Rais Samia: Simba alikuwa hatulii kama ‘Mwanangu Lissu’, ndio maana nikasema apewe jina hilo

'Simba abubujikwa machozi na kupata kiwewe kwa kumuona mpendwa rais Samia" - Lucas Mwashambwa.
 
👆
Chawa wajengewe uwezo zaidi, wawezeshwe, na wapate nafasi za uwakilishi bungeni.
 
Lissu ana uwezo mkubwa sana kiakili.

Hata kesho ukiwepo mjadala wa wazi wakakaribishwa Lissu na Samia kuchambua issue za mbalimbali za kitaifa mtajionea.

Samia ni mweupe mno kichwani na hii inajidhihirisha katika historia yake kitaaluma mpaka hapo alipofika hata huo udaktari wake ni wa kutunukiwa tu asingeweza kuupata kwa kuingia darasani na kwenye tafiti.

Pia Lissu katika eneo lake la ubobezi[sheria] anayo mengi sana ameyafanya ya kukumbukwa tangu 1997 kwenye kesi za madini Nyamongo ukiwa ni utawala wa Mkapa na kabla Lissu hajaingia kwenye siasa.

Kiufupi Lissu amefanya mengi sana na kuonyesha uwezo wake kitaaluma hata kabla hajaingia kwenye siasa!

Je Samia alifanya kipi cha kukumbukwa katika eneo lake la ubobevu kabla hajaingia kwenye siasa?
 
🤣🤣
 
..Samia asingekuwa Raisi nani angemtaja?

..Lissu anatajwa pamoja na kwamba hajawahi kuwa hata Mkuu wa wilaya.
 

Mods unganisheni huu uzi, habari moja iandikwe mara 10. Chawa Lucas Mwashambwa leo umechelewa, wenzio wamekuwahi, washatolesha watu machozi.
 
Ukweli ni kwamba Tundu lissu anamtisha sana Rais anampa hofu isiyo kifani,ndio tafasili ya yule Simba aliekuwa na ghadhabu.tulikuwa tunahangaika kujiuliza kwa Nini mama alitaka Simba yule aitwe jina la lissu sasa yeye mwenyewe katupatia majibu.
 
Anachoweza kukumbukwa lisuu ni mimameno yake ya ubaguzi, uchochezi na matusi tu.

Lakini Rais wetu amefanya mambo mengi ambayo hayawezi kufutika wala kufutwa na yeyote yule katika Taifa letu. Ni Mama Samia Rais wetu mpendwa ndiye amefanya Elimu kuwa bure kabisa hadi kidato cha sita.ambapo sasa watoto wanasoma kwa furaha na matumaini makubwa sana ya kutimiza ndoto zao.

Ni Mama Samia Rais wetu mpendwa ambaye ametoa maelfu kwa maelfu ya ajira kwa vijana kila mwaka tangia ameingia madarakani.ni Mama Samia amepandisha bajeti ya kilimo kutoka Billion 250 hadi Trilioni 1.2. ni Rais Samia Mama yetu Mpendwa ameweka rekodi ya kuzindua mradi wa treni ya mwendo kasi ,kukamilisha bwawa la mwalimu Nyerere ambalo alilikuta likiwa 34% .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…