lisuu ni nani kwanza ??Anachoweza kukumbukwa lisuu ni
Lissu kachochea nini?mimameno yake ya ubaguzi, uchochezi na matusi tu.
Lissu kambagua nani?
Mbaguzi ni nani kama sio Samia anayefukuza watu kwenye ardhi yao ya asili huku Lissu akikemea wazi ubaguzi huo sasa hapo mbaguzi nani?
Naungana na mchangiaji mmoja aliyeomba machawa mjengewe uwezo [capacity building] kwenye kujibu hoja baada ya kupandisha mabandiko na mpunguze hizo lullabies.
Yapi ?Lakini Rais wetu amefanya mambo mengi ambayo hayawezi kufutika wala kufutwa na yeyote yule katika Taifa letu.
Hebu orodhesha 10 tu!
Elimu bure sio kigezo mmechelewa sana na sikulaumu wewe sababu watanzania wengi exposure ni ndogo.Ni Mama Samia Rais wetu mpendwa ndiye amefanya Elimu kuwa bure kabisa hadi kidato cha sita.ambapo sasa watoto wanasoma kwa furaha na matumaini makubwa sana ya kutimiza ndoto zao.
Mimi nimewahi kutembelea nchi kadhaa elimu ni bure sababu inagharamiwa na kodi za wananchi na si kitu cha kumpa heko mtawala.
Usikute wewe licha ya kuwa Mbeya hujawahi hata kufika nchi jirani kama Malawi na Zambia tu .
Ajira zipi ?Ni Mama Samia Rais wetu mpendwa ambaye ametoa maelfu kwa maelfu ya ajira kwa vijana kila mwaka tangia
Unaweza kuweka takwimu hapa?
Maana vijana hao hao ndio tunaona humu wamegeuka kujiita "maafisa ubashiri" je kamari ni ajira rasmi,?
Malalamiko ya ajira yamo lukuki humu.
Hizi pesa anatoa wapi yeye kama rais?ameingia madarakani.ni Mama Samia amepandisha bajeti ya kilimo kutoka Billion 250 hadi Trilioni 1.2.
Hizo ni kodi na tozo wanazolipa wananchi ,rais hana hizo pesa na sio zake hivyo hastahili sifa yoyote hapo wapongezwe watu kwa kulipa kodi sio mtawala.
Kuzindua mradi nacho ni kitu cha kujisifia ?ni Rais Samia Mama yetu Mpendwa ameweka rekodi ya kuzindua mradi wa treni ya mwendo kasi ,kukamilisha bwawa la mwalimu Nyerere ambalo alilikuta likiwa 34% .
Hizo pesa za kugharamia mradi zimetoka wapi?
Nani watalipia gharama za huo mkopo wa kujenga hiyo miradi kama sio watumiaji wa mwisho ambao ni wananchi?
Samia tangu amezindua hiyo treni kapanda lini tena , mfano huko Kizimkazi alipokuwepo wiki nzima kwenye bonanza alienda na treni ?
Kuzindua sio jambo la kupongezwa hakuna sifa yoyote kwenye kuzindua bali wanaotakiwa kujipongeza ni wanachi kodi zao ndio zimejenga mradi huo uwanufaishe wao.
Je Samia mbona ameshindwa kudhibiti wizi ambao magenge ya wezi yanachepusha makusanyo ya kodi kwenda katika njia zisizo rasmi?
Au kwenye mambo ya wizi , ubadhirifu,matumizi mabaya ya ofisi sio uongozi wa Samia au huko Tanzania ni ya rais mwingine na sio Samia?