death penalty. Sasa Rais kusaini mtu auliwe wapi na wapi? Sijawahi kusikia
 
Magazeti ya kesho nisipoona hilo neno nyooo nitayashitaki yote kwa kumnukuu vibaya Mh. Rais maana wamezoea kupotosha.
 
Sifa zote kwa Rais,basi na lawama zote kwake pia,yeye ni binadamu na hakuna binadamu aliye mkamilifu kwa 100%. Mapungufu yake yakisemwa siyo kumkosea heshima bali ni kudhihirisha ubinadamu wake.
 
Mimi kwa upande wangu naamini maneno yake. Kinachoniumiza na kunisikitisha kwa nini manusura wanawataja watesi na wauaji wao hadharani kabisa na hawachukuliwi hatua zozote. Hii ni nini maana yake?
Na hiyo ndio inafanya watu wamhusishe yeye moja kwa moja kwakuwa mamlaka ya kuchukua hatua anayo lakini hatuoni akichukua.
 
You shameless leaders, when are you going to stop hypocrisy???
Vyeo visifanye mtu usahau vitabu vitakatifuu....
Si lazima kushiriki direct lkn hatakama unajua na unaficha na kutetea mauaji tayari umeshiriki mauaji hayo!!
Mtangulizi hakufanya direct ila alitetea kama anavyotetea mpokea kijiti huku akiuficha ukweli badala ya kuruhusu waovu wachukuliwe hatua stahiki yeye

You shameless leaders, when are you going to stop hypocrisy???
Vyeo visifanye mtu usahau vitabu vitakatifuu....
Si lazima kushiriki direct lkn hatakama unajua na unaficha na kutetea mauaji tayari umeshiriki mauaji hayo!!
Mtangulizi hakufanya direct ila alitetea kama anavyotetea mpokea kijiti huku akiuficha ukweli badala ya kuruhusu waovu wachukuliwe hatua stahiki yeye anawapa vyeo!!!

Even the truth can be deceptive , dah wanatukosea sana.
 
Tlaatlaah Lucas Mwashambwa ChoiceVariable mmesikia ujumbe wenu, mama anataka mjibu hoja sio kumsifia..
Na hicho ndicho tunachokifanya mimi pamoja na hao wangwana wazalendo muhimu sana kwa Taifa uliowatag. ChoiceVariable na Lucas Mwashambwa

Kazi yetu kwa niaba ya chama na wananchi ni kujibu hoja na kueleza kinagaubaga mama huyu kipenzi cha waTanzania Dr. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake sikivu ya CCM wanafanya nini kwa maslahi mapana ya waTanzania wote.

Hata siku moja huwezi kuta mimi au hata hao wangwana tunampongeza Rais bila kwanza kueleza kinagaubaga alichofanya kwaajili ya manufaa ya hawa waTanzania..

Kwa mfano,
Hembu angalia uzalendo, nia na dhamira njema ya mama huyu kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, leo alipaswa kuhutubia Baraza kuu la umoja wa Mataifa huko new York marikani, akaamua kung'ang'ana tu na kuwaletea maendeleo waTanzania wa Ruvuma na Songea.

Kweli tuache kumpongeza Rais kwa hilo mpendwa mtumishi Lamomy na hata haijulikani umekurupukia kutoka wapi maana ni kitambo hauko jukwaani?, real?🐒
 
Na hicho ndicho tunachokifanya mimi pamoja na hao wangwana wazalendo muhimu sana kwa Taifa uliowatag. ChoiceVariable na Lucas Mwashambwa

Kazi yetu kwa niaba ya chama na wananchi ni kujibu hoja na kueleza kinagaubaga mama huyu kipenzi cha waTanzania Dr. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake sikivu ya CCM wanafanya kwa maslahi mapana ya waTanzania wote.

Hata siku moja huwezi kuta mimi au hata hao wangwana tunampongeza Rais bila kwanza kueleza kinagaubaga alichofanya kwaajili ya manufaa ya hawa waTanzania..

Kwa mfano,
Hembu angalia uzalendo, nia nadhamira njema ya mama huyu kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, leo alipaswa kuhutubia Baraza kuu la umoja wa Mataifa huko new York marikani, akaamua kung'ang'ana tu na kuwaletea maendeleo waTanzania wa Ruvuma na Songea.

Kweli tuache kumpongeza Rais kwa hilo mpendwa mtumishi Lamomy na hata haijulikani umekurupukia kutoka wapi maana ni kitambo hauko jukwaani?, real?🐒
Unaponichosha ni hayo magazeti yako 😂😂😂
Nyie watu sio machawa ila kunguni mnang’ata kisha mnapotea
 
mzalendo ni huyu Afande wa guinnea

1727534964879.jpeg
 
Unaponichosha ni hayo magazeti yako 😂😂😂
Nyie watu sio machawa ila kunguni mnang’ata kisha mnapotea
hiyo ni Neema na Baraka za Mungu iliyo ndani yangu dhidi ya watu wa Mungu. Na ntaandika sana. Just imagine kuongea nakuaje sasa , hususani wakati wa kuhubiri au siasa?

utazoe tu mtumishi pole pole, maana maelezo hayo yana ambatana na maombi muhimu ya nguvu sana 🐒

ulikua wap kwanza, Roho Mtakatifu ananielekeza kwamba mmeongezeka. Hongera
 
Back
Top Bottom